Wanaomwangusha Rais Magufuli katika Sekta ya Afya hawa hapa

Wanaomwangusha Rais Magufuli katika Sekta ya Afya hawa hapa

Kuna Tangazo Channel 10 kila kabla ya Taarifa ya Habari ya Saa 1 usiku, Magufuli mwenyewe anasema wameongeza Bajeti ya dawa na vifaa tiba kutoka Tsh 30 Bilioni hadi Tsh 260 Bilioni.

MSD wanapaswa watueleze hizo Tsh 260 Bilioni wamefanyia nini?
Halafu dawa hazionekani.
 
Hakuna kumung'unya maneno hali ya vituo vya kutolea huduma za afya (dispensary, vituo vya afya na hospitali) vya serikali vipo taabani katika kuhudumia wanyonge. Dawa hakuna, mabomba ya sindano hakuna, gloves hakuna etc, kiufupi hali ni mbaya sana.

Kiufupi wanaochangia huduma mbovu katika vituo vya kutolea huduma vya serikali, hivyo kumwangusha rais wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli ni wafuatao.

1. MSD (hawana ubunifu, kazi yao kubwa ni ufisadi, wamebaki kusingizia ya kwamba serikali hawapatii fedha. Shida ni kwamba hata hicho wanachopewa na serikali bado kinaishia kwenye matumbo ya watu. Pamoja na kupelekwa Mjeshi kuisimamia MSD, bado hawezi fanya kitu,sababu matatizo ya MSD ni ya kimfumo. Napendeka/ nashauri MSD ifumuliwe yote.

2. Waganga wakuu wa Wilaya/mikoa: Hili ni jipu kubwa sababu asilimia kubwa hawana ubunifu na pia kuwa wagumu kukubali mabadiliko ili kuendana na wakati. Kwa mfano kuna ushahidi wa kutosha ya kwamba ufungaji wa mashine za kielectronics zinasaidia kuongezeka kwa mapato ya serikali, lakini bado asilimia kubwa ya waganga wakuu wa wilaya wameshindwa kufunga mashine hizo katika vituo vya kutole huduma, hivyo kupelekea mapato kuendelea kuwa chini sana.

Sambamba na hilo pia bado kuna asilimia kubwa ya waganga wakuu wa wilaya/mikoa hawana uwezo wa kuongoza na ubunifu aidha kwa sababu hawakuzaliwa hivyo au hawana elimu sahihi kuhusu vipengele hivyo."Wengi wao kazi yao kubwa ni kusoma na kupitisha mafaili ya watumishi." DMOs na RMOs msisingizie mazingira magumu ya kazi, ugumu huo nduo ulifanya mkapewa nafasi hizo ili mpambane kuondo ugumu huo.

3. BIMA YA AFYA (NHIF); Hili nalo ni jipu kubwa, wamekuwa wakivitesa sana vituo vingi vya kutolea huduma serikali kwa kuvilipia malipo madogo uku wakisingizia kwamba vituo vy a serikali vinajaza fomu vibaya. Taarifa za kuaminika toka kwa wadau ni kwamba NHIF kwa kiasi kikubwa wanalazimisha makosa ili mwisho wa siku walipe kiasi kidogo kwenda kwenye vituo vya kutolea huduma ( makosa mengi ya ujazaji wa fomu hayana uhalisia). Tunaambiwa NHIF wanafanya hivyo ili wabaki na fedha nyingi sababu mojawapo kupata fedha za kulipana posho.
...................................................................................................................
Niishie hapo kwa leo, nina hasira sana huduma mbovu zimempoteza jamaa yangu juzi kisa hakuna dawa.
Huo ni ukweli kabisa, nadhani KM na Mawaziri wanasubiri kutumbuliwa. Mfano huo wa kielectronic unaziba mianya ya kuvuja mapato ndiyo maana DMOs na RMOs hawataki kuweka, pia MSD nao shida
 
Kumbuka MSD wanaidai serikali mamilioni ya shilingi. Bajeti ya wizara ya afya pesa zilizotolewa hazifiki asilimia 20. Usilaumu MSD wala waganga tatizo linaeleweka.
Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa siyo MSD tu inayoidai Serikali bali nayo TAMISEMI inaidai MSD kwa fedha ambazo imepeleka kwenye akaunti yao nao MSD hawajatoa dawa na vifaa kwa vituo vya afya na zahanati na hospitali za wilaya zilizo chini ya TAMISEMI.
 
MSD ni jipu sugu.
 
Fedha zinapelekwa MSD, lakini dawa hazionekani, sasa hivi kuna vituo ukienda ata panadol hakuna.
 
1. To a ushahidi Wa ufisadi Wa msd,onyesha kiasi walichopewa na serikali na kikatumika vibaya.Tofauti na hapo no porojo na kujipendekeza.
JIBU
Tatizo lako unadhani ni serikali tu ndiyo inapeleka fedha MSD. Kumbuka kuna wahisani kibao wanamwaga fedha nyingi tu uko MSD, zinatafunwa na mchwa( Kesi kibao tu zipo mahakamani na wengine walishafukuzwa kazi/kufungwa). Sasa kama unasubiri nilete ushahidi utasubiri kwa sana tu.

2.Ubunifu gani unazungumzia?mashine afunge DMO/RMO au serikali? acha majungu.
JIBU
Sasa kama wasimamizi wakuu RMO/DMO wameshindwa kusimamia ufungwaji wa mashine za electronic (ambalo ni jambo dogo tuu) unadhani watweza jambo gani. Na kwa taarifa yako kwa wale waliofanikiwa kufunga machine hizo mapato yamepanda kwa kiasi kikubwa na na fedha hizo zimesaidia kununua madawa na kushughulikia matatizo mengineyo kwa idara ya afya.
3.Haujawahi kusikia serikali kuchota mabilioni kutoka NHIF?watafanyaje kazi ikiwa pesa zao zinakombwa?FIKIRIA\.
JIBU.
Kwa hiyo kama serikali inachota mabilioni huko NHIF, ndiyo inachofanya kuzipunja hospitali za serikali malipo yao kwa kutumia visingizio vingi visizo na mashiko kwenye ujazaji wa fomu ??
1.Bado haujathibitisha ukwapuaji Wa fedha,wawe wanatoa serikali au donors,let's ushahidi Wa utafunaji fedha
2.Machine zipi?kusimamia ufungaji Wa machine nao no ubunifu?
3.Wewe ulitaka wafanyaje?ni Kama vile inavyotokea kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii,pesa ikichotwa na kupeleka kwingine kusikohusika lazima kutakuwa na nakisi,unafikiri nakisi hiyo inafidiwaje?
 
Billion 260 alafu hata panadol hakuna
Hii Serikali Takwimu zote ni za kupima. Inakuwaje na huduma mbovu ya dawa wakati unatowa Tsh 260 Kwa mwaka? Kumbe wakati wa JK Tsh 30 Bilioni haikupigiwa mapambio na ilitosha
 
Fedha zinapelekwa MSD, lakini dawa hazionekani, sasa hivi kuna vituo ukienda ata panadol hakuna.
Hakuna kitu kibaya kama kuingiza siasa kwenye vitu vyenye tija kama hivi yaaani mwanasiasa akikuambia usitoke nje mvua inanyesha kaa ndani ndugu toka uhakikishe mvua inanyesha kweli ? Ingekuwa nchi za wenzetu zamaani Mwandishi wa habari angeshaingia chimbo kuutafuta uhalisia na ukweli uu wapi ila ndio hivyo tena wanasemaga majanga zitendwa mbali na zilongwa mbali yetu macho
 
1.Bado haujathibitisha ukwapuaji Wa fedha,wawe wanatoa serikali au donors,let's ushahidi Wa utafunaji fedha
2.Machine zipi?kusimamia ufungaji Wa machine nao no ubunifu?
3.Wewe ulitaka wafanyaje?ni Kama vile inavyotokea kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii,pesa ikichotwa na kupeleka kwingine kusikohusika lazima kutakuwa na nakisi,unafikiri nakisi hiyo inafidiwaje?
Kesi zipo nyingi mahakamani, na watumishi wengine wa MSD walishahukumiwa kwenda jela kwa ufisadi.
 
Kujenga majengo ya zahanati yaliyokosa manesi na madokta hili nalo nani anamwangusha?
Praise team; come up in the open. Where are you? Ndege, bwawa la nyerere, fly-overs, barabara za lami, n.k. zinamsaidiaje "directly the grass-root person?" Maendeleo ni watu na siyo vitu (alisema baba wa Taifa).
 
Na kuna watu haohao wanamwangusha JPM kupeleka maendeleo kwa watu,ili dhana ya maendeleo ni watu itimie.
 
Back
Top Bottom