Wanandoa na extended family


ushakuwa na mawazo hasi juu ya ndugu kabla hata ya kuolewa...dah!
 

chakula ndo kila ktu hasa kwa sisi wabongo
hata ukirudu kwenu watakuuliza vp kula lakini
mtu mwenye roho mbaya lazma akunyime kula maana atahisi we unammalizia au umezidisha bajeti
bila kula husomi,hulali usiku utahesabu kenchi
bila kula utadhoofika
kula kwqnza ndo msingi wa yote
 

Hakuna guarantee kwamba ukiwasaidia ndugu watahudumia familia yako ukikutwa na mauti. Kama hao ndugu hawawezi hata kukusalimia ukiwa hai, wataanzia wapi kuhudumia familia yako ukitangulia mbele za haki?

Kwa nini tusiwekeze kwenye vitega uchumi vyenye uhakika au bima?

Habari yandu sitaki kusikia kabisa!
 
ushakuwa na mawazo hasi juu ya ndugu kabla hata ya kuolewa...dah!

Tafadhali mkuu, mbona kuni-attack hivyo, ni wapi nimekuwa na mawazo hasi?

Nimeileta hii thread tujadili kama nilivyoona matatizo katika ndoa na mahusiano ya rafiki zangu.

Nahitaji kufahamu nini chanzo na solution. "Don't put words in my mouth"
 

Usemalo ni kweli mkuu, ubinafsi ubinafsi ubinafsi. Utakuta mwanamke kaolewa na kawakuta ndugu wa mume na mume wanaishi vizuri.

Lakini kimbembe afike mke wale ndugu wataonekana wabaya ilhali miaka kadhaa wamekuwa wakiishi na kaka yao kwa amani.
 
hakuna guarantee kwenye chochote duniani mkuu, hata vitega uchumi vinaweza kufa, hata bima watoto bila msaada na ushauri mzuri wanaweza itumia vibaya, kumsaidia ndugu yako unamsaidia sababu ni damu yako, na ni investment kama nyingine tu unaweza pata return au usipate, mimi naamini katika kusaidia ndugu zangu ila sio kukaa na nao kibao home kwangu, huo ulikuwa mfano tu.
 
ukishakuwa na msemo kuwa NDUGU WA MUME HATA UMBEBE MGONGONI HARIDHIKI kwenye akili yako hutakaa ukawa na amani....
kila watakachofanya hata kama ni yale ya kawaida ambayo hata mamaako au dadaako au kakaako angefanya ww utaona wanafanya kwa sababu ni ndugu wa mume..

WANAWAKE; acheni kuwa na inferiority complex.. itawatesa sana..

chukulia maisha simple... MBONA SIMPLE TU?
 
Loo pole kwa hivyo ukawa na familia mbili?
Nilikuja kujua kumbe kweli Mdigo Mzigo shemeji yangu alipokuja kuishi nasi pamoja na mke na watoto wanne.Mie Karucee lo!
 

Wengi wetu hatuwezi kufuata mifumo tunayoikuta kwenye nyumba za wengine, tunataka tuishi tunavyotaka bila kufuata taratibu zilizoko. Na kuna wengine wanafanya kwa makusudi judt to provoke wenye nyumba na hapa siongelei ndugu wa mume, hata ndugu wa mke wanaweza kuwa tabu tupu.

Ni muhimu kuweka wazi kwa ndugu that your house is not a hotel to hang around. Ndugu watakaribishwa kusalimia au kama wana jambo la kufanya muda utakapoisha na wamemaliza kilichowaleta kila mtu arudi kwake.
 
lakini ndugu zake yeye hawana masimango na wanaridhika!!!...mmh!

ndugu yangu sijui kwa nini wanawake wa kiafrika ni wabinafsi sana linapokuja suala la kusaidia ndugu. Anataka ndugu zake tu ndio wasaidiwe lakini sio wa upande wa mwanaume. wa kiume watabambikiwa kila aina ya roho mbaya ili mradi tu waonekane wabaya!! jamani wadada hatukuzaliwa peke yetu, tuna mama, baba, dada kaka nk. na wengine ndio waliochangia mafanikio yetu mpaka mkatuona hivyo tulivyo!!
 

Sasa kwa nini tatizo la uchoyo wa chakula wanalo wanawake zaidi? Mbona asilimia kubwa ya wanaume hawana mda na mambo ya misosi?
..yaani mtu kuja kwa kupata lunch unaona anachukua mamilioni ya shilingi?..worse enough, akiwa ndugu yako wala hutamaindi, ila akiwa wa mume utasema maneno ya ajabu.. Kwa nini??
 
Mfumo huo wa kijamaa na undugu umeshapitwa na wakati..... Sehemu nyingi duniani hakuna tena kubebana kama vile mtu anakilema!! maLovers wanaishi wawil na vitoto vyao kama wamezaa!!

kwani alijizaa na kujisomesha? bado tuko Afrika ambako extended family ni kitu cha kawaida. hatupo hizo sehemu unazoota wewe.
 
Labda uwe na roho mbaya na roho ya kisilani na wakati mwingine hizi roho mbaya za uchoyo huanza udogoni hivyo kama zitaendelea maana yake zinaweza kuingia hadi kwenye mahusiano na ndoa.kama ni mwanamke anza kujiassess unaishije na familia yako marafiki na jirani zako,kama huwezi kuishi nao vizuri basi hata ndugu wa mume watakushinda.unaambiwa tenda wema uende zako.. For me nadhani ni roho mbaya tu hakuna lingine because toka unaolewa unajua kabisa kuwa mumeo ana ndugu zake na IPO siku watakuja kwenu/ kwako kukutembelea ama kuishi kabisaa...na ndio maana tunaambiwa kama haupo tayari kuoa ama kuolewa
Ni bora ukae zako peke yako milele na daima.NDOA na iheshimiwe na watu WOTE, over!!
 
Nilikuja kujua kumbe kweli Mdigo Mzigo shemeji yangu alipokuja kuishi nasi pamoja na mke na watoto wanne.Mie Karucee lo!

huyo alizidi sasa khaaa! yaani mumlee yeye pamoja na familia yake! hata mie siwezi.
 

Ndugu yangu, ukitaka kuelewana na mtu yoyote epuka chakula chake.....take my Words....
 

Dada everlenk habari? Samahani, umeolewa?!
 
Last edited by a moderator:
for more than 14 yrs ndani ya ndoa, ndg wa mume hawajawah kuwa mwiba kwangu despite the fact that maudhi madogo madogo yapo na haya huyaepuki.

to me kila binadamu anakosea katika hali ya kbinadamu sana na zaid ya hapo kila unachotendewa ambacho ni kibaya/kizuri wewe binafsi umeplay part katika tendo hilo liwe jema ama baya.

ukishajua hivyo katika kila kosa hutamhesabia mtu kuwa na hatia, cha msingi ishi vizuri na kila mtu kwa kadiri ipasavyo, usiwepo unafiki, isiwepo chuki, yasiwepo masimango, uwe na matunda ya rohoni yaani utu wema, kuvumiliana, ukarimu, upendo na heshima.

hizi zimekuwa ni principle kwangu, and i do keep them, Mungu pekee ndiye anayenisimamia manake hata pale ninapotaka kuchoka bado hunihubiria kwamba mtu akienda katika machezo hapewi taji hata asiposhindana kwa halali na pia hakuna askari aandikwae kwenye vita af akayafanya ya dunia ili amfurahishe bosi wake, na pia yamfaa mkulima mwenye taabu nyingi za kazi kuwa wa kwanza kufaidi matunda ya kazi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…