Wanaomkosoa Nyerere wana hoja?


Mkandara nimetafuta thanks haipo, likes haipo nakupa hii Thank you sir!
kilichonifurahisha ni kuwa umempa mifano inayolenga kumtibu Shamu ugonjwa wa chuki aliofundishwa na kukariri bila kujua kuwa yale anayosema yanaisuta nafsi yake na yanamhukumu. Ndiyo maana nasema ni vema kuelewa kuliko kukariri.
Shamu soma between the lines alichosema mkuu Mkandara, halafu jiulize kama Nyerere hakuwa na demokrasi, je kule UN kwenye kura ya VETO kuna demokrasi! Kama Nyerere hakuwa na demokrasi je ipo Vatican au Saudia arabia?
 
NYERERE ALIKUWA NA MAFANIKIO YAKE NA MAPUNGUFU YAKE.

KUNA MAMBO MAWILI TU NDIO YAMEBAKI YANALINDA JINA LAKE

1. Kuondosha ukabila na udini [ingawa naanza kupata wasiwasi na dhamira ya watanzania, kwani siku hizi wanaanza kubaguana kwa misingi hii]
2. Muungano

AZIMIO la Arusha ilikuwa ni nadharia nzuri sana ya ujamaa, lakini haikutekelezeka. Amepigania na kusimamia azimio hilo, lakini limefeli.
 


First, ile video clip ilikuwa na maneno yake mwenyewe, ndiyo maana nimekuambia iangalie ili uyasikie maneno yake mwenyewe anasema kwamba ni DICTATOR. Kwa hiyo ile documentary ilikuwa na ushahidi wa maneno yake mwenyewe Nyerere, kwa hiyo ni USHAHIDI tosha.

Pili, nimekuambia kwamba hatukuwa na demokrasia hata ya kutumia kalamu kuandika yale yanayohusu Nyerere na nchi nzima. Hapo si internet peke yake, ni freedom yote ya press, demokrasia, human rights kwa ujumla.

Nyerere achievement? ndiyo maana nimekujibu yale mazuri aliyofanya hayafikii yale mabaya aliyofanya. Kafanya mazuri, lakini mabaya ni makubwa zaidi. Ndiyo maana analaumiwa zaidi kutokana na mabaya yake.
 

Huwezi kusema kwa sababu mtu fulani au nchi fulani imefanya unyama fulani kwa watu wake basi iwe ndiyo solution kwa binadamu kwa kuwa hakuna njia nyeingine bora. Hitler alikuwa NATIONALISM, aliwapenda Aryan race na kuwapa kila kitu. Alijenga barabara nyingi sana Ujerumani, maisha ya Aryan race yalikuwa mazuri. Je alikuwa kiongozi mzuri?
 
Just a matter of correction. Eli Anangisye hakuwekwa detention kwa sababu ya kupinga bajeti ya Nyerere. Anangisye alihusishwa kwenye mipango ya Kambona ya kupindua nchi 1967-68. Tulikuwepo, tunajua.
 
Katika kazi ninazo ziheshimu ni ya Ualimu.
Nyerere Kafanya mazuri
Kwa mfano? japo mmoja tu
 
Kwa nini uwe na utaratibu vitabuni unaokuruhusu ku rape watu halafu utuambie eti hupendi ku rape, eti ukitaka unaweza?

Tueleze ni namna gani huo "utaratibu vitabuni" umekarabatiwa tokea Nyerere aondoke madarakani hadi hivi leo. Tupatie historical and political context ya hali ilivyokuwa enzi za Nyerere, na jinsi ilivyo hivi leo siyo, siyo unaishia kulaumu tu. Hiyo aidha ni dalili ya intelllectual laziness at best, or malice and slander at worst. Vinginevyo umetoa anecdotes na simulizi za second-hand ambazo huwezi kuthibitisha. Angalau tuambie ni sheria zipi hizo moja baada ya nyingine, unazodai JKN alipitisha kinyemelea.
 
 
 


Duh, nimesoma maelezo yako na kuyarudia tena na tena na kugundua kuwa hujaonesha mahali popote kuwa Nyerere alihusika kwa namna yoyote kuvunja Assemblies of God kama ulivyosema hapo awali.

a. Mgogoro wa Lazaro na Kulola ulianza lini - Bahati nzuri nami nawajua wote wawili kwani nimeabudu katika makanisa yao kwa muda na kushiriki huduma zao ya Kulola pale Bugando Mwanza na mwanae Dan, na ya Lazaro pale Arusha na hata pale Moshi. Na Nilikuwepo nchini at the heat of the conflict ya hao wawili hadi kuchukuliana makanisa! Sikumbuki hata mara moja kuwa Nyerere alikuwa anahusika! Nyerere aliondoka madarakani 1985.

b. Kama kuna jambo jingine lililokuwa limeanza kutokea wakati wa Nyerere (akiwa Rais) na ambalo lilimfanya aingilia kati na kuvunja kanisa hilo ningefurahi, maana isije kuwa alihusika na mgogoro wa dini wa Meru, au Rungwe vile vile.

c. Kuna uwezekano mkubwa sasa (tukichanganya ya M. Said na hili la kwako) na kuchanganya akili zetu za kimbayuwayu, Nyerere yawezekana aliwachukia Waislamu, na Walokole. Tukijumlisha na alivyotaisha mashule ya Wakatoliki na kumtimua yule padre wa Kikatoliki nchini, na hotuba yake nzito aliyoitoa kuhusu nafasi ya Kanisa kwenye Mkutano Mkuu wa Maryknoll, NY, yawezekana aliwachukia Wakatoliki vile vile!! A many of many hatreds.
 
Just a matter of correction. Eli Anangisye hakuwekwa detention kwa sababu ya kupinga bajeti ya Nyerere. Anangisye alihusishwa kwenye mipango ya Kambona ya kupindua nchi 1967-68. Tulikuwepo, tunajua.

Jasusi, ukifuatilia wanahistoria wetu humu.. utashangaa wakati mwingine wanazungumza with such authority utadhani Denzel Washington kwenye "Training Day" aliponguruma "King Kong got no shyt on me!" alivyosema na kusimama you could almost believe him!
 
 
Malaria Sugu;2173888]aliwanyima watu wa pwani elimu, na kuwekeza sana arusha na kuitwa azimio la kuijenga arusha
Miaka takribani 27 Nyerere hayupo madarakani na duniani, je kuna maendeleo gani ya kielimu yamefikiwa mikoa ya pwani tofauti na wakati wake?
Wakati wa uhuru miongoni mwa watu waliosoma dua ya kumuombea ni marehemu Kadinali Rugambwa. Kadinali alikuwa na elimu kiwango cha juu sana. Je huko kagera alipotoka Rugambwa walipendelewaje na Nyerere hata kabla ya uhuru?
Je makongamano yanayoendelea kila siku diamond jubilee yanalenga vipi kumkomboa mtu wa pwani zaidi ya 'matamko' ya kisiasa?
Kama aliwanyima elimu watu wa pwani,JE na kule Zanzibar, Mombasa na Lamu kwenye tatizo kama hilo mwalimu alihusika vipi.


Ukisoma ule mpango wa maendeleo wa Nyerere 1963 hakika kuna watu wanaweza kuwa na mashaka ya kuonewa, si watu wa pwani au kusini.
Kwa ujumla mpango ule ulizingatia wapi nyumba inavuja zaidi na wapi pana angalau unafuu, Wapi patasaidia tunyanyuke na tuwekeze nini.
Endapo miaka 50 imepita na bado tunalalamika mkoloni alitunyonya au pwani wameonewa inafikirisha sana.
Marehemu Mwl wangu Mziray aliwahi kusema ' If you have a problem and you can't solve it, you're the problem to begin with'.

Sidhani watoto wa Hans Pope, Banyikwa, Mcgee, Barongo, Kambona wanaweza kusema Nyerere alifanya mema achilia mbali yale wanayodhani ni mabaya. Kwao Nyerere ni mbaya 100%. Wengi wamerithishwa au kufundishwa chuki.
Ukifuatilia maongezi mengi kwemye baadhi ya 'semina' wasemaji wengi wamekuwa wanahubiri ubaya wa Nyerere, jambo la haki kwani si kila kitu kilikuwa kizuri kiwango cha asilimia mia. Kinachosikitisha hawawezi kusema hata neno moja linaloonyesha kuwa mwalim alilifanya na lilikuwa zuri.

Ni kweli wakati wa mwalimu usalama wa taifa ulifanya kazi vizuri, nadhani tunajua kuwa TZ ilikuwa imehifadhi watu wengi wenye maadui. Mondlane aliuawa Dar es salaam, sasa sijui akina Mugabe, Neto, Nkomo, Mashell wange survive vipi katika usalama lege lege.
Tusisahau kuwa vita baridi ilikaribisha watu wasiotutakia mema na usalama wa taifa ulikuwa muhimu.
Zaidi ya hapo hatukuwahi kuona ndege za jeshi la nchi nyingine zkiingia kuzoa rasilimali za taifa bila serikali kujua.
Na mwisho, je sisi kuishi kwa utangamno kwa miaka hiyo ya mwaalimu halikuwa jambo jema

Kuhusu EAMWS, Mohamed Saidi alikiri hapa kuwa kulikuwa na mgogoro wa uongozi kutokana na uroho wa madaraka, na hilo lilitoa mwanya kuundwa Bakwata. Sidhani waislam ambao walisismama kidete kupigania uhuru dhidi ya mkoloni wangeshindwa kusimama kidete dhidi ya Nyerere. Tatizo ni kuwa hakukuwa na mkakati wala uweledi na wengi walivutwa kwa matamanio binafsi kama tunavyoona leo hii. Huwezi kuniambia taasisi lukuki zimeshindwa kujenga taasisi moja yenye nguvu.

Bukuku na Mohamed Said tunaomba muweke historia vema kwasababu kama ninyi 'mnaofahamu' mnapingana wasomaji watakuwa na hali gani.
Tatizo ni masimulizi yanayoweza kutofautina kutoka mtu hadi mtu. Uandishi unaozingatia bias na si fact.
Tuelezeni Nyerere na EAMWS ilikuwaje?
 
Hii mijadala ya Nyerere inazidi kushika kasi hapa jf.

Ngoja wengine tuendelee kujielimisha tu, manake kuna watu wanagawa taaluma ya historia ya Nyerere si mchezo.

Mwisho wa siku kitaeleweka tu pamoja na haya mashambulizi na utetezi wa Nyerere, ukweli utabaki umesimama.

Baada ya hii thread kufika mwisho sitoshangaa mwingine anaibuka tena na Nyerere kafanya vile na vile!!

Au huu mchakato wa "kumtakatifusha" ndio umeleta hili sekeseke??
 

SIdhani kuwa sababu ya 'kumtakasisha' inaweza kubwa hivyo. Kama ndiyo inashinikizwa na kitu kingine kwasababu suala hili ni binafsi na linawahusu watu wenye imani yao katika jamii. Wapogoro au waluguru wakiamua kumfanya chifu mangungo mtakatifu wao inahusu nini sisi kama jamii.
Kama wakatoliki wameamua kumfanya hivyo inahusu nini watu wa madhebu au imani nyingine. Tunaposema uhuru wa kuabudu hii ndiyo maana yake. Kama tunadhani kuna makosa kufanya hivyo,ipo siku tutakwenda kuvunja mibuyu au majabali ya watu wanayoyaamini.
Kama wakatoliki wataamua kumfanya Nyerere mungu wao inamhusu nini asiye amini?

Tatizo la kuvuruga au kupotosha historia ili kumshambulia mwalimu limepamba moto siku za karibuni kama sehemu ya utetezi wa serikali iliyopo madarakani ili kuonyesha kuwa matatizo ni sehemu yetu hata wakati wa kiongozi kama Nyerere yalikuwepo.
Kibaya zaidi ni kuhusisha matatizo yetu na utawala wa Nyerere. Mtu anaposema tatizo la Nyerere ni kutowekeza katika umeme inafikirisha na kusitisha.Hata pale isipothibitika au kuwa na ushahidi bado watu wameng'angania tu kumpaka matope ili viongozi waliofuata na waliopo waonekane japo wasafi na matatizo yamesababishwa na Nyerere.

Tukumbuke kuwa mti wenye matunda ndio utupiwao mawe. Mtu mwenye calibre ya Nyerere ni talk of the century. Kwahiyo mjadala unazidi kutufanya tumwelewe Nyerere(kama hukufundishwa chuki) kwa mema na makosa katika utawala wake.

Tumewasahau Mwinyi, Mkapa, Obote, Kenyatta, Idd Amin kwasababu hawana la kuongelea. Na kama kipo kizuri ni kwa misingi iliyojengwa na waadilifu, bahati mbaya utamuongeleaje mtu kama mkapa umtenge na ufisadi na kama kiongozi aliyetufikisha hapa kimaadili.
Utamuongeleaje Mwinyi bila kuongelea udhaifu wa uchumi wa ndani ya nchi.

Tutawaongelea akina Churchill, FDR, Nkrumah, Tito, Mahatman Gandhi, Indira Gnadhi, Mahathiri Mohamed, Mao tse tung, Gamar Abdel Nasar, Menachim Begin, Anwar Saadat, Fidel Castro, Billy Clinton, Ayatollah Khomen ,Olf Palme,Mandela, Nyerere n.k Hawa wana kitu cha kuongelewa kwa sura yoyote.

Historia ielezwe na iandikwe kwa ukamilifu wake bila kumpendelea au kumuonea mtu.
Ufumbuzi wa matatizo yetu hautatokana na lawama kwa mwalimu na tusijiche vichwa chini ya mchanga kama Mbuni.
 
Just a matter of correction. Eli Anangisye hakuwekwa detention kwa sababu ya kupinga bajeti ya Nyerere. Anangisye alihusishwa kwenye mipango ya Kambona ya kupindua nchi 1967-68. Tulikuwepo, tunajua.
Ulikuwepo? Humiliki facts za Bunge la Pili na kujaribu kumsafisha Nyerere kwa sababu eti "nilikuwepo."

Hansard, October 1st, 1968, Collumn 23

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

African Journal of Political Science (2002), Vol 7 No. 2
Mohabe Nyirabu

TANU – "The Nationalist"
Oktoba 21, 1968


Raia Mwema
Januari 26, 2011
Joseph Migangwa



"Kwenye Kikao cha Bunge cha Oktoba 1968, Mbunge wa Taifa, Wilfred Mwakitwange, kwa kukerwa na ubabe wa Chama dhidi ya Bunge, aliitaka Serikali ifafanue, kama TANU ndicho kilichoongoza Serikali au Serikali ndiyo iliyoongoza TANU. Alijibiwa kwa hasira na vitisho na aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Richard Wambura kwamba:

"Nataka ieleweke kuwa, ni Chama kilicho juu ya vyote; Wabunge wanapaswa kufanya kazi chini ya Chama ambacho ndicho kilichowateua, na hivyo kina haki ya kuwashikisha adabu ……Bunge hili ni la TANU" [Hansard, Oktoba 1, 1968].

Mwakitwange akasimama tena na kuuliza: "Kama ndivyo hivyo; ni nani anayepaswa kukishikisha adabu Chama?".

Ndipo Makamu wa Pili wa Rais mwenyewe, Rashidi Mfaume Kawawa, akasimama na kusema: "Chama hakina mpinzani wala mshindani…….. Hili nataka lieleweke mara moja kwa wote; na iwe mwisho kuhoji hoji Chama".

Kabla ya hapo, mapema Julai 1968, Mbunge wa Iringa Mashariki, M. Chogga, wakati akichangia Muswada wa Marekebisho ya Katiba, alitaka ibara ya 6 (2) ya Katiba irekebishwe kulifanya Bunge kuwa Mshauri Mkuu wa Rais, ili atekeleze shughuli zake tu kwa ushauri wa Bunge ambalo alisema ndilo kuu na kiongozi wa mihimili mingine yote.

Alitaka pia mambo makuu yote ya kitaifa yanayoshughulikiwa na chombo chochote cha Kitaifa, kama vile Bunge na Baraza la Mawaziri, hatimaye yawasilishwe bungeni kwa hatua na idhini ya mwisho.

"Hii ndiyo demokrasia sahihi kwa Tanzania; sikubaliani na mfumo mwingine wowote kuitwa wa kidemokrasia", alisema Chogga.

Kisha akaendelea kushambulia sharti la Wabunge kuwa wanachama wa TANU akisema kuwa, wakati Chama hicho kilikuwa na wanachama robo tu ya Watanzania wote, hakikuwa na uhalali wowote wa kumfukuza Mbunge aliyechaguliwa na robo tatu ya Watanzania wasiokuwa na kadi za TANU. Kwa maelezo hayo, akawa amewasha moto wa vita juu ya ukuu wa Chama dhidi ya Bunge.

Suala hili liliibuliwa tena na Chogga mwezi Oktoba 1968, wakati wa kujadili Muswada wa Kurekebisha idadi ya Majimbo ya Uchaguzi, alipohoji uhalali wa Bunge kuwa na Wajumbe 204, wakiwamo 107 wa kuchaguliwa, 10 wa kuteuliwa na Rais kutoka Tanzania Bara na Visiwani, 15 wa kuchaguliwa na Bunge kuwakilisha Taasisi za Umma, Wakuu wa Mikoa 20, Wajumbe 32 wa Baraza la Mapinduzi; na Wajumbe 20 kutoka Visiwani wa kuteuliwa na Rais kwa kushauriana na Makamu wa Rais na Rais wa Zanzibar.

Kuhusu madai yake kwamba Wabunge wa kuteuliwa hawawakilishi watu wala mhimili wa Bunge, Chogga alisema: "Siamini kitu hiki kinachoitwa uteuzi. Mtu anapomteua mwingine, mteuliwa huyo lazima afuate na akubaliane na kila kitu cha aliyemteua. Na kama Wahenga walivyosema, ‘amlipaye mpiga zumari ndiye huchagua wimbo', Wabunge wa kuteuliwa si Wabunge wa wananchi, bali ni wapiga zumari wa Rais", alifafanua Chogga.

Akapendekeza pia kwamba Rais aondolewe robo tatu ya madaraka aliyokuwa nayo (anayo mpaka sasa) chini ya Katiba, yahamishiwe kwenye Bunge; na kwamba, Tanzania iwe nchi inayofuata mfumo wa Vyama vingi vya Siasa na kuwe na wagombea Urais zaidi ya mmoja.

Akamaliza kwa kusema, Bunge lilikuwa juu ya Chama na Serikali, na si kinyume chake. Hapa tena, Chogga akawa amewasha moto na kuchokoza hasira za wahafidhina wa Katiba ya kidikteta.

Hasira ya TANU haikuwabakiza Wabunge wote waliotaka ukuu wa Bunge, kwani Halmashauri Kuu ya TANU ilipokaa mjini Tanga, Oktoba 1968, iliwavua uanachama na ubunge Mwakitwange, Chogga, G. Kaneno (Karagwe), T. Bakampenja (Ihangiro), Joseph Kasella-Bantu (Nzega Mashariki) na J. Kibuga (Mufindi), kwa kosa la kupungukiwa maadili mema na kwa kuhoji ukuu wa Chama.

Wengine mashuhuri waliofukuzwa ni aliyekuwa Waziri wa Tawala za Mikoa na Mbunge wa Morogoro Mashariki, Oscar Kambona, ambaye baadaye alikimbilia uhamishoni nchini Uingereza na Mbunge wa Rungwe Kaskazini ambaye pia alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa TANU [TYL] Elli Anangisye, ambaye pia alitiwa kizuizini na baadaye kuachiwa.

Sababu za kufukuzwa kwa viongozi hao, kama zilivyoelezwa na gazeti la TANU – "The Nationalist" la Oktoba 21, 1968, zilikuwa ni "kujaribu kuhujumu Serikali ya TANU…..Hao wawili ilibidi wafukuzwe kwa sababu hawakuwa waumini wa TANU wala itikadi ya Ujamaa."
 

Sasa hapo umethibitisha vipi madai yako ya awali (kuhusu yaliyomsibu Elli Anangisye) au kukosoa sahihisho la Jasusi? Hebu tufafanulie tafadhali.
 
Sasa hapo umethibitisha vipi madai yako ya awali (kuhusu yaliyomsibu Elli Anangisye) au kukosoa sahihisho la Jasusi? Hebu tufafanulie tafadhali.
Kambona alikimbilia Uingereza mwaka 1967. Hapo hii ripoti imekosea. Kama alifukuzwa kutoka TANU basi alifukuzwa in absentia. Lakini hakuna mahali popote pale inapoonyesha kuwa Anangisye alitiwa kizuizini kwa kauli zake bungeni. Wanasema tu kuwa "kujaribu kuhujumu serikali ya TANU". Nijuavyo ni kwamba alihusika katika njama za Kambona kupindua serikali na alikuwa na mawasiliano naye. Taso bado anayo homework.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…