Wanaoisaliti CHADEMA ni viongozi

Wanaoisaliti CHADEMA ni viongozi

Lema bila vurugu hawezi 'kuonekana'
kwenye vurugu ndio 'anaonekana'
so zikikosekana vurugu inabidi azianzishe i guess

lema endelea kuiwatimulia vumbi ni bora simba mia walioko nje kuliko nyoka mdogo aliyeko ndani
 
Think tank yenyewe ni lema na sugu unategemea nini hapo
 
Mlikuja na mbinu za ukabila zikagota! Mkabuni ile ya ukanda, ikayeyuka! Mkaparamia udini, haukulipa! Mkaibua ugaidi, ukawarudi wenyewe! Sasa mnapiga mayowe ya demokrasia! Mbinu hii nayo imeanza kuwarudi!! Sasa mnatapatapa mithili ya vifaranga wanaopigwa na mvua kali wakati mama yao akiliwa na kimbulu! Je baadaye mtakuja na mbinu gani tena?

Tulia mabosi zako wafundwe, we hujui kitu zaidi ya kumchangia LEMA sadaka!
 
Tatizo la Chadema wanadanganywa na vijana wa Arusha wanadhani Tanzania yote kama Sakina au Standi ya vifodi.
 
1. Viongozi wa Chadema wanatumia muda mwingi na resource za Chama kuchumia matumbo yao, then wanatumia resource zaidi kuficha uovu wao na kuwalipa mashabiki wao wakaeneze sumu mitandaoni dhidi ya wanachadema wenzao huku wakidai kua "wanasafisha chama", ndio maana hawawezi kudumisha demokrasia. Kusafisha kwenyewe hawasemi kutachukua muda gani na what are the criteria to this witch hunt!

wataje kwa ushahidi mkuu

2. Wanasema uchunguzi unaendelea hawawezi kulizungumzia.

watalizungumziaje bila uchunguzi?

3. Chadema na misingi yao: chama kinajiita cha demokrasia ila ukileta mawazo mbadala unaitwa msaliti. Ukiuliza kuhusu uchaguzi unaitwa masalia. Ukihoji matumizi ya pesa wanasema umepandikizwa. Hakuna mechanism za checks and balance. Wanao set agenda ya chama ni watu sio zaidi ya 5. Hawaheshimu uongozi wa ngazi za chini na wanadai wanataka serikali ya majimbo.

hali hiyo ingelikuwa kama unavyojaribu kutuaminisha, CDM isingeliwahangaisha watabiri wa kifo chake

4. Kujigawia viwanja, wamo! Kujinunulia majumba ndani na nje ya nchi, wamo! Sasa wanataka posho na mishahara waongezwe!
kuhusu ufisadi: serikali imeshindwa kuwakamata mafisadi wa CDM hadi watu mbweke hapa kama......asiye na meno? wachunguzeni
kuhusu posho" hivi nani alilianzisha hili la posho? kiranja wa bunge ni nani na wa chama gani vile? :A S-confused1::help:


5. Role model wa chadema ni ccm: wanalazimisha wanachama kuamini kua ccm ikifanya jambo basi rukhsa kwa kila chama. Kwanini wasikaguliwe? Mbona ccm haijakaguliwa. Mbona viongozi wanatumua vibaya per diem? Mbona vasco de gama nae anatumia vibaya. Mbona viongozi hawawekezi nyumbani, wananunua majumba nje? Eti ccm nao wapo kama hao. So what? If you are a mere copy paste of ccm how are you an alternative???

think beyond that

6. Chadema na dharau kwa wanachama: hatuwezi kuitisha uchaguzi sababu tunataka kwanza kusafisha chama. Kwanini hamkusafisha kabla muda wa uchaguzi haujafika? Kalenda ya huo usafi ni lini hadi lini ili wanachama wajipange? Kuna viongozi wasaliti ila hatuwezi kuwataja: kwanini? Mnawaona wanachama wajinga and undeserving of knowledge? Kama mtu kama lema aliweza kuona na kuelewa basi hata mtoto wa primary ataelewa (nimetaja primary makusudi kabisa).

kwa wewe kuliona hili, mtoto wa nursery haitamsumbua,(Ooop dont mind my language) teh teh teh

7. Chadema na sera za wananchi: mara ya mwisho hawa viongozi ambao sio wasaliti walileta agenda yenye sera za kitaifa ni lini? Agenda ambayo inamanufaa kwa nchi na sio kwa chama chao? Wabunge wao inabidi wapeleke hoja kama hoja binafsi na kulisimamia wenyewe maana imeshindikana kabisa kuomba support ya chama kwa mambo yasio ya manufaa ya chama, na chama ni cha familia mbili. Ya first lady na mume wake, na ya mkwe wa mwanzilishi. Bow or die. Kila ukiskia CHADEMA kwenye magazeti ni sababu wana zungumzia mambo yao ya ndani ya chama (most of the time schandals). Never about wananchi. Na ikitokea mmoja achukue agenda ya maji, au ya ardhi ya wananchi wake basi wananongonezana kua anatafuta sifa. Wanao beba agenda za kitaifa ndio kabisaaaa wanasema ni agenda ya ccm. Kumbe wanajua ccm ndio taifa?

walisema elimu itatolewa bure. walisema wakipewa madaraka mfuko wa saruji utashuka bei, n.k. hizi zilikuwa sera za mtu binafsi, mgombea wa Uraisi 2010, Dr W Slaa. Hakika hazikuwa za chama

8. Anyway, najua walio na macho hawaambiwi tazama. Chadema has the potential to be an alternative to ccm ila kwa tunayo yaona siku baada ya siku tunakua na doubt. Na wanao wasaliti wanachama si wengine bali ni baadhi ya viongozi. Bahati mbaya hawawezi kuondolewa maana wamesha sitisha uchaguzi na wamebadilisha na katiba!

have you ever stopped doubting CDM in your life?


NB: Bila kujali itikadi za kisiasa na tukiacha ubafiki, usaliti na ubinafsi taifa litasonga mbele kwa kasi ya ajabu
 
Mwenye Macho haambiwi TAZAMA. Mwenye Mapenzi kweli haoni 🙂
Ndugu yangu mbona unarudi na tactics zile zile za kupotosha ideas and concepts kwa kytumia habari za sani na bongo? Hayo ya mimi kua na ukaribu na zitto yanatoka wapi na yanahusika vipi? Mnataka kudiscredit hoja kwa kunihusisha personally na Zitto. Ningekua mwanaume ungesema hivo? Try to distant yourself from this type of thinking.

Mi sijawahi kua member wa chadema na sijawahi sema kua mimi ni mwana chadema. Nataka kuona mabadiliko. Kila unaposoma post yangu kaa na hili kichani: sitetei mtu, sitetei chama. Natazama maslahi ya watanzania. iwe posho, ruzuku, utoroshaji wa ushuru etc, yote ni agenda zenye maslahi. Ukiona jina la zitto linajirudia ni sababu he leads those process. Siku mngine akilead nae atatajwa, full stop.

Mimi sio pro-Zitto ila nakubaliana na mengi sana anayo yafanya. He might not be perfect ila Kwa mtu wowote anae taka mabadiliko ni rahisi kumsupport, irrelevant of chama, social status, education, dini, kabila, na mengine yanayo tutenganisha. Hana siasa za fingerpointing, anapiganisha misingi mibovu na kubadili system, not people. Anafata misingi ya chama alicho jichagulia mwenyewe. (Mtu asipofata misingi ya chama chake atafataje misingi ya nchi?) Sijawahi mskia katika siasa za kuchafuana au za kuwekeana sumu.

Siasa ni struggle for power na kila mwanasiasa anataka madaraka. Either collectivelly (chama kipewe madaraka) or personally (yeye apewe madaraka). Kuna wanao tumia nguvu za uma kuonesha they deserve to be trusted. Kuna wanao tumia nguvu za chama chao. Kuna wanao tumia public image. Kuna wanao beba agenda za population, kuna wanao tumia agenda za wanasiasa wengine. Wapo watakao tupilia mbali personal valuea na party values na kujiunga na mafisadi ili ky-protect their pisition and income. Ndio unataka tuwajadili hawa?

Muhimu ni population kua makini na kuhakikisha wanampa support mwanasiasa anae ambatanisha personal motivation yake na maslahi ya wananchi. Wapo wengi ambao personal ambition haipo aligned na maslahi ya wananchi, na hawa ndio kikwazo cha mapinduzi.
 
Mwanachama mpya wa CHADEMA karibu

Kaka sio mpya ni yule yule head wa masalia hii ngoma itakwenda mpaka mwishoni mwa mwaka tumeshazoea sasa na itapoa mwanzoni mwa mwaka kwa sababu wataanza kwenda kwenye kanda ha ha nacheka mie JF ni hazina ya wajinga wengi kama mwali safari hii watakubangua kama korosho once and for all
 
Tatizo la Chadema wanadanganywa na vijana wa Arusha wanadhani Tanzania yote kama Sakina au Standi ya vifodi.
ninachojua mimi ni wa Pwani chini ya mwana wa mfalme Ridhiwani kuapiza kuwa kamwe kamwe kaskazini haitakaa ichukue nchi tunamgoja safari hii Salma Kikwete kupitishwa na chama chake kuwa mgombea na hakika wa pwani lazima wawe maraisi kwa kudra za Ritz
 
Tulia mabosi zako wafundwe, we hujui kitu zaidi ya kumchangia LEMA sadaka!

Hakuna shida fedha za mapembe ya ndovu from Kinana Lukuvi and the core zinafanya kazi mr book seven huitaji kuwafunda wezi wa nyara za umma
 
Think tank yenyewe ni lema na sugu unategemea nini hapo

ndio kweli yenyewe au wewe mwigulu mrusha mabomu na ma zungu ya unga MACCM kwako ndio mathink tank Arusha inazizima na mbeya inazizima wewe unaota
 
Acha ujuha wewe ule ushahidi utakaukbaliwa hata mbinguni umeishia wapi!? Kesi mbona imefutwa...Unafikiri CCM na Serikali yake jinsi inavyoihofia CHADEMA kungekuwa na ushahidi unadhani viongozi wa CHADEMA wangekuwa bado wako mtaani!? Uwe unafikiri kwa kina kabla ya kuandika pumba. Narudia tena ndani ya CHADEMA hakuna makundi kuna mchumia tumbo mmoja mbunge kupitia CHADEMA na mwingine ambaye mara zote ndiye chanzo cha matatizo ndani ya CHADEMA.

Na haya je?
1. Kundi la walisha watu sumu wakiongozwa na lwakatare,ben sa8
2. Kundi la wamwagia watu tindikali under henry kileo
3. Kundi la walipua mabomu chini ya lema
..kundi la slaa
...kundi la mbowe
...kundi la zito aka prezo
 
Chadema ni genge la wapigaji
Tangu Mh KIkwete atangaze deal la kuaga IKULU MACCM mumeehuka haishangazi kwenye psychology wanasema binadamu anakataa kufa mpaka dakika ya mwisho ya kukata roho ,mwenyekiti anadeclare rushwa ni sera ya ccm wewe unajikongoja kumuamini duh watu muna viburi kweli
 
Mamlaka yote ya maamuzi ndani ya chadema yako kwenye mkoba wa Mzee Mtei.

Yeye ndio anachagua nani ampe cheo. Mtu yeyote anayeongea kitu tofauti na anavyotaka Mtei huitwa msaliti kwa sababu lengo la kumpa cheo hicho ni kulinda matakwa ya mtei.

Mapropagandist wa CCM kama wazungu wa unga madawa ya kulevya mpaka yamewalevya hawana tofauti na nzi anabeba kinyesi toka eneo moja mpaka linguine watu wako kwenye misingi unaongea habari za Mtei who is Mtei kwenye M4C mutalisoma jua madalali wa pembe za ndovu ,wabariki zero kuwa division 5 big result now
 
Viongozi wa Chadema wanatumia muda mwingi na resource za Chama kuchumia matumbo yao, then wanatumia resource zaidi kuficha uovu wao na kuwalipa mashabiki wao wakaeneze sumu mitandaoni dhidi ya wanachadema wenzao huku wakidai kua "wanasafisha chama", ndio maana hawawezi kudumisha demokrasia. Kusafisha kwenyewe hawasemi kutachukua muda gani na what are the criteria to this witch hunt!
Mwali, je kwa resources ilizo nazo chama tawala, huamini kwamba wanaweza kuweka mapandikizi ndani ya upinzani? Je ungeshauri Chadema ikigundua kwamba kuna mvurugaji miongoni mwao, wachukue hatua gani? Tofauti na wewe mimi siamini kuwa Chadema wanawalipa mashabiki wao wakaeneze sumu mitandaoni dhidi ya wanachadema wenzao. Wengi wanaoitetea Chadema mtandaoni, mimi nikiwa mojawapo, wanafanya hivyo kwa sababu moja tu, wanaamini CCM haina ujasiri, uwezo wala nia ya kutokomeza maovu katika jamii. Mathalani leo hii kama NCCR ndio ingekuwa na ushawishi, nguvu na ari ilizo nazo Chadema, nisingesita kuwaunga mkono kwa sababu naamini kwa dhati kuwa adui wetu mkubwa kama Watanzania ni CCM, period.
Kwa mtindi huu (sorry, i meant kwa mtindo huu) sioni Chadema ikichukua uongozi in the next 100 years. Tukumbushane tu mambo kadhaa...
Yawezekana mwanzoni ulikuwa na hoja nzuri na ulitaka kuipa ushauri Chadema lakini kwa kauli yako hili umeharibu kabisa na kuonesha kuwa huna nia njema na Watanzania. Pengine umesukumwa zaidi na utashi binafsi kuliko utashi halisi bila kutafakari kwa upana athari za kauli kama hizi za kukatisha tamaa. Na kama kuna watakaokubaliana na wewe ni wale walio na woga wa mabadiliko, yalisemwa 1992 na leo, miaka 21 baadaye, unayarudia.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Finally, someone discussing the topic and not people!

1. Viongozi wa Chadema wanatumia muda mwingi na resource za Chama kuchumia matumbo yao

wataje kwa ushahidi mkuu
Lema anapo zungumzia maswala ya posho kuongezwa kwenye vikao vya chama ni kwa maslahi ya walio wachangia ku-organise hicho kikao?

2. Wanasema uchunguzi unaendelea hawawezi kulizungumzia.

watalizungumziaje bila uchunguzi?
if only they could aply this wisdom to all affair, and display some understanding wanapoambiwa hivo! Na mbona double standarda? Mengine yanazungumziwa bila uchunguzi ila yanao waponza lazima yachunguzwe.

3. Chadema na misingi yao: chama kinajiita cha demokrasia ila ukileta mawazo mbadala unaitwa msaliti. !

hali hiyo ingelikuwa kama unavyojaribu kutuaminisha, CDM isingeliwahangaisha watabiri wa kifo chake
Inawasumbua zaidi wanachadema kuliko hao watabiri wa nje. Chama cha demokrasia, inakuaje mawazo mbadala yanajafiliwa magazetini na mitandao ya jamii, kwa kutumia insinuations au majina bandia, wanashindwa kuyajadili vikaoni?

kuhusu ufisadi: serikali imeshindwa kuwakamata mafisadi wa CDM hadi watu mbweke hapa kama......asiye na meno? wachunguzeni
kuhusu posho" hivi nani alilianzisha hili la posho? kiranja wa bunge ni nani na wa chama gani vile? :A S-confused1::help:
Hili la posho linauma sana maana linaonesha watu wanataka posho ili wao KWANZA waanze kufaidi. Na wanao pokea, wanao kataa, wanao lead kwa example wanajulikana. Not everybody is expected kukataa posho kwa sasa ambapo bado ni kanuni la bunge, ila tunategemea kuwaona wakipinga raise.


6. Chadema na dharau kwa wanachama:

kwa wewe kuliona hili, mtoto wa nursery haitamsumbua,(Ooop dont mind my language) teh teh teh
. Never mind kaka. Elimu yangu ni ya kawaida sana, average tanzanian. Ndio maana naweza kujilinganisha na any illeterate. Kama yeye kaelewa kwanini mimi wa kawaida kabisa nisielewi?

7. Chadema na sera za wananchi:

walisema elimu itatolewa bure. walisema wakipewa madaraka mfuko wa saruji utashuka bei, n.k. hizi zilikuwa sera za mtu binafsi, mgombea wa Uraisi 2010, Dr W Slaa. Hakika hazikuwa za chama
Nani anaedelea hiyo agenda tangu yeye kuachana na ubunge? The only example of collective strugle dates waaaay back .

have you ever stopped doubting CDM in your life? NB: Bila kujali itikadi za kisiasa na tukiacha unafiki, usaliti na ubinafsi taifa litasonga mbele kwa kasi ya ajabu
I can't stop doubting politicians. Sio ndugu zetu. Na political parties ni kundi la polititians. Nisipo doubt nitakua kondoo ninae pelekwa machinjioni. Kudoubt na kujiridhisha ni muhimu kwa manufaa ya nchi na kwa manufaa ya kudumisha siasa zenye kutetea maslahi ya wananchi.
 
Ni dalili za kuweweseka Mkuu maana wanajua fika kwamba CHADEMA ni ngangari, propaganda zao zote mbuzi za kuisambaratisha CHADEMA ili watimize ndoto yao ya kuitawala Tanzania milele zimegonga ukuta na huku CHADEMA ikizidi kuchanja mbunga.

Mlikuja na mbinu za ukabila zikagota! Mkabuni ile ya ukanda, ikayeyuka! Mkaparamia udini, haukulipa! Mkaibua ugaidi, ukawarudi wenyewe! Sasa mnapiga mayowe ya demokrasia! Mbinu hii nayo imeanza kuwarudi!! Sasa mnatapatapa mithili ya vifaranga wanaopigwa na mvua kali wakati mama yao akiliwa na kimbulu! Je baadaye mtakuja na mbinu gani tena?
 
Back
Top Bottom