Wanandoa wasiobahatika kupata watoto wafanyeje?

Dick

JF-Expert Member
Feb 10, 2010
477
8
Imetokea mara nyingine kuwepo kwa Wanandoa ambao hawajaliwi kupata (wa/m)toto kwa sababu mbalimbali zaidi sana kwa Ugumba au Utasa.

Kutokana na mambo mengi katika jamii inayotuzunguka, Wanandoa hao (baadhi yao) huachana, hutoka nje ya ndoa, huzunguka sana kwa waganga wa jadi, na wachache sana huendelea kuishi pamoja ndani ya ndoa.

Wana JF mnawashauri nini Wanandoa kama hawa?
 
Kama ikishindikana watoto wanaweza kuchukua watoto yatima wanaoshi katika mazingira magumu na kuwalea.Ni makubaliano kati ya watu wawili
 
Wamwombe Mungu kwa IMANI watapata mtoto kwani HAKUNA NENO GUMU lolote la kumshinda Mungu.
Mifano katika Bible.....
Hana mamake Samweli
Sara na Ibrahim
Elizabeth mamaye Yohana Mbatizaji
list goes on.
 
Naomba kujua.... Lengo la kuoana ni Kupata watoto??

Mi nilidhani kusaidiana katika maisha (kwa shida na raha)
 
Unajua watoto ni majariwa sasa huwa nashangaa mama akiwa hazai mtu anampiga chini why?Hakupenda awe ivyo ingawa kama alikudanganya then unaweza mtimua but otherwise NO.
Mkae mkubaliane ata kuadopt ila mkisikiliza maneno ya watu lazima mtimuane seriuosly.
Personally nimeoa juzi juzi tuu mungu akitujalia mtoto ntashukuru ila asipotujalia sitamwacha Mke wangu
 
Naomba kujua.... Lengo la kuoana ni Kupata watoto??

Mi nilidhani kusaidiana katika maisha (kwa shida na raha)
.........Baba Askofu,wewe kanisa lako hamsomi biblia? Biblia inasema .........zaeni mkaongezeke.Na ndio maana hao waliokosa watoto walimng'ang'ania Mungu mpaka awape watoto.Tatizo letu siku hizi maendeleo ni mengi....Lakini lengo mojawapo la ndoa ni watoto.
 
kupata na kukosa ni mipango yake Mungu, ni muhimu kuendelea na kumuomba Mungu tuu, hakuna dogo kwa Mungu.Hakuna kaburi la mgumba wasikate tamaa kwa kudra za Mungu
 
.........Baba Askofu,wewe kanisa lako hamsomi biblia? Biblia inasema .........zaeni mkaongezeke.Na ndio maana hao waliokosa watoto walimng'ang'ania Mungu mpaka awape watoto.Tatizo letu siku hizi maendeleo ni mengi....Lakini lengo mojawapo la ndoa ni watoto.

Asante Charity... Tunasoma Baibo, lakini kumbuka Mungu alimuumba Adam kwanza, then akasema "nitampatia msaidizi" ndio maana akamtoa katika ubavu wa Adam... baada ya hapo na pilika za hapa na pale ndio akawaambia kwamba "zaeni muongezeke mkaijaze nchi"... Lakini kwanza ilikuwa ni kusaidiana

Hili tatizo linakuzwa na pressure za watu wa pembeni sana... lakini inatakiwa watu waombe muongozo wa roho mtakatifu
 
Wanatakiwa kumshukuru Mungu kuwapa uhai na hiyo ndoa na kuwaepusha na masikitiko......wakati mwingine kuwa na watoto ni balaa pia....namjua bwana mmoja alijaliwa watoto watatu napesa nyingi sana....mmoja ni marehemu,waliobaki mmoja shoga mwingine msagaji....na yeye kaachana na mke hana raha na chochote pesa,ndoa,watoto.....analalama tu kama anayeonewa....pia si vibaya ku adopt watoto...wako watu wamejaliwa uzazi na uwezo wa kulea hawana...ni vema kuwasaidia...na zaidi ya yote watoto si wetu niwa MUNGU
 
Naomba kujua.... Lengo la kuoana ni Kupata watoto??

Mi nilidhani kusaidiana katika maisha (kwa shida na raha)

Watu wengine wanapenda sana kumkufuru Mungu. Wengine wanapenda kwenda kinyume na maagizo ya Mungu. Wengine wanapenda kumpangia Mungu.

Ukweli unabakia palepale: Ardhi na mbingu na vyote viijazavyo ni MPANGO wa MUNGU!!
 
.........Baba Askofu,wewe kanisa lako hamsomi biblia? Biblia inasema .........zaeni mkaongezeke.Na ndio maana hao waliokosa watoto walimng'ang'ania Mungu mpaka awape watoto.Tatizo letu siku hizi maendeleo ni mengi....Lakini lengo mojawapo la ndoa ni watoto.
sasa kuzaa na kuongezeka LAZIMA MUOANE?
 
.........Baba Askofu,wewe kanisa lako hamsomi biblia? Biblia inasema .........zaeni mkaongezeke.Na ndio maana hao waliokosa watoto walimng'ang'ania Mungu mpaka awape watoto.Tatizo letu siku hizi maendeleo ni mengi....Lakini lengo mojawapo la ndoa ni watoto.

Kupatikana au kutopatikana kwa watoto ni MPANGO WA MUNGU!

Laleni mmegane 24/7. Mvua inyeshe jua liwake. Upepo uvume bahari ikumbwe na mawimbi makali. Mwezi ung'ae Jua lichome. Mungu ndiye muamuzi wa KUPATA WATOTO.

Sasa temeni mate chini na mtubu dhambi zenu.
 
Naomba kujua.... Lengo la kuoana ni Kupata watoto??

Mi nilidhani kusaidiana katika maisha (kwa shida na raha)

Askofu katika ndoa zetu za kiafrika ni muhimu kupata watoto ndani ya ndoa maana mkibahatika mara nyingi huboresha zaidi ndoa, lakini katika nchi za wenzetu sasa hivi wengi wanaoana huku wakiwa wamekubaliana kwamba hawatakua na watoto katika ndoa yao ili kutoharibu pattern ya maisha yao wanayoyafurahia na cha kushangaza idadi ya wanandoa kama hawa inaongezeka kwa kasi sana na hivyo kupunguza mno birth rates katika nchi mbali mbali za dunia ya kwanza lakini sijui kama hili litaingia katika nchi zetu hivi karibuni. Bado tunathamini sana kupata watoto ndani ya ndoa na kama wanandoa wasipojaaliwa basi ndugu, jamaa na marafiki huanza kuongea pembeni.
 
Nasubiri jibu la swali hili ili niwahi Drogba Vs Ronaldo.
namsubiri charity hapa!...
kumbu kumbu zangu zinaniambia kwa madhumuni ya kuzaana tu na kuijaza dunia
1-ABRAHAMU ALIMEGANA NA KIJAKAZI
2-YAKOBO NAE ALIT.....A NA KIJAKAZI
3-RUTHU ALIWALALA MABINTI ZAKE

well!...
 
Ahsante honey. Leo tutaimba wimbo mmoja

Duh School mate upo fastaa - kumbe una kina honey humu humu JF. safi saana. nifanyie mpango na mimi. tutakutana kule kwa wakubwa siyo hapa lakini.

Kuhusu swala la watoto ktka ndoa naunga mkono wazo lako - Yote kwa mungu Muweza......
 
Kupatikana au kutopatikana kwa watoto ni MPANGO WA MUNGU!

Laleni mmegane 24/7. Mvua inyeshe jua liwake. Upepo uvume bahari ikumbwe na mawimbi makali. Mwezi ung'ae Jua lichome. Mungu ndiye muamuzi wa KUPATA WATOTO.

Sasa temeni mate chini na mtubu dhambi zenu.

aaaaaaaaah
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom