Wanaomwangusha Rais Magufuli katika Sekta ya Afya hawa hapa

moesy

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
3,555
3,529
Hakuna kumung'unya maneno hali ya vituo vya kutolea huduma za afya (dispensary, vituo vya afya na hospitali) vya serikali vipo taabani katika kuhudumia wanyonge. Dawa hakuna, mabomba ya sindano hakuna, gloves hakuna etc, kiufupi hali ni mbaya sana.

Kiufupi wanaochangia huduma mbovu katika vituo vya kutolea huduma vya serikali, hivyo kumwangusha rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli ni wafuatao.

1. MSD (hawana ubunifu, kazi yao kubwa ni ufisadi, wamebaki kusingizia ya kwamba serikali hawapatii fedha. Shida ni kwamba hata hicho wanachopewa na serikali bado kinaishia kwenye matumbo ya watu. Pamoja na kupelekwa Mjeshi kuisimamia MSD, bado hawezi fanya kitu,sababu matatizo ya MSD ni ya kimfumo. Napendeka/ nashauri MSD ifumuliwe yote.

2. Waganga wakuu wa Wilaya/mikoa: Hili ni jipu kubwa sababu asilimia kubwa hawana ubunifu na pia kuwa wagumu kukubali mabadiliko ili kuendana na wakati. Kwa mfano kuna ushahidi wa kutosha ya kwamba ufungaji wa mashine za kielectronics zinasaidia kuongezeka kwa mapato ya serikali, lakini bado asilimia kubwa ya waganga wakuu wa wilaya wameshindwa kufunga mashine hizo katika vituo vya kutole huduma, hivyo kupelekea mapato kuendelea kuwa chini sana.

Sambamba na hilo pia bado kuna asilimia kubwa ya waganga wakuu wa wilaya/mikoa hawana uwezo wa kuongoza na ubunifu aidha kwa sababu hawakuzaliwa hivyo au hawana elimu sahihi kuhusu vipengele hivyo."Wengi wao kazi yao kubwa ni kusoma na kupitisha mafaili ya watumishi." DMOs na RMOs msisingizie mazingira magumu ya kazi, ugumu huo nduo ulifanya mkapewa nafasi hizo ili mpambane kuondo ugumu huo.

3. BIMA YA AFYA (NHIF); Hili nalo ni jipu kubwa, wamekuwa wakivitesa sana vituo vingi vya kutolea huduma serikali kwa kuvilipia malipo madogo uku wakisingizia kwamba vituo vy a serikali vinajaza fomu vibaya. Taarifa za kuaminika toka kwa wadau ni kwamba NHIF kwa kiasi kikubwa wanalazimisha makosa ili mwisho wa siku walipe kiasi kidogo kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma ( makosa mengi ya ujazaji wa fomu hayana uhalisia). Tunaambiwa NHIF wanafanya hivyo ili wabaki na fedha nyingi sababu mojawapo kupata fedha za kulipana posho.
...................................................................................................................
Niishie hapo kwa leo, nina hasira sana huduma mbovu zimempoteza jamaa yangu juzi kisa hakuna dawa.
 
Na bado Ummy Mwl anasifiwa kwa kufanya kazi nzuri?

Hakuna shortcut kwenye hili, serikali ipeleke pesa MSD/NHIF, acheni kulaumu wakati pesa hazipelekwi.
 
Na bado Ummy Mwl anasifiwa kwa kufanya kazi nzuri?

Hakuna shortcut kwenye hili,serikali ipeleke pesa MSD/NHIF, acheni kulaumu wakati pesa hazipelekwi.
Kama hakuna usimamivi mzuri(good governance and leadership) ni kazi bure, maana huko kuna michwa wanatafuna siyo mchezo.
 
Bado kuna sekta za serikali zinafanya kazi kwa mazoea ikiwemo ttcl.suluhisho ni kuzifumua na kuziunda kwa mfumo mpya.
Narudia kusisitiza watoe Wazee wenye mazoea wapumzike. Waweke watu wenye ubunifu na mageuzi. Sekta zinazoendeshwa as if tupo mwaka 1970 zibadilishwe Management ya juu.
 
Back
Top Bottom