aminiusiamini
JF-Expert Member
- Aug 25, 2011
- 3,577
- 2,227
Mimi kwa mawazo yangu nasema huyu askari ameonesha busara kubwa sana. Ingekuwa ni wale fyatu angeweza kuua hata watu wanne au kumi na kusingizia kuwa walikuwa wanamzuia kufanya kazi au walikuwa wanataka kumnyang'anya silaha. Lakini pamoja na kuchochewa hasira amesoma mazingira na kuona ataumiza na kuwa watu wasiokuwa na hatia akaamua kuacha kutumia silaha tena hata hakufyatua hewani kuwatawanya. Ningekuwa mkuu katika jeshi la polisi ningempandisha cheo. Huyu amejua maana ya upolisi ni zaidi ya silaha na combat. Watu wa haki za binadamu wanapaswa kumpongeza sana huyu askari. Askari wengine wakiwa na bunduki hawakawii kufyatua hewani kuelekea kwa watu. Kwakweli huyu askari amenivutia sana ukiacha labda kosa alilofanya labda kusababisha ajali au chochote kile. Tungekuwa na askari wengi wa aina hii leo David Mwangosi na Akwilina Akwilini wangekuwa hai. Lakini bahati mbaya miongoni mwa polisi wapo fyatu wasiokuwa na akili na busara kabisa wao wanajua kufyatua risasi tu bila kujali nani atakufa au kuathirika. Hongera sana askari. Ndiyo maana mwananchi mmoja akasema KUNA TOFAUTI KATI YA POLISI NA TAKA TAKA. Huyu ni polisi kweli kweli sio taka taka kama wale waliouwa na kujeruhi wananchi wasiokuwa na hatia.
Mkuu angeua wangapi? Na yeye asingebaki. Katumia akili sana.