Hata wanawake waliosoma wanajua kujishusha mkuu, sema hujakutana nao labda. Tatizo wanaume kuna wakati tunapenda kutumia mfumo dume hata pasipo kuwa na sababu. Wale wanawake wanaojishusha hata kama wewe mwanaume unakosa ni kwa sababu they are economically dependent. Haya mambo tulikuwa tunayaona hata kwa walezi wetu, unaona kabisa hapa mwanamke kaonewa lakini kwa sababu mwanaume ndio kila ndio kila kitu basi mwanamke ananywea.
Kuna mfano mdogo tu ninao, juzi juzi kuna ndugu yangu ambaye ni mdada kaja kunilalamikia, anasema bwana ake anamwambia asiende kanisani siku ya katikati ya wiki, awe anaenda jumapili tu, sababu hatoi. Cha kushangaza huyu mdada anayemwambia amempita elimu mbali sana, sasa unategemea nini siku akija react unatasema elimu imememfanya areact, mwanamke yupo commited na dini,wewe bila kumpa moyo unamkandamiza.
Nyingine ni mke na mume, ndoa ya juzi tu hapa. Mwanamke analalamika mumewe anashinda baa mpaka saa 7 usiku kila siku. Akitoka kazini anafikia baa, na huyu pia mkewe ni msomi mzuri tu kumzidi yeye. Akija kureact baadae utasema kwa ajili ya usomi wake.
Ninachosema hivi upu.....mba.......vu wa binadamu awe mwanamke au mwanaume hauna uhusiano na elimu. Mimi naishi uswahilini nawaona wake za majamaa walisoma na huku wake zao wakiwa hawana elimu, wake zao wanaburuzwa tena kweupe hadi kwenye magari tena mita 120 toka wanapoishi na mumewe. Tena wanaburuzwa vijana ambao ni jobless forever, anasubiri baba yake amuwekee pesa kwenye meza.