Wanaopinga mahakama Kadhi "Intellectual Arguments" only

Status
Not open for further replies.
Kwann isiweze ndo pakushangaza kenya na uganda kuna nn na hapa kuna nn.kwan uganda nchi ya kiislam mbona wako ois.kama kitu hakina madhara kwa din nyingine sion sababu ya kukatalia.weng wasio waislam hawajui mahakama ya kadh itafanya kaz vp ndo mana weng wanapinga

Umeshaambiwa Tanzania ni sovereign state, haijalishi Kenya na Uganda wao wanafanya nini.Ukiona huko kunakupendeza zaidi, basi unaweza kuhamia huko badala ya kutamani Tanzania ifanye kama wao.
 
Kwanza hakuna kitu kama ukubwa wa maili 362,000, huo ni urefu wa kamba au wa barabara. Pili, malipo ya wafanyakazi wa mahakama hizo hayawezi kuwa "kitu kidogo sana" wakati wewe mwenyewe umesema, msingi wa hoja yako ya kupinga mahakama hizi ni, "resources za ziada kutoka kwa walipa kodi." Kumbe hizo resources ni nini kama sio administrative costs ambazo kikubwa chake ni payroll and benefits?

Umenipatia hapo ehh!? Sawa nilikosea - but still it is approximately
364,900 square miles! Meaning that the country is vast.Ukiwa kama msomi ungeweza kusahihisha kisomi zaidi badala ya kuuliza kuwa ni urefu wa kamba.Nimesahihisha!

Nimezungumzia "resources za ziada" naamini unajua kuwa its more than admin costs, in particular payroll.... sijui kama unaelewa kuwa hata vyumba vya mahakama havitoshi pale penye mahakama, ukiacha mbali maeneo mengi yasiyokuwa na majengo ya mahakama.Hii inamaanisha resources za ziada ni pamoja na kujenga majengo ya kutosha au kuongeza vyumba, na kuviwekea vifaa, usafiri nk over and above personnnel who need to be tooled /retooled waweze ku respond to the needs.

Moja ya unpalatable aspects ya mahakama hizi ni kuongeza ukubwa serikali. Zilizopo zimeshatushinda, wafanyakazi kila kona ya nchi mishahara haitoshi au hawalipwi, sidhani kama unaweza ku minimize dimension hiyo ya costs.

Unaponda halafu unaunga mkono hoja! Nice one!
 
Tufanye HARAMBEE ya kusaidia kuanzisha mahakama ya KADHI, tuachane na hela za serikali maaana zingine ni kodi za pombe na kitimoto!
 
Kwahiyo kenya wakipeleka majeshi somalia na sis tupeleke?
Kwann isiweze ndo pakushangaza kenya na uganda kuna nn na hapa kuna nn.kwan uganda nchi ya kiislam mbona wako ois.kama kitu hakina madhara kwa din nyingine sion sababu ya kukatalia.weng wasio waislam hawajui mahakama ya kadh itafanya kaz vp ndo mana weng wanapinga
 
Assume wewe ni muislam na una wake watatu na watoto 5:4:3 yaani 12 jumla kwa wake watatu..umefariki

Kwa sheria za ndoa ya 1971; ugawaji wa urithi huo hauwezekani japo muislam huyu aliruhusiwa kuoa kiislam

Kwanini mali yake isigawanywe kiislam?? tunataka kadhi wawasaidie hao wanawake, watoto kuhusu mgawanyiko wa mali ya muumini huyu.. siyo voluntarily iwe sheria kabisa na hukumu itolewe na mahakama..ok

Ndio maana tunataka mahakama ya Kadhi..

NB: Naomba wale wenye hasira na uislam na waislamu watuache kwanza tuseme kwanini tunataka mahakama ya kadhi ili mtuelewe

Hivi hiyo serikali iliyo nadi kwamba wao ni makaafir, leo mnawaomba wawapangie utaratibu wa ibada? daah huo ni msiba mkubwa! yaani rejea yenu sio kolani, hadith ima sunna za mtume wako bali ni serkali iliyo nadi wao ni makaafir. ahahahaa kweli uislam uishie!
 
Hivi uislamu ni mahakama ya kadhi tu? Tena kwa ajili ya ndoa na mirathi tu? Uislamu kamili ndo unaishia hapo tu? Vipi kuhusu sharia law kwa ujumla wake kwani nini hiyo waislamu wa tanzania hawaidai?
 
"Jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza"
Jamani hiyo ya 10. ni kitu gani?maana sie wengine viingereza vyetu ni vya serikalini.

Nenda kajinyakulie nakala yako ya kiswahili ya 'kitabu kitukufu' fungua hiyo aya ujisomee mwenyewe kwa kiswahili. Lkn ukumbuke kukibusu kwanza maana maneno ya humo ndani ni matukufu yameshushwa toka kule inakotogeaga mvua.
 
Duh, naona hoja ambayo ni intellectual argument ni mbili
1. inayohusiana na gharama za kuendesha kesi katika mahakama ya kadhi!
2. Waanzishe waislamu pekee

Majibu:

1. Gharama za kuendesha kesi hizo ni vema zitoke serikalini kwakuwa kadhi courts itakuwa pia imepunguza kwa kiasi kikubwa kesi za waislamu zinazofanywa na mahakama za serikali (inabidi tufanye calculation ili tupate kiasi hasa ni kesi ngapi za waislamu kwa sasa zipo mahakamani ambazo zinatakiwa kupelekwa kadhi courts na gharam yake ni shilingi ngapi each case..tukipata tuna transfer kiasi hicho kadhi courts

2. Ni muhimu kuanzishwa kisheria ili watu walioamua kufuata sheria hiyo wakubaliane na hukumu ya kadhi, kama itakuwa haitambuliki kisheria itakuwa haina maana kwasababu itakuwa hakuna tofauti ni kutokuwa na mahakama..kutambulika ni jambo la lazima ili iweze kuitwa mahakama..lakini kuhukumiwa huko ni optional siyo lazima..lakini unapokubali mahakama hiyo lazima ukubali hukumu zake..ok

tuache jazba nataka intellectual arguments ok

J
 
Kanisa Katoliki linazo mahakama zake na zinahusiana na masuala ya Ibada, ndoa na talaka vile vile. Na zinaendeshwa na Wakatoliki wenyewe na wapo watu wamesomea sheria hizo na kuna mfumo wa rufaa hadi Vaticani. Maamuzi yake yanaheshimiwa na sheria za nchi zilivyo sasa na serikali haiwezi kuingilia maamuzi ya mahakama hizo. Zina majaji na mawakili na zinafanya kazi miaka nenda rudi na hazijahitaji hata mara moja kuingizwa kwenye katiba ya nchi au kutengewa fedha za serikali. Hakuna sheria yoyote iliyotungwa yenye kuzitambua mahakama hizi kwa sababu ni sehemu ya ibada ya Wakatoliki na hatuhitaji sheria ya Bunge kutambua ni sehemu gani ya ibada yetu ni halali. Ninaamini Waislamu wakianzisha mahakama ya kadhi na kuwa ni sehemu ya ibada yao hakuna mtu atawauliza.

Mahakama za kadhi zinaweza kufanya kazi kwa mtindo huu huu. Vinginevyo, na watu wa dini nyingine nao wakitaka kuanzisha mahakama yao inayogharimiwa na Watanzania wote itakuwaje; hatuna uwezo wa kuendesha mahakama za kidini. Binafsi ninaamini (nilishalionesha hili miaka karibu mitatu nyuma) kuwa Waislamu wanaweza kabisa kuendesha mahakama zao na wanaweza kutumia serikali kufanikisha hivyo kwa mfano.

a. Taasisi za Kiislamu ziunganike na kufanya mazungumzo na serikali (kitu ambacho tayari kinafanyika) jinsi ya kuendesha mahakama hizo.

b. Waislamu wote na watu wengine (kama wapo) ambao wangependa kuona mahakama ya kadhi inakuwepo wapewe nafasi ya kuchangia kwa kukatwa mishahara yao kila mwezi ili kujenga mfumo wa kulipia hilo. Serikali inaweza kukata mishahara ya watumishi Waislamu wote (au wenye majina ya Kiislamu) unless wakatae. Kwa mfano, kama kila mfanyakazi Muislamu akikatawa shilingi 20,000 kwa mwezi na tuseme wapo wafanyakazi 200,000 tu basi kwa mwezi the Kadhi Fund itakuwa na shilingi 4,000,000,000 (shilingi bilioni 4).

c. kwa vile si Waislamu wote wako kwenye ajira rasmi basi kila msikiti wa Tanzania utatakiwa kuwa na sadaka ya Mfuko wa Kadhi ambapo Waislamu watatoa wenyewe (sijui utaratibu wa kuchangia mambo ukoje) na kwa vile tumewambiwa hiki ni kilio cha Waislamu nina uhakika fedha nyingi tu zitaweza kupatikana kila wiki au kila mwezi kuchangia ule mfuko wa kadhi.

d. Waislamu wataweza kuajiri na kulipia gharama zote za mahakama ya kadhi, serikali inaweza kusaidia kuadminister mfuko huo (kwa malipo siyo kama hisani). Kwa mfano, kwa mfano kila makato yanayosimamiwa na serikali kutakuwa na gharama ya kama shilingi 1500. Hivyo, Waislamuw wanapata fedha za kuendeshea na serikali nayo inanufaika kwa kukusanya mapato.
 
Duh, naona hoja ambayo ni intellectual argument ni mbili
1. inayohusiana na gharama za kuendesha kesi katika mahakama ya kadhi!
2. Waanzishe waislamu pekee

Majibu:

1. Gharama za kuendesha kesi hizo ni vema zitoke serikalini kwakuwa kadhi courts itakuwa pia imepunguza kwa kiasi kikubwa kesi za waislamu zinazofanywa na mahakama za serikali (inabidi tufanye calculation ili tupate kiasi hasa ni kesi ngapi za waislamu kwa sasa zipo mahakamani ambazo zinatakiwa kupelekwa kadhi courts na gharam yake ni shilingi ngapi each case..tukipata tuna transfer kiasi hicho kadhi courts

2. Ni muhimu kuanzishwa kisheria ili watu walioamua kufuata sheria hiyo wakubaliane na hukumu ya kadhi, kama itakuwa haitambuliki kisheria itakuwa haina maana kwasababu itakuwa hakuna tofauti ni kutokuwa na mahakama..kutambulika ni jambo la lazima ili iweze kuitwa mahakama..lakini kuhukumiwa huko ni optional siyo lazima..lakini unapokubali mahakama hiyo lazima ukubali hukumu zake..ok

tuache jazba nataka intellectual arguments ok

J

Hoja zako hapo juu ni batili for the simple reason kwamba Tanzania is constitutionally defined as a Secular State, na kwa mantiki hiyo basi, Serikali/Dola haiwezi kujihusisha na shughuli zozote zinazopendelea au kuendana na imani fulani au yoyote ya kidini. Period.
 
acheni ushabiki na mahaba ya kipuuzi... Yaani hiyo hela atakayolipwa kadhi mnaiona nyingi sana kuliko hii hela wanayolipwa wafanyakazi wa serilkali wasiofanya kazi hata kidogo.. Wanakwenda maofisini kusoma magazeti na kunywa chai?? Wengine ni hewa hawako makazini lakini wanalipwa?? Acheni mahaba na ushabiki wa kidini..
 
Katiba na sheria zetu zimejengwa kwenye misingi ya tamuduni za mfumo kristo(judeo christian traditions , values and morals). Muslims demand for kadhi courts to address mirathi is surely not asking for too much. We must learn to give and take.
 
Sina uhakika kama atatoke mmoja wetu na kukuomba uthibitishe madai haya kwa kutumia katiba hii tulio nayo utaweza kuandika hata mstari mmoja. Kama utaweza basi nakuomba utupe ushahidi wa hizo values, traditions na morals ili nasi tufunguke.

Lakini pia jiulize wewe umefanya nini ili kupata katiba mpya isiyokuwa na mfumo wa kidini. Juzi tumeona uhuni bungeni na tumekaa kimya kwa kuaminishwa kuwa katiba italetwa na malaika wachache wanoishi kama wanadamu, halafu leo tunasema katiba imeandikwa kwa msingi wa dini fulani. Swali, unafanya nini ili kuhakikisha haindikwi na mfumo unaousema wewe.

Pili, kama suala la kadhi linahitaji serikali basi hakuna sababu ya kuunda chombo kingine. BAKWATA inatosha na labda ifanye utaratibu wa kumpata kadhi. Nina uhakika kwa maneno hayo wapo ambao nyongo zimewachemka matumboni na wengine wananiona
hayawani

Nina sababu za msingi, ya kwamba madai mengi ya waislam ni kuwa BAKWATA ni chombo cha serikali na kinafadhiliwa na serikali ili kuhujumu uislam.Kumbu kumbu zangu zinanionyesha kuwa Sheikh mkuu kwa nyakati hizo(sijui sasa) alikuwa anapewa nyumba na serikali ikiwa ni pamoja na usafiri. Hii labda ndio sababu inayopelekea wengi kuamini BAKWATA ni chombo cha serikali pamoja na madai mengine.

Unapoomba mahakama ya kadhi ihudumiwe na serikali, hapo tayari umeshaingia katika mfumo wa serikali. CAG itabidi akague fungu linafanyaje kazi na kama kuna ubadhirifu basi wahusika watafikishwa mbele ya sheria na wizara kama ya fedha zinatingia.
Ikifika hapo tutasikia madai kuwa serikali inainglia mambo ya dini na maandamano. Ikumbukwe kuwa serikali siku zote ni taasisi inayokuwa 'Regulated' na hivyo itaweka regulations kwa mujibu wa sheria. Hiyo mahakama inayodhaniwa itakuwa huru haitakuwa huru kwasababu mkono wa serikali umeingia kama ulivyoingia BAKWATA kwa makusudi au kwa uhalali na kisheria.

Tatu, kama ndoa inayofungwa na sheikh popote inakubalika na makubaliano ya jinsi gani ifanyike ni kati ya wana ndoa na sheikh wao, na kuwa serikali inatambua hivyo kwanini asiwepo kadhi ambaye kisheria anatambuliwa (labda jina la kadhi ndilo linahitajika) ashughulikie masuala hayo? Kama yupo anayekataa uwepo wa kadhi basi aniulize nimthibitishie.

Nne, kama waislam wanaweza kuhudumia misikiti na miradi yao kwanini iwe tabu kupata chanzo cha fedha kumhudumia kadhi.
Na ikumbukwe kuwa kama sheikh anavyofanya mazishi ya mtu kwa imani au kumfungisha ndoa au kusuluhisha mgogoro ndivyo kadhi anatakiwa aendeshe shuguli zake kwasababu ni sehemu ya ibada. Ima atawezaje kujikimu hilo linabaki suala la waumini husika kama wanavyoweza kumhudumia sheikh, kulipa bili za umeme na maji n.k. Ni kwa njia hiyo pekee waislam wataweza kuwa na vyombo vyao huru.

Tano, hoja na umuhimu wa kadhi ubaki kwa mantiki yake. Usifanywe kama simba na Yanga kwasababu hiyo ina 'adulterate' mamlaka na hadhi ya kadhi. Kazi ya kadhi sio mirathi ya kugawa mali. Kadhi anashugulikia mambo yote yanayohusu sheria ikiwa ni pamoja na mahusiano ya ndoa na kutafsiri sharia kama zilivyo. Ndiyo maana katika enzi za zamani ni makadhi waliokuwa na hadhi ya kuwashauri waumini wao juu ya tafsiri za ibada kama mfungo wa Ramadhani n.k.
Kufanya kazi ya kadhi ni kugawa mali(ambazo pengine hazipo) ni kutoelewa nini maana ya kadhi kunakochangiwa na kukariri maneno

Mwisho, suala la kadhi ni nyeti na lenye mantiki na hekima zake. Linatakiwa lishugulikiwe na watu wenye weledi wa hali ya juu. Kuliacha mitaani lizagae zagae na kila mmoja kuliandikia anachofikiri linapoteza mantiki kwasababu tu wapo waliokaririshwa kutoa hoja lakini hawawezi kuzitetea. Hoja ya kadhi inahusu imani na uhuru wa kuabudu na sio suala la fulani anapata hiki basi wale nao wapewe kile.
Sio suala la kugawana mali ni suala la kufuata sharia katika mambo ya kijamii ili kuleta utangamano katika ibada.
 
Umeshaambiwa Tanzania ni sovereign state, haijalishi Kenya na Uganda wao wanafanya nini.Ukiona huko kunakupendeza zaidi, basi unaweza kuhamia huko badala ya kutamani Tanzania ifanye kama wao.
............ bado huna hoja ya ushawishi ! Hukumu za kesi wakati mwingine Majaji huzitoa kufuatia reference ya kesi nyingine, huongozwa na busara na mazingira ya kufanana na tukio ua kesi husika. Hili liko pia katika ushahidi, ambapo Wakili unaweza kujenga hoja (Authority) kufuatia maamuzi ya kesi fulani inayofanana na hiyo na Jaji akashawishika na kutoa hukumu (hata kama kesi ni ya 1920 !). Hivyo bado Mifano ya Kenya na Uganda matters ! Mbona Wakoloni wa Kiingereza walikubali hii Mahakama ? hebu onyesheni threat, yaani ambaye hahausiki atapoteza nini ? Ndio maana mleta mada alileta angalizo la "Interllectuals" hivyo fuata ushauri wake kwenye kujenga hoja !
 
Mimi mpagani nakatwa kodi ili iendeshe shughuli za serikali........sasa wewe unataka kodi yangu iendeshee mahakama yako ilhali mimi sio mwislamu?
 
Watu hatuna hata hospitali nyie mnadai kitu ambacho wala hakina umuhimu
.............. kipimo chako cha kukosa umuhimu ni kipi ? kwa mfano katika mirathi husika "Mrithi" halali, amelazimishwa kugawana mali ya ziadi ya Tsh Mil 500, na mtoto wa nje, ambaye baadae inakuja kuthibitika huyo mtoto hata DNA hazikubali hilo unalionaje ?! Mtoa mada amesisitiza wachangiaji wawe Interllectuals, hilo umezingatia !?
 
Mimi mpagani nakatwa kodi ili iendeshe shughuli za serikali........sasa wewe unataka kodi yangu iendeshee mahakama yako ilhali mimi sio mwislamu?
............hiyo kodi unalipa peke yako ? hakuna watu wa imani nyingine wanaolipa ? hiyo mahakama itachukua % ngapi ya kodi katika kuiendesha !
 
Prof Kasamanda, did you know "two wrongs never make it right"?, kama unajua kuwa wafanyakazi wa serikali wanalipwa pasi kufanya kazi unaona mbadala wake ni hela hizo apewe kadhi?, nenda shule ukajifunze kujenga hoja.

Back
Top Bottom