Wanaopinga mahakama Kadhi "Intellectual Arguments" only

Status
Not open for further replies.
Topical anatetea ajira yake jamani, yumo kwenye list ya makadhi pamoja na vile vizee vinavyoshinda kwenye mabao na kahawa na kuoa wake wengi, wanataka warambe ajira serikalini kilaini bila jasho la kufuta umande

This is not intellectual arguments ok??
 
@shizukan
Wanawake waislam wanapenda hukumu za kiislam sana tu, na katika jamii inayoongoza kwa kuingia katika haki ni wanawake duniani ..

naomba ujibu yale maswali with intellect, siyo ushabiki bearing in mind tuna waislam 50% in Tanzania ok
 
Kwa sheria za ndoa ya 1971; ugawaji wa urithi huo hauwezekani japo muislam huyu aliruhusiwa kuoa kiislam
Topical, hiyo sheria ya ndoa ya 1971 inasemaje hapo, na kwa nini haiwezekani kwa mujibu wa sheria, in other words, kipengele husika ni kipi ambacho hakiwezekaniki kuwa applied katika mazingira hayo?
 
@shizukan
Wanawake waislam wanapenda hukumu za kiislam sana tu, na katika jamii inayoongoza kwa kuingia katika haki ni wanawake duniani ..

naomba ujibu yale maswali with intellect, siyo ushabiki bearing in mind tuna waislam 50% in Tanzania ok
Yaani unataka kutuaminisha wanawake wa kiislamu wanapenda sheria za kiislamu za kuwazuia kuendesha magari na kuwazuia kupiga kura?
Kuna some hidden Agenda hapa.
 
Assume wewe ni muislam na una wake watatu na watoto 5:4:3 yaani 12 jumla kwa wake watatu..umefariki

Kwa sheria za ndoa ya 1971; ugawaji wa urithi huo hauwezekani japo muislam huyu aliruhusiwa kuoa kiislam

Kwanini mali yake isigawanywe kiislam?? tunataka kadhi wawasaidie hao wanawake, watoto kuhusu mgawanyiko wa mali ya muumini huyu.. siyo voluntarily iwe sheria kabisa na hukumu itolewe na mahakama..ok

Ndio maana tunataka mahakama ya Kadhi..

NB: Naomba wale wenye hasira na uislam na waislamu watuache kwanza tuseme kwanini tunataka mahakama ya kadhi ili mtuelewe

Ndio maana Tanzania haina sheria moja ya mirathi: ziko tatu - ya jadi/customary ( wanaopendelea mila zao zaidi), za kidini ( kwa waislam) na Indian Succession Act 1865!( imeazimwa na kutumika toka Ukoloni). Sasa Waislam wanatakiwa kutumia hiyo sharia yao ndani ya mfumo wa kimahakama.Kwanini wasidai kuboreshwa mfumo huo kama kuna mapungufu, na badala yake watake mfumo parrallel utakaohitaji resources za ziada kutoka kwa walipa kodi ambao wengine siyo waislam?Mimi sioni kwanini Watanzania wasio wasilam kulazimika ku support mfumo wa kidini ambao hauwahusu.
 
Nimeuliza tatizo lenu nini hasa?
Kama ni fedha serikali inalipa mahakimu sasa kwa kuendesha kesi za waislamu
ambazo wanakosea sana hukumu

Kwa hiyo kukiwa kadhi hela hiyo hiyo inayotumika sasa ndio itatumika ok

usiwe na wasiwasi na hela ok..

naomba solution ya mambo haya niloyaeleza hapo juu..

Nimevutiwa na hii mada hasa kwa vile umeweka angalizo kuwa ni "intellectual arguments' !! Lakini hadi sasa sijaona u -intellectual wowote zaidi ya mtizamo mwepesi mno kwa ishu very serious!
Nitaendelea na intellectual argument anyway kama ifuatavyo:
Mahakama siyo mshahara tu... ni mambo mengi sana ndugu yangu! Mshahara mbona ni kitu kidogo sana?
Waislam hawako mjini tu wako nchi nzima.Utahitaji network ya kutosha.Tanzania ina ukubwa wa maili 362,000! Population more than 40m.Unafikiri tatizo ni mshahara wa mahakimu tu? Ungependekeza kwa mfano, wanasheria waislam "wajitolee kubobea" kwenye Islamic/Mohamedan Law ILI HATIMAYE WAPANGWE KUSIMAMIA HIZO SHERIA na tafsiri sahihi ili mridhike.Ujue kuna non-muslims wamebobea kwenye hizo sheria lakini kutokana na huu ubaguzi ulioibuka karibuni sidhani watakuwa wa msaada sana.
 
Ndio maana Tanzania haina sheria moja ya mirathi: ziko tatu - ya jadi/customary ( wanaopendelea mila zao zaidi), za kidini ( kwa waislam) na Indian Succession Act 1865!( imeazimwa na kutumika toka Ukoloni). Sasa Waislam wanatakiwa kutumia hiyo sharia yao ndani ya mfumo wa kimahakama.Kwanini wasidai kuboreshwa mfumo huo kama kuna mapungufu, na badala yake watake mfumo parrallel utakaohitaji resources za ziada kutoka kwa walipa kodi ambao wengine siyo waislam?Mimi sioni kwanini Watanzania wasio wasilam kulazimika ku support mfumo wa kidini ambao hauwahusu.

Na hii nayo sio intellectual argument,kwani hayo mapesa ambayo leo serikali inapatia makanisa kwa kuendeleza makanisa na mashule yao...!!hizo kodi na wakristo pekee!!!sijui kwa nini nchi hii viongozi wandamizi wengi wao ni legelege wanashindwa hata kuamua mambo mengi madogo madogo ambayo yanaweza kuleta machafuko ya kidini.
Vipi kuhusu kenya,nchi ambayo takwimu inaoneshwa wengi ni sio waislam lakini wakristo wamepiga kelele lakini govt wamerudisha tena kwenye katiba mpya.Hii nchi bwana...kwisha kabisa,kila kitu ni siasa,kila kitu udini....!
 
Kwanini msianzishe mahakama hiyo kama waislamu? Sioni ni kwanini mnapoteza muda mrefu kwa majadiliano ambayo jibu lipo just withini your reach. Mkiamua, hata leo mtaanzisha mahakama ya kadhi. Tatizo ni kutaka kila mtu ahusishwe na mahakama hiyo wakati wengine wala hatujui hata huyo kadhi anafanya nini
 
Kama hawataki kwenda mahakama hizi za kawaida (kwasababu za imani yao na wao ni watanzania) tuwafanyeje?? acha ushabiki nataka intellectual arguments

Swali langu lina maana. Wewe umekuwa possessed na mahitaji yako ya ndoa kiasi sasa unaona kila anayepinga ni mbaya. Kama hawataki kwenda mahakama za kawaida basi na wawajibike kujenga hizo wanazotaka. Ukiona msosi wa shule ni mbaya unatoa hela yako mfukoni kununua unaoona mzuri hotelini, au wewe unaonaje bwana kidume?

Wewe ni intellectual? If you are, then we are done.
 
@shizukan
Wanawake waislam wanapenda hukumu za kiislam sana tu, na katika jamii inayoongoza kwa kuingia katika haki ni wanawake duniani ..

naomba ujibu yale maswali with intellect, siyo ushabiki bearing in mind tuna waislam 50% in Tanzania ok

Wale waliolelewa kinyonge na kunyimwa nafasi za elimu na ufahamu. Wale walioenda shule hawatataka hii kitu. Wewe ndio shabiki tena mbaya zaidi unashabikia kitu kisicho na manufaa. Jibu ni rahisi: watagawana kwa utaratibu waliokubaliana.

Ngoja nikusaidie jambo wewe usiyependa kufikiri. Kama mtu ni muislamu, maana yake anafuata kanuni na imani ya dini. Kufuata kanuni na imani maana yake ni kwamba, atazingatia taratibu za ufanyaji wa mambo kwa mujibu wa kiislamu. Ikiwa, mtu hafuati mambo ya mirathi kwa taratibu za dini, (na kwa kuwa dini ni hiyari ya mtu) basi mtu huyo na asipelekwe mahakamani kwa kuwa hajamkosea mtu bali Mungu. Lah uniambie Mungu wako hana uwezo wa kuwaadhibu watu wake mpk wewe ndio uchukue jukumu hilo. Na mimi nitatafsiri kama ulazimishanaji wa mtu kufanya mambo asiyoyataka kwa jina la imani. Imani gani ya kuamuliwa na mahakama badala ya mtu kuamua kwa kadiri anavyotaka mahusiano yake na Mungu wake yaboreke?

Nakupa mfn: Ikiwa wewe ni mwanachama wa kikundi fulani, lets say cha michezo. Chama kimeweka taratibu kuwa ili uanachama wako uwe hai yakupasa kuhudhuria vikao la hasha ukikosa vikao vitatu uanachama wako u mashakani. Je, usipohudhuria vikao utapelekwa mahakamani kulazimishwa kuhudhuria vikao au chama kitaacha tu kukutambua kama mwanachama?
 
Na hii nayo sio intellectual argument,kwani hayo mapesa ambayo leo serikali inapatia makanisa kwa kuendeleza makanisa na mashule yao...!!hizo kodi na wakristo pekee!!!sijui kwa nini nchi hii viongozi wandamizi wengi wao ni legelege wanashindwa hata kuamua mambo mengi madogo madogo ambayo yanaweza kuleta machafuko ya kidini.
Vipi kuhusu kenya,nchi ambayo takwimu inaoneshwa wengi ni sio waislam lakini wakristo wamepiga kelele lakini govt wamerudisha tena kwenye katiba mpya.Hii nchi bwana...kwisha kabisa,kila kitu ni siasa,kila kitu udini....!

Tumia akili moja kuelewa mambo mengi. Mahospitali na shule ni kwa ajili ya jamii yote lkn mahakama ya kadhi ni kwa ajili ya mambo yenu binafsi. (hivi ni kweli huoni tofauti au mnaleta makusudi hapa).

La pili kaa ukijua Tanzania ni Jamhuri kwa hiyo haiendeshwi kwa mujibu wa Kenya inaendeshwaje. Na ndio maana kule Kenya mirungi inauzwa hadharani Mombasa huku hapa Tanzania ni mihadarati ambayo ukikamatwa nayo unashtakiwa. Kama unavutiwa na Kenya, hamia huko.
 
Guys, hapa si suala la Mahakama ya Kadhi kama ilivyo. Waislamu tunahaki ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi, but kinachopingwa, naomba ifahamike ni kuhusu kuihusisha Serikali katika mchakato huo. Serikali haiwezi kutamka kuwa mahakama ya Kadhi ianzishwe au isianzishwe! La pili linalopingwa kisheria ni namna mahakama ya kadhi itakavyoingiliana mamlaka na mfumo wa mahakama zilizopo kiserikali.

Kwa hiyo basi;

Iwapo kwa Waislamu mahakama ya kadhi inahitajika katika mfumo wa Dini, ni ruksa kuianzaisha, lakini Kikatiba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haina Dini na hivyo haitajihusisha na masuala ya Dini mija kwa moja, kama katika uanzishwaji wa Mahakama hiii muitakayo.

Pili,kama mnaitaka mahakama hii ianzishwe, basi ianzisheni kwa kutumia uhuru wa kuabudu( Freedom of Religion/Freedom to Worship). Na ianzishwapo, ni lazima muhakikishe kuwa haiingiliani na mfumo wa Sheria za nchi hasa katika mpangilio wa mahakama(Court's Hierachy). Kwa mfano inazishwe kama ni ngazi ya usuluhishi awali wa masuala yahusuyo Uislamu, kwa maana ya kwamba jambo litasuluhishwa kwanza huko, ikishindikana ndipo mtu aende mahakamani.

Zaidi ya namna hizo mbili, mahakama ya Kadhi muisahau katika Tanzania, labda katiba itakapoandikwa upywa, suala hili likiwekwa katika katiba,la sivyo; ieleweke kwamba kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini ni unconstitutional and hence an illegal concept. That is why JK amefeli kuitimiza,japo aliwaahidi kulishughulikia,si aliwajibu?

Being intellectual ni pamoja na kuzielewa vizuri sheria za nchi unayoishi. What sort of an intellectual are you that you dont?

Nawasilisha.
 
Pelekeni watoto SHULE achana na mambo ya URITHI na Madrasa!

Urithi pekee kwa mtoto ni ELIMU na siyo Majumba na Magari - Wakimaliza kukutia kwenye sanda wanayauza na wanakwenda BAR kunywa na kufanya mambo ya namna hiyo! kha!!
 
Kama hawataki kwenda mahakama hizi za kawaida (kwasababu za imani yao na wao ni watanzania) tuwafanyeje?? acha ushabiki nataka intellectual arguments

njia nzuri ya kutoa urithi ni kwa wosia, sio waislam tu wenye watoto wengi kwa mama tofauti bali hawawezi kudai serikali iwaanzishie mahakama ha kugawa mirathi- wengine wana mifumo thabiti na hawateteleki. Sijaona kundi au jamii iliyopinga kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi bali watu wanaona waislam wanataka kujiingiza katika utumwa wa mambo yao ya kiimani kusimamiwa na serikali. Siamini kama miaka yote hii waislam hawajawahi kutoa miradhi sawia na imani yao, kama hawajawahi na wanataka serikali iwaanzishie itakuwa ni aibu na fedheha kubwa.
 
Kama swala hapa ni kuanzisha mahakama ya kadhi kwa lengo la urithi eti waislamu wanaoa wake wengi hiyo ni sababu dhaifu sana maana swala la urith pale mtu anapokufa liko mikononi mwake kabla ya kufa si anaandika usia na kama hakuandika kuna hati za ndoa zitakozowatambua wanawake aliowaoa na kwa hali hiyo watoto wote watakuwa na haki sawa juu ya urithi ,kama mwanzilishi wa hii mada anahitaji ushaidi juu ya hili aisome shahada ya ndoa jinsi ilivyotofautisha aina za ndoa.

Tunahitaji wenzetu mtambue kuwa msimamo wa Tanzania ni ule ule maswala ya dini yanabaki kwenye dini siyo serikalini.
Hili swala la mahakama ya kadhi linakuzwa mno na wale wanaotaka urais chini ya Membe ambaye anajitahidi sana kuliendeleza lakini hawezi kushinda hata siku moja
 
Nchi hii aiendeshwi na Sharia, so mahakama ya kazi haikubaliki.
 
si muunde? kwani serikali imewakataza?

halafu kwa nini msilee watoto kwa misingi ya kujitegemea na si kutegemea urithi? unless ufe watoto waje wadogo,na unaishi na wake zako wote nyumba moja
 
Sophia Kawawa (RIP) alikuwa muislam, arithubutu kutoa kauli kuwa dini ya kiislam ilikuwa ilipoka haki za wanawake kwa kuruhusu ndoa za wake wengi- zanzibar waliandamana kupinga kauli yake.
Yaani unataka kutuaminisha wanawake wa kiislamu wanapenda sheria za kiislamu za kuwazuia kuendesha magari na kuwazuia kupiga kura?
Kuna some hidden Agenda hapa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom