Wanaomwangusha Rais Magufuli katika Sekta ya Afya hawa hapa

Wanaomwangusha Rais Magufuli katika Sekta ya Afya hawa hapa

Praise team; come up in the open. Where are you? Ndege, bwawa la nyerere, fly-overs, barabara za lami, n.k. zinamsaidiaje "directly the grass-root person?" Maendeleo ni watu na siyo vitu (alisema baba wa Taifa).
Huduma za afya ni muhimu sana kwa watu wa chini,ndiyo maana Magufuli anajaribu kuiboresha lakini bado wapo watu/taasisi chache zimekuwa kikwazo.
 
Baba yangu alikuwa hoii taabani tukampeleka hosp ya rufaa ya mkoa wa Morogoro. Nilichokishuhudia Mungu anajua. Tulinunua mpaka canula tena wametuandikia kwenye form ya bima ya afya wangali wakijua hawana. Yale maduka ya dawa pale nje yanafanya bishara. Tulifanikiwa kumtoa pale siku iliyofuata na kwenda Muhimbili ambako hali ni tofauti utadhani si Tanzania moja. Mungu atusaidie kwa kweli.
 
Pole sana, kwa kweli huduma katika hospitali zetu bado zipo chini sana,yaani salama yako ni kuomba kutougua.
 
umeacha kusema kuhusu fedha toka HSBF kwenda vituoni kuwa hazipelekwi kwa wakati.
 
Mifumo mingi ya Taasisi za serikali ni mibovu plus UTOPOLO na Njaa za Watendaji wake.

Hata kama utakuja na namna nzuri ya kuboresha, utaambiwa eti sheria na kanuni haziruhu
 
Pole sana, kwa kweli huduma katika hospitali zetu bado zipo chini sana,yaani salama yako ni kuomba kutougua.
Asante sana ndugu yangu. Kuugua hakuepukiki waboreshe tuu huduma katika hospitali zetu za mikoa na wilaya. Fasa na vifaa tiba ni changamoto.
 
Kabudi atakuja kutoa ufafanuzi hayo unayolalamikia
 
Naungana na wewe Mifumo ya taasisi mbalimbali ndiyo inayozirotesha utoaji wa huduma ikiwemo kufanya kazi kwa mazoe, na kuondoa mfumo inahitaji muda kidogo naimini Mh. Raisi analijua hili ni swala la muda Raisi wetu ni msikivu sana.

Tumeona maeneo mengi alipo tumia vijana as top sayers or leaders mambo yameende kwa kasi sana ni kwa sababu vijana wanahari na wengi hawako affected na mifumo ukiachia wachache ambao walishakuwa kwenye mfumo tayari. Hii inadhihirisha kwamba kama taasisi nyingi zitakuwa na new blood basi kero nyingi zitatoweka. Kwenye issue ya risiti za EFD huko ni balaa zaidi kunahitajika elimu ya kutosha sana hasa kwa raia maana siku hizi ni kama hazitolewi kabisa na usipodai ndio kabisa.
 
Umechambua vyema kabisa
 
umeacha kusema kuhusu fedha toka HSBF kwenda vituoni kuwa hazipelekwi kwa wakati.
Fedha za basket fund zinatolewa na mabeberu,sasa sijui uchelewaji unatokea katika level ipi kati ya beberu na level ya wizara(wizara ya afya+tamisemi).
 
Hakuna kumung'unya maneno hali ya vituo vya kutolea huduma za afya (dispensary, vituo vya afya na hospitali) vya serikali vipo taabani katika kuhudumia wanyonge. Dawa hakuna, mabomba ya sindano hakuna, gloves hakuna etc, kiufupi hali ni mbaya sana.

Kiufupi wanaochangia huduma mbovu katika vituo vya kutolea huduma vya serikali, hivyo kumwangusha rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli ni wafuatao.

1. MSD (hawana ubunifu, kazi yao kubwa ni ufisadi, wamebaki kusingizia ya kwamba serikali hawapatii fedha. Shida ni kwamba hata hicho wanachopewa na serikali bado kinaishia kwenye matumbo ya watu. Pamoja na kupelekwa Mjeshi kuisimamia MSD, bado hawezi fanya kitu,sababu matatizo ya MSD ni ya kimfumo. Napendeka/ nashauri MSD ifumuliwe yote.

2. Waganga wakuu wa Wilaya/mikoa: Hili ni jipu kubwa sababu asilimia kubwa hawana ubunifu na pia kuwa wagumu kukubali mabadiliko ili kuendana na wakati. Kwa mfano kuna ushahidi wa kutosha ya kwamba ufungaji wa mashine za kielectronics zinasaidia kuongezeka kwa mapato ya serikali, lakini bado asilimia kubwa ya waganga wakuu wa wilaya wameshindwa kufunga mashine hizo katika vituo vya kutole huduma, hivyo kupelekea mapato kuendelea kuwa chini sana.

Sambamba na hilo pia bado kuna asilimia kubwa ya waganga wakuu wa wilaya/mikoa hawana uwezo wa kuongoza na ubunifu aidha kwa sababu hawakuzaliwa hivyo au hawana elimu sahihi kuhusu vipengele hivyo."Wengi wao kazi yao kubwa ni kusoma na kupitisha mafaili ya watumishi." DMOs na RMOs msisingizie mazingira magumu ya kazi, ugumu huo nduo ulifanya mkapewa nafasi hizo ili mpambane kuondo ugumu huo.

3. BIMA YA AFYA (NHIF); Hili nalo ni jipu kubwa, wamekuwa wakivitesa sana vituo vingi vya kutolea huduma serikali kwa kuvilipia malipo madogo uku wakisingizia kwamba vituo vy a serikali vinajaza fomu vibaya. Taarifa za kuaminika toka kwa wadau ni kwamba NHIF kwa kiasi kikubwa wanalazimisha makosa ili mwisho wa siku walipe kiasi kidogo kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma ( makosa mengi ya ujazaji wa fomu hayana uhalisia). Tunaambiwa NHIF wanafanya hivyo ili wabaki na fedha nyingi sababu mojawapo kupata fedha za kulipana posho.
...................................................................................................................
Niishie hapo kwa leo, nina hasira sana huduma mbovu zimempoteza jamaa yangu juzi kisa hakuna dawa.
Uchunguzi wenye malengo ya kuboresha na kuwatoa wahujumu ufanyke. Majungu yasiwe ni kigezo cha kuonea mtu
 
Uchunguzi wenye malengo ya kuboresha na kuwatoa wahujumu ufanyke. Majungu yasiwe ni kigezo cha kuonea mtu
Bila shaka kazi itafanyika kwa weledi, ili kufikia lengo la kuwa na Tanzania yenye wananchi wenye afya bora.
 
Kwenye kampeni za uchaguzi mwaka huu, kero nyingi zitakazoibuliwa na wanachi, ni huduma mbovu za afya.
 
Fedha za basket fund zinatolewa na mabeberu,sasa sijui uchelewaji unatokea katika level ipi kati ya beberu na level ya wizara(wizara ya afya+tamisemi).
Kumbe mabeberu wanatufaa sana,
Mwaka huu hali imekua mbaya sana kwa fedha za HSBF,robo ya mwisho hola mpaka mwaka umepinduka alafu mwanasiasa anasimama jukwaani eti wananchi wasikose dawa waendapo vituo vya tiba vya serikali.
 
Poleni sana.
 
NHIF ni jipu zito, kuwa na bima ni kama mzigo, ukienda hosp ni kusumbuliwa tu, oh sijui mtandao haupo sijui nn
 
Back
Top Bottom