Viongozi wa dini mnafanya nini? Mbona mauaji baina ya wanandoa yanazidi?

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Niende moja kwa moja kwa mada, visasi baina ya wanandoa chanzo cha mauaji ya wanandoa.

Kumekuwa na visa mbalimbali baina ya wanandoa kutoana uhai na mauaji hayo yamekuwa yakutisha sana.

Wengine wanauana kwa kuchomana visu na wengine wanauana kwa risasi.

Kuna ambao walishaua na wakazika wenyewe ila naona hayaongelewi na kanisa kabisaa.

Sasa imezoeleka kuwa ni kama kawaida ila sio kawaida kabisa kuna shida ndani ya ndoa za watu mbalimbali.

Ajabu ni kuwa wachungaji hawaongelei juu ya haya masuala yanayotokea kwa ndoa, hawahubiri kwa kutilia mkazo suala hili la ndoa wameacha kabisa.

Wamekazania kuhubiri mambo mengine tu ila suala hili la ndoa wameliweka mbali kabisa yaani, wanawaacha wanandoa wanaokufa tu kila mara.

Wanandoa wamekosa neno la kuwahamasisha na kutia moyo, kama neno uchumi na sadaka linavyotiliwa mkazo huko makanisani.

Kuna moto unawaka baina ya wanandoa wengi ila unawaka na kuzima na kuacha majivu juu ila moto upo chini.

Moto huu ni magomvi baina ya wanandoa ambayo yamekuwa yakihifadhiwa ndani ya mioyo ya baina ya wanandoa.

Chuki zimekuwa nyingi maana hawana mahali pa kuongelea mambo yao, watu wamebeba mizigo miyoyoni mwao.

Wanajua kabisa hakuna mahali ambapo patawasaidia na kuwawekea huru, ndio maana wameamua kuchukua hatua ya kuua maana kifo ndicho mliwaambia kitawatenganisha.

Wachungaji, kama kuna eneo ambalo linatakiwa kuhubiriwa kwa wingi ni hili la ndoa maana limeingiliwa na mauaji sana.

Ifike mahali wachungaji na Manabii wasimamie neno la kuweza kuoakoa wanandoa na ndoa zinazokufa na wanandoa kufa.

Wachungaji mmekuwa vinara wa kufungisha ndoa wandoa ila namna ya kuweza kuwafanya wakae kwa furaha mumewaacha wao wenyewe.

Kila mara mmekuwa mkihubiri watu kuoa na kuolewa mara utapata ndoa na ifike mahali muwafundishe na namna ya kuishi huko kwenye ndoa na kudumu kwa amani.

Watumishi wa Mungu amkeni, ndoa zimeingiliwa sana na mauaji na kuvunjika.

Donatila
 
Wachungaji wenyewe ndoa pia zinawashinda

Mchungaji wangu sasa ni mwezi kaachana na mkewe wana watoto 3
kisa mama mchungaji katoa mimba ya mwanaume mwingine

Huku mama mchungaji anadai mumewe alimsaliti na mzee wa kanisa
Walitishiana hadi visu nusu kuuana.
 
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari,

Niende moja kwa moja kwa mada, visasi baina ya wanandoa chanzo cha mauaji ya wanandoa.

Kumekuwa na visa mbalimbali baina ya wanandoa kutoana uhai na mauaji hayo yamekuwa yakutisha sana.

Wengine wanauana kwa kuchomana visu na wengine wanauana kwa risasi.

Kuna ambao walishaua na wakazika wenyewe ila naona hayaongelewi na kanisa kabisaa.

Sasa imezoeleka kuwa ni kama kawaida ila sio kawaida kabisa kuna shida ndani ya ndoa za watu mbalimbali.

Ajabu ni kuwa wachungaji hawaongelei juu ya haya masuala yanayotokea kwa ndoa, hawahubiri kwa kutilia mkazo suala hili la ndoa wameacha kabisa.

Wamekazania kuhubiri mambo mengine tu ila suala hili la ndoa wameliweka mbali kabisa yaani, wanawaacha wanandoa wanaokufa tu kila mara.

Wanandoa wamekosa neno la kuwahamasisha na kutia moyo, kama neno uchumi na sadaka linavyotiliwa mkazo huko makanisani.

Kuna moto unawaka baina ya wanandoa wengi ila unawaka na kuzima na kuacha majivu juu ila moto upo chini.

Moto huu ni magomvi baina ya wanandoa ambayo yamekuwa yakihifadhiwa ndani ya mioyo ya baina ya wanandoa.

Chuki zimekuwa nyingi maana hawana mahali pa kuongelea mambo yao, watu wamebeba mizigo miyoyoni mwao.

Wanajua kabisa hakuna mahali ambapo patawasaidia na kuwawekea huru, ndio maana wameamua kuchukua hatua ya kuua maana kifo ndicho mliwaambia kitawatenganisha.

Wachungaji, kama kuna eneo ambalo linatakiwa kuhubiriwa kwa wingi ni hili la ndoa maana limeingiliwa na mauaji sana.

Ifike mahali wachungaji na Manabii wasimamie neno la kuweza kuoakoa wanandoa na ndoa zinazokufa na wanandoa kufa.

Wachungaji mmekuwa vinara wa kufungisha ndoa wandoa ila namna ya kuweza kuwafanya wakae kwa furaha mumewaacha wao wenyewe.

Kila mara mmekuwa mkihubiri watu kuoa na kuolewa mara utapata ndoa na ifike mahali muwafundishe na namna ya kuishi huko kwenye ndoa na kudumu kwa amani.

Watumishi wa Mungu amkeni, ndoa zimeingiliwa sana na mauaji na kuvunjika.

Donatila
Mnasumbua manabii wenu wa mchongo
20240110_104947.jpeg
 
Haki sawa, wanawake wa siku hizi ni vijogoo kwenye familia. Wanafokea wanaume kama watoto na kusababisha stress na kutokuelewana. Kwa wanaume halisi kinachotokea ni ama zangu ama zake
Nilichoapa ni kwamba sitokaa niwe na mwanamke mmoja japo kwa sasa naishi na mmoja, hata awe na heshima kiasi gani. That's is my commitment
 
Back
Top Bottom