Wanaoisaliti CHADEMA ni viongozi

Wanaoisaliti CHADEMA ni viongozi

Kwenye michango humu jf nimeelza suala hili. Kiukweli, watu waliotoka NCCR/ TLP, wana matatizo. Wanaanzisha maneno na majina ya ajabu kidogo kidogo, halafu mtafaruku unaibuka. Neno msaliti au kirusi ni mabaya sana ktk siasa. Mrema walimvuruga hadi akabaki kama kipepeo, akawa hajui cha kufanya. Muda si mrefu chadema vikao vitavurugika kwani tayari kuna virusi na wasaliti vikaoni. Wataelewanaje? Chonde chonde viongozi dhibitini hali hii mapema, vinginevyo mtaungana na Nccr na Tlp.
 
amina ningechukua nafasi hii kumwomba mh lema aendeleze mapambano aachane na wanafiki ambao ipo siku munngu atawaumbua na siku si nyingi,
 
Kama hao wote waliotajwa na Mleta mada wametokea NCCR-Mageuzi, ipi ni CHADEMA? kwa nini hiki chama kissitwe NCCR-MASALIA?
 
Kweli makamanda wasaliti wapo daima na wala hatuna haja ya kuwahofu wala kutuamisha focus yetu kuelekea 2015
 
Wote tunajua kuwa mapambano yoyote ya kujikomboa huwa hayakosi vikwazo, au wapinzani wa Mapambano hayo wawe wa kutoka ndani au nje ya kundi linalopambana! Wakitoka ndani ya kundi ndo wanaitwa wasaliti. Lakini katika Historia wasaliti hawajawahi kuzuia dhamira ya mapambano isitimie kwa wakati! Chadema ilipofikia na mapambano yalipofikia haina haja ya kuhofia wasaliti, inayo nguvu na uwezo wa absorb shock zitakazoletwa na msaliti wa aina yoyote! Ziko namna za kudeal na wasaliti kwa calculations ili kupunguza risk na impact yake kwenye Chama, lazima ujue hao unaowaita wasaliti nimwatumishi wa kambi nyingine iliyokinyume na Chadema either kwa kujua au kwa kutokujua, kwahiyo Chama lazima kiwe na busara ya kudeal nao. Lazima ujue msaliti huwa anasura mbili sura inayoonekana nje siyo ya kisaliti anaonesha sura malaika lakini ndani ni umbwa mwitu, na hivyo baadhi ya watu hao huwa ni watu wenye ushawishi kwenye jamii lakini ndani yao ni wasaliti wakubwa, kwahiyo lazima chama kiwe na busara namna ya kudeal na wasaliti, wasaliti hawataisha kwenye taasisi yoyote, na pengine siyo wote watakaondolewa au hata kugundulika na wasaliti wengine hawatakiwi kuondolewa kwenye chama kabisa kwasababu kuwabakiza na kuwanyima mazingira ya kuondoka ni mkakati pia wa ushindi kwa dhamira ya ukombozi. Na Hapa nitaomba with all due respect nitofautiane na Kiongozi wangu Mh. Godbless Lema, Chadema haiwezi kuacha ku-pursue cause ya mabadiliko na ikaazisha vita ya wenyewe kwa wenyewe eti ya kupambana na wasaliti, hatuna sababu ya kufanya hivyo wala si busara kufanya hivyo! Wasaliti hawajaizui Chadema kujenga Chama na kuendelea kujiimarisha vijijini na mijini, katika kipindi chote baada ya uchaguzi mkuu 2010 Chadema imepiga hatua kubwa na imejenga imani kubwa sana kwa wananchi siyo kwamba wasaliti hawakuwepo, wasaliti wanapaswa kuwepo washuhudie dhamira ya ukombozi ikitimie mbele yao, hatuna sababu ya kuanzisha vita na wasaliti, wakati nguvu hiyo tunaweza kuitumia kuingiza maelefu ya wanachama wapya wanaoisubiri chadema vijijini na hawajafikiwa! Mimi naamini Godbless Lema ni mtu ambaye ni positive thinker sana ila kwa hili la wasaliti approach yake ni destructive kwa mustakabali wa Chama na itatuchelewesha kutimiza dhamira yetu ya Ukombozi. Na yeye kama mjumbe wa kamati kuu amepotoka kuongelea maswala nyeti ya Chama kwenye mitandao! Nashauri atumie vikao husika ambavyo yeye ni mjumbe kutoa maoni yake. Mwisho nitoe wito kwa wapenzi na wanachama wa Chadema na wapenda mabadiliko wote kuwa Chadema iko imara, Chadema haina hofu na wasaliti, Chadema imejipanga kuchukua dola 2014/2015!
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Chadema.

Nichukue tu hiyo mistari michache ya mwisho. Wewe ni nani mpaka uwaondoe HOFU wana-CDM? wenye chama huwa wanakuja na majina yao halisi humu. Tunawajua akina SLAA, BEN SAANAE, MWIGAMBA na weingine, iweje uje kututoa hofu na Id feki. Ukumbuke kuwa wengi kutofikiwa na CDM viijijini ni sababu mojawapo ya hao unaowaita wasaliti kutaka wafikiwe kwa hali mali na ndipo hubadilishiwa kibao na kuitwa wasaliti. Watafikiwaje wakati kuna watu wanataka kutengeneza mfumo wa fedha kwa tsh. mil 18 badala ya mil.2? watafikiwaje wakati machapisho ya kadi za chama yanafanywa na kampuni ya Mwenyekiti huko china, kwani kadi haziwezi kuchapishwa Tanzania? Kama mnataka CHADEMA isife ni lazima kwanza mtambue madai ya akina MWIGAMBA na wenzake kuwa ni ya msingi badala ya kuwaita wasaliti.
 
amina ningechukua nafasi hii kumwomba mh lema aendeleze mapambano aachane na wanafiki ambao ipo siku munngu atawaumbua na siku si nyingi,

Kwa shutuma hizi dhidi ya LEMA si ni dhahiri na yeye ni msaliti?
 
Tusonge mbele na tutashinda vita hii.Traitor atapimiwa kipimo kile kile tunachowapimia CCM

Wewe ugonjwa wako ni kuamini tu wasaliti wanatumwa na CCM, hili ndilo jambo litakaloiua CHADEMA kilaini sana, mnaacha kuyafanyia kazi madai ya watu wanaopigania UWAZI ndani ya CHAMA mnaendeleza tabia ya kuwa VIBARAKA wa wachache ndani ya CHAMA na kuwabambika wenzetu waliowafikisha hapo mlipo majina ya USALITI, dhambi hiyo itawatafuna sana.
 
ameni baba, ila yote haya yana mwisho simpend chief mnafiki mkuu kunasiku nilikutana naye mirambo50 kwenye ofisi ya rostam sijui alifata nini.
Chief ndiyo nani ndani ya CHADEMA?
 
ni kweli, mh lema zingatia huu ushauri, tnapaswa kukijenga chama, chadema inakubalika sana, 2014 kna uchaguz wa local govenment, its time now kuelekeza nguv vijijin tnasubiliwa uko.

wasaliti tshawajua na hakuna kitu kizur km kumjua mbaya wako, na zaid hakuna kitu kibaya kwake km ktomshirikisha kt ratiba za ujenz wa chama aka m4c wanaumia vibaya

so mh lema its right time now kuendeleza harakati za kujenga chama hasa vijijini ili kuhakikisha 2014 tnakuwa na viongoz wa kutosha ngaz za vijiji, mashina, matawi na wao watasaidia pakubwa kuwapata wabunge weng pia kura nying za uraisi apo 2015
 
Chadema haiyumbishwi na wasaliti bali wasaliti wanayumbisha watanzania,

Wembe tunaomnyolea ccm, ndio huohuo tutakao wanyolea wasaliti hawa,
 
frema120 nikweli hakuna mtu anapenda kuishi na msaliti, lakini usipokuwa makini kazi ya msaliti moja wako ni kukuondoa kwenye dhamira, kwahiyo mnaweza mkajikuta mnatimiza malengo yao badala ya lengo la chama! Wito wangu tusiwe paranoid na wasaliti tukasahau jukumu letu la ukombozi!
hivi nini maana ya neno saliti? mbona mnalitumia vubaya, mtu akitaka kujua ukweli wa namna chama kinavyo-operate ni usaliti? mtu akihoji sababu za Katiba ya chama kukiukwa ni usaliti?
 
hakika hili kundi la mbowe, slaa, ben saanane, lema na wenzao litaaibika sana, sijui ni kwa nini hawataki kusikia changamoto ndani ya chama.
wakubaliana cha changamoto ya kukiuza chama kwa ccm!bado sijaona watu wenye nia njema ya kukiongoza chama zaidi ya hawa tulionao!kunabaadi ya hao unaowaamini wanamiliki mabilioni uswiss!
 
ni kweli, mh lema zingatia huu ushauri, tnapaswa kukijenga chama, chadema inakubalika sana, 2014 kna uchaguz wa local govenment, its time now kuelekeza nguv vijijin tnasubiliwa uko.

wasaliti tshawajua na hakuna kitu kizur km kumjua mbaya wako, na zaid hakuna kitu kibaya kwake km ktomshirikisha kt ratiba za ujenz wa chama aka m4c wanaumia vibaya

so mh lema its right time now kuendeleza harakati za kujenga chama hasa vijijini ili kuhakikisha 2014 tnakuwa na viongoz wa kutosha ngaz za vijiji, mashina, matawi na wao watasaidia pakubwa kuwapata wabunge weng pia kura nying za uraisi apo 2015

huu wimbo wa "KUELEKEZA NGUVU VIJIJINI' mbona unajirudia sana, sababu za mipango hiyo kukwamba ni nini, au ukihoji na hilo utaitwa MSALITI?
 
wakubaliana cha changamoto ya kukiuza chama kwa ccm!bado sijaona watu wenye nia njema ya kukiongoza chama zaidi ya hawa tulionao!kunabaadi ya hao unaowaamini wanamiliki mabilioni uswiss!

kwa hiyo usaliti maana yake ni kukiuza chama CCM? kweli mfa maji haachi kutapatapa.
 
Back
Top Bottom