Wananchi wanyonge wa Chasimba Wazo wampinga Waziri Lukuvi wamwomba Rais Magufuli aingilie kati na kuwasaidia

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,975
Wananchi wanaoishi mtaa wa Chasimba na Chatembo eneo la Wazo Tegeta wamemwomba Rais Magufuli aingilie kati mgogoro wao na kiwanda cha Cement na kuwasaidia.

Wananchi hao wamesema uamuzi wa waziri wa ardhi wa kuwataka kumlipa mzungu tsh 6400 kwa kila mita moja ya mraba kufidia maeneo yao ya makazi hawauafiki.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama
 
Washauri waende mahakamani hili sio suala la no 1,watanzania tuwa ajabu mno kabla ya kupigania taasisi huru na independent sisi bado tunamkuza no 1 why? Nani katuvuruga kiasi hiki yaani kila kitu ni ikulu ndio iamue? Hii in issue ya kisheria sio kisiasa.
 
Hilo suala lao lilishawahi kupelekwa mahakamani au bado, huo mgogoro ni wa muda mrefu sana, lakini wawe makini pia, wasijekimbilia mahakamani halafu mahakama ikaamua wamlipe mzungu kiasi kikubwa zaidi ya hicho cha waziri.

Huyo wanaemuomba msaada hawasikii kelele za kumtafuta zinavyopigwa? vyema hao wakazi wakatambua tu hata huyo mzungu pia ana haki zake.
 
Hilo suala lao lilishawahi kupelekwa mahakamani au bado, huo mgogoro ni wa muda mrefu sana, wawe makini pia, wasijekimbilia mahakamani halafu mahakama ikaamua wamlipe mzungu kiasi kikubwa zaidi ya hicho.
Ushauri mzuri!
 
Eneo walilovamia lina hati ya kiwanda cha Twiga Cement na waziri kawafafanulia vizuri tuu na thamani ya eneo ni bilioni 60 or 50 kutokana na mali iliyopo humo na kuna wanahisa Watanzania kwenye hiyo kampuni.

Wanachotaka kiwanda 10B waachie ili nao wapewe hati nyingine na wananchi wapewe hati nao. Sasa raisi awasaidieje?hikiwa hawataki kumsikiliza waziri. Maana haki sio wao tuu hata wenye kiwanda wahaki.

Haya wamsubiri atakuja kuwasaidia
 
Washauri waende mahakamani hili sio suala la no 1,watanzania tuwa ajabu mno kabla ya kupigania taasisi huru na independent sisi bado tunamkuza no 1 why?nani katuvuruga kiasi hiki yaani kila kitu ni ikulu ndio iamue?hii in issue ya kisheria sio kisiasa.
Lissu alishasema hili. Raisi kawa kama Mungu.
 
Waliopinga ni Chatembo na Chasimba tu,

Chachui wao wameridhika na maamuzi hayo....!

Yaani Chasimba, Chatembo, Chachui wote wameungana kupambana na Chatwiga (mzungu) lakini walio asisi majina haya nashauri watafutwe, ndo waliotutengenezea huu mgogoro.
 
Eneo walilovamia lina hati ya kiwanda cha Twiga Cement na waziri kawafafanulia vizuri tuu na thamani ya eneo ni bilioni 60 or 50 kutokana na mali iliyopo humo na kuna wanahisa waTZ kwenye hiyo kampuni.Wanachotaka kiwanda 10B waachie ili nao wapewe hati nyingine na wananchi wapewe hati nao.Sasa raisi awasaidieje?hikiwa hawataki kumsikiliza waziri.Maana haki sio wao tuu hata wenye kiwanda wahaki.Haya wamsubiri atakuja kuwasaidia
Huu ndio ukweli mtupu. Washukuru mwekezaji amekubali kuachia eneo wamlipe fidia ndogo ya 6000 /sqm ni heri wapambane hata kuahid kulipa kwanawamu ila wakikataa zaidi itakula kwao.

Mwekezaji ana wanahisa na wanahisa wanahesabu mali yao na mali haigawiwi hovyo bila Wana hisa kukubali. So kama wanahisa wameamua kuwaachia wananchi inabidi wakubali tu.

Kumbuka hicho kiwanda kiliwekwa kule miaka ya sitini ikiwa ni porini kuepuka vumbi na uchafuzi wa mazingira wenzetu wanajua haya mambo ila sababu kiwanda kiliattract fursa mbalimbali watu wakakifuata kiwanda.

Wao walikuwa wanajichukulia maeneo bila kupima wajue mipaka ya kiwanda ni ipi? Walidhani kiwanda kinaishia kwenye fence tu kumbe kuna free zone ambayo kiwanda imeweka kwa ajili ya kuzia wananchi wasisogelee.
 
Wananchi wanaoishi mtaa wa Chasimba na Chatembo eneo la Wazo Tegeta wamemwomba Rais Magufuli aingilie kati mgogoro wao na kiwanda cha Cement na kuwasaidia....
Uamuzi wa Lukuvi unaleta mashaka kwamba kala rushwa nzito sana kutoka kiwandani .
 
Hilo suala lao lilishawahi kupelekwa mahakamani au bado, huo mgogoro ni wa muda mrefu sana, lakini wawe makini pia, wasijekimbilia mahakamani halafu mahakama ikaamua wamlipe mzungu kiasi kikubwa zaidi ya hicho cha waziri.

Huyo wanaemuomba msaada hawasikii kelele za kumtafuta zinavyopigwa? vyema hao wakazi wakatambua tu hata huyo mzungu pia ana haki zake.
Inasemwa kuwa lilifika mahakamani na hukumu ilishatoka kuwa eneo ni la mwekezaji na wananchi wavamizi wakaamriwa kuvunja majengo yao na kuondoka.

Wizara ya Ardhi ikaona iingilie kati kwa kujadiliana na mwekezaji kuwaombea hao wakazi wasiondoke kwa kuwa wameshajenga makazi hapo, ndio mwekezaji akakubali ombi la wizara kwa kutaka arejeshewe fedha kiasi ili anunue mahali pengine, yaani wakazi walipie viwanja walivyopo lakini kwa bei ndogo kuliko ile ya soko wakati huu, naona ndio wananchi wanapinga tena
 
Kesi ilienda mahakamani wananchi wakashindwa,wakakata rufaa wakazuia wasibomolewe hadi rufaa isikilizwe ,wakashindwa rufaa,wizara ikawasiliana na kiwanda ikawa wameomba 8000 wazungu wakagoma wakataka bei halali 20,000/ ya thamani halisi,wakaombwa bodi ikakaa wakashushiwa hadi 6400/kama wanasubiri Raisi sawa
 
Wananchi wanaoishi mtaa wa Chasimba na Chatembo eneo la Wazo Tegeta wamemwomba Rais Magufuli aingilie kati mgogoro wao na kiwanda cha Cement na kuwasaidia....
Watu waliozoea kuishi squatter kila kitu wanataka kiwe bure, kama machinga.

Watu waeleweshwe kuwa kulipia premium ya Ardhi ni zaidi ya kiasi hicho.
 
Back
Top Bottom