Wanandoa ni Lazima Wa-share Password za Akaunti Benki na Simu.

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
WANANDOA NI LAZIMA WA-SHARE PASSWORD ZA AKAUNTI ZA BENKI NA SIMU

Anaandika, Robert Heriel
MTIBELI.

Dunia ya kitapeli huzalisha ndoa za kitapeli, Wanandoa matapeli, Watoto na kizazi cha kitapeli.

Kama mnafichiana namba za Siri za BENKI na akaunti na bado mnadanganyana ni MKE na Mume basi ninyi ni matapeli na Wanafiki Kwa kiwango cha juu. Hakunaga ndoa Hapo. Ni ujanja ujanja. Watibeli ni Bora kuishi mwenyewe kuliko kuishi na mtu ambaye humuamini au hakuamini.

Uaminifu ndani ya Ndoa ni moja ya Nguzo muhimu Baada ya upendo.

Kama MTU hajawa tayari kukupenda, kukuamini na hujawa tayari kumpenda na kumuamini ni Bora kila MTU apite kivyake.
Hakunaga ndoa ya Aina hiyo.
Hapo kitakachofuata ni ubinafsi wa kushangazaa.

Watibeli, naam Mimi kama Mtibeli ninawaagiza Vijana na mabinti, ili ndoa zenu ziwe ndoa kweli basi itahitaji mambo Makubwa yafuatayo;
1. Upendo, hapa tutazungumzia Moyo.
Ishu za kujali, kuthamini, kutunza na kuhudumia na mambo yote yahusuyo Hisia.

2. Imani, Hapa tunazungumzia Roho.
Hapa tunazungumzia ishu za Uaminifu, maadili na uadilifu, Tabia, kusamehe, na mambo yote yahusuyo Imani.

3. Utashi, hapa tunazungumzia Nafsi.
Mambi yahusuyo utambuzi, Akili, mtazamo, hasira, chuki, Mema na mabaya, n.k.

Hayo mambo Matatu lazima mkaribiane Kwa kiwango kikubwa. Kama mnapishana Sana basi hapo hakuna Ndoa. Lazima Haki za mmoja wenu zikanyagwe, na maumivu lazima yatokee. Hatimaye ndoa inakua ndoano.

Hakuna sababu yoyote ya maana hata Moja ya kumzuia Mwenza wako asijue Mambo yako nyeti kama Password ikiwa kweli mnasema mnapendana. Penye upendo hakuna sababu ya namna hiyo.

Unapoamua kuoa au kuolewa unaamua kuyafanya Maisha yako kuwa ya mwingine na Yale ya mwingine kuwa Maisha yako.
Mwili wako kuwa mwili wa mwingine, na wake kuwa wako
Siri zako kuwa siri za mwingine, na zake kuwa zako.
Madhaifu yako kuwa madhaifu ya mwingine, na yake kuwa yako.
Mali za mwingine kuwa zako, na zake kuwa zako.
Hiyo ndio ndoa.

Mwenza wako anapoficha Mambo yake ikiwemo namba za Siri anajaribu kueleza Jambo moja kuu kuwa Hakuamini, na kama Hakuamini basi ni kuwa Hakupendi Ile yenyewe.

Mtu Mwema na mwenye Upendo WA dhati haoni shida ku-share vitu na MTU anayempenda,

Ingawaje Kutokana na dunia hii kuwa na matapeli wengi, hasa Wanawake wanaopenda wanaume Kwa sababu ya Mali. Basi ni akheri
 
Namba za siri za benki na mobile money naweza mpa,ila Kuna vitu vyangu private ambavo havihusiani na usaliti wa ndoa au kuhatarisha ndoa yetu. Mfano vitu vya kazi,siri za watu wengine na mambo yangu binafsi zaidi.
Ndoa haina maana mtu avunje individuality yake yote kabisa.

Mwanamme unatakiwa hata ukimpa simu mkeo aangalie mwenyewe aogope kupofuka macho, aseme hapana baba.

Akaunti ya Benki unampa card na PIN ajichotee anavyotaka.

Siyo unaanguka unaumwa, hela zipo, lakini hakuna anayeweza kuzitoa.
 
95% ndoa hazina sifa hizo kuu Upendo zero, Imani zero, Utashi zero ❤️❤️❤️
 
Ndoa haina maana mtu avunje individuality yake yote kabisa.

Mwanamme unatakiwa hata ukimpa simu mkeo aangalie mwenyewe aogope kupofuka macho, aseme hapana baba.
Ndoa haina maana mtu avunje individuality yake yote kabisa.

Mwanamme unatakiwa hata ukimpa simu mkeo aangalie mwenyewe aogope kupofuka macho, aseme hapana baba.

Akaunti ya Benki unampa card na PIN ajichotee anavyotaka.

Siyo unaanguka unaumwa, hela zipo, lakini hakuna anayeweza kuzitoa.
Nakubali nakubali, this is the Anthem for all men out there. 💪
 
Mkuu nakuunga mkono,hii inawezekana kwa wanandoa wanaopendana,mke wangu anaweza maliza mwaka hajaenda benki ni mimi na kadi yake ,na yeye pia anajua nywila zote za simu na bank,hii ni nzuri binafsi sina hofu na mke wangu na sidhani kama anaweza shikwa na tamaa ya kunipora.
 
WANANDOA NI LAZIMA WA-SHARE PASSWORD ZA AKAUNTI ZA BENKI NA SIMU
Ah Wapi! Hakuna kitu kama hicho, ndoa ni mkataba wa kuishi pamoja na kutengeneza familia tu, hakuna kuaminiana wala hakuna kitu kinaitwa mapenzi, kuna kitu maslahi tu. Ndio yanayotufanya kua pamoja na maslahi yakiisha kila mmoja ataelekea upande wake.
 
Sasa kama mtu unamvulia utupu wako na kumuacha auchezee wakati toka asubuhi mpaka jioni watu unawaficha kwa kuvaa nguo ili wasione uchi wako

Sembuse password ya simu?

Siku zote definition ya mficha password za simu ni kumaanisha sio mwaminifu
Passwords ni zaidi ya kuvua nguo uonwe tupu.Hata mtoni watu huvua nguo kwa sababu wavuaji wanajua huwezi "kudukua" wala kutwaa viungo vyake.
 
Back
Top Bottom