Kwangu mimi Rais Magufuli amefanya jambo la haraka kumuondoa Naibu Waziri wa Madini, hakuna uhusiano wowote kati ya kuzungumza na kufanya kazi

Course Coordinator

JF-Expert Member
Jul 27, 2019
1,681
3,063
Francis Ndulane alikuwa Mhasibu Mkuu wa Tanroads Mkoa Lindi, Magufuli alipo ingia Madarakani kama Rais akamteua kuwa Mkurugenzi wa Mji Ifakara.

Mwaka huu akagombea ubunge, kwenye kura za maoni ndani ya chama akashika nafasi ya tatu kwa kupata kura 21 nyuma ya Ahmed Raphael Bongi aliyekuwa amshindi wa kwanza kwa kura 155 ambaye alikuwa ni Mhasibu mkuu wa Mkoa wa Lindi.

Ila kamati kuu ya CCM ikarudisha jina aliyeshika nafasi ya tatu Francis Ndulane kuwa mgombea jimbo la Kilwa kusini.

Rais Magufuli mwenyewe ameunda Baraza lake baada ya kupita takriban wiki 3 baada ya uchaguzi kupita ,hivi bila shaka alijidhihirisha kuwa ni mtendaji mzuri.

Kilichompata ndugu yetu kinaweza kumpata mtu yeyote katika mazingira yoyote mathalani ni jambo furaha hivo mhusika alikuwa yuko temper.

Mh. Francis Kumba Ndulane. Mbunge wa Kilwa kaskazini - CCM aliyekuwa ameteuliwa kuwa Naibu Waziri Nishati, kwa bahati mbaya ameondolewa katika nafasi hiyo kwa kile kinachodaiwa kushindwa kuapa. Mh Ndulane anaonekana katika video akisoma kiapo kwa kusitasita kama anakigugumizi (stama).

Kilichompata Mh. Ndulane kisaikolojia kinaitwa ' Occasional Anxiety'. Kiufupi ni hali ya wasiwasi isiyotarajiwa inayomkuta mtu kufuatia jambo fulani kumpata au kulazimika kulifanya.

Jambo hilo laweza kuwa geni kabisa au kutokana na uzito wake likawa na mvuto mkubwa kijamii. Mazingira haya hutufanya baadhi yetu kuingiwa na wasiwasi hatimaye kushindwa kulifanya kwa ufanisi unaotarajiwa.

Katika mazingira ya uanafunzi, baadhi wanapokuwa katika vyumba vya mitihani ya taifa hukumbwa na hali hii. Hukuta hata mwanafunzi anashindwa kushika kalamu na kujikuta vidole vikitoa jasho huku mkono ukitetemeka,saa zingine hutokea wakati wa ku-present kitu ,niliwahi kusoma na msichana yani alipoingia panel alizimia kabisa.

Baadhi yetu tumeshuhudia katika mazingira ya vyuo vikuu, wanachuo wenzetu wakishindwa kusimama mbele ya wanafunzi wenzao na kuzungumza. Ipo mifano mingi.

Hali hii huwa haina kusema umesoma shahada (degree) ngapi. Ni tendo kisaikolojia. Katika matukio kama ya kuhutubia, kuapishwa nk.ndio maana ili kupunguza uwezekano wa kutukia kitu kama hicho, watu hulazimika kufanya kitu kinaitwa ' rehearsal' kabla ya tukio husika.

Tusimshambulie mh. Francis Ndulane kama mtu wa ajabu kwakuwa kilichomtokea, kimewatokea wengi na kitawapata wengi.

Tusimfedheshe. Tumfariji, hasa ukizingatia kapoteza fursa adhimu ambayo wengine huitafuta kwa udi na uvumba,wengine hutoa hadi kafara.

Hapo washauri wa Mh.Rais wanatakiwa kumshaauri vizuri haikupaswa hatua ya kumwondoa iwe kwa haraka vile. Lile ni jambo la kawaida sana.

Hakuna uhusiano kati ya utekelezaji majukumu kwa ufasaha na uwezo wa kuzungumza na ikizingatiwa kwa Ndulane nafasi kubwa kama ile nadhani ni ngeni na ni mara ya kwanza kwake kuteuliwa kuwa naibu waziri , lkn wkt mwingine feelings na namna mtu anavyolichukulia jambo kwa uzito mkubwa huweza kumfanya yeyote akakutwa na hali ile hali...ukichukulia ule ukali wa Magufuli wa kuwatukana mawaziri wapumbavu ndo basi kabisa Ndulane alitaka afanye haraka amalize.

Hata leo Biden alikuwa anaapisha baadhi ya watendaji kuna mama alikuwa anakosea hadi lugha lakini hamkumuondoa.

Tujifunze kuvumiliana.
Thats why there is always a room for the second chance.
Najua washauri wa Rais watamshauri ampatie jamaa nafasi ya pili..Majaliwa na Makamu wa Rais kasi kwenu.
 
Naomuomba mh. Raisi amurudishie nafasi yake. Maaana mpaka ampe uteuzi ule kunamambo alichunguzwa ya kiutendaji ambayo ni inje na kiapo cha kutumiaa yale maandishi. Kwa kuwa raisi wangu nimsikivu, naomba alirudishe jembe hiliii. Sisi tutalipima kwa vitendooo.
Binafsi ni muumini wa kumpa nafasi mtu mara ya pili.
 
Waziri siyo mtendaji bali anashughulika zaidi na sera sasa kama hawezi kuongea then he is unfit for the position.
Not for that extent...yule jamaa sio kwamba hawezi kuongea ni just high feeling imetokea au low confidence ukichukulia Rais na ule ukali wake ..waziri mkuu yuko pale..wenye suti nyeusi wako pale ...so akawa na temper ya kufa.

Chukulia alikuwa mhasibu wa mkoa zen mkurugenzi means Takukuru ,TISS ,CAG amekutana nao so leo sio Rais ashindwe halafu sio mara ya kwanza kuapa mbele yake ila ile position ndo huenda mhusika amechukulia kwa mihemko mingi.
 
Waziri siyo mtendaji bali anashughulika zaidi na sera sasa kama hawezi kuongea then he is unfit for the position.

Hawezi kuongea kivipi? Huyu ambaye ameshika nyadhifa byingi kabla hata ya kugombea ubunge bila shaka alikutwa na maswahibu ya kisaikolojia yaliyomfanya atekewe na kushindwa kuzungumza. Rais angetafakari kumpa nafasi nyingine.
 
Hatujui ni kwanini Rais alimteua (inawezekana Rais aliuziwa mbuzi kwenye gunia na wasaidizi wake), sasa baada ya kufungua gunia akakutana na kitu ambacho hakukitegemea, he was not impressived enough! Hivyo hata akimtumbua ni sawa tu.

Yote kwa yote, huyo jamaa huenda atarudishwa tena kwenye hiyo nafasi yake, jipe muda. Magufuli pale alikuwa anatafuta media attention tu, ni bingwa wa kutengeneza tatizo na kuja kulitatua.
 
Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani wakati wa raisi Jimmy Carter,
Edmund Muskie, aliingia kwenye mbio za kuwania uraisi kwa tiketi ya chama cha Democrats.

Katika mkutano na waandishi wa habari kwenye mbio hizo alionekana kujibu maswali kwa kutetemeka sana hadi kwenye vidole.

Mchambuzi mmoja wa habari akasema kesho yake:
“Nadhani wote tumeona jinsi seneta Muskie alivyokuwa akitetemeka jana. Ni wazi kuwa Marekani haihitaji mikono ya mtu kama huyu juu ya swichi za silaha zetu za nyuklia.

Hio ndio ikawa hatima ya seneta Muskie katika kuusaka uraisi wa Marekani!
 
Francis Ndulane alikuwa Mhasibu Mkuu wa Tanroads Mkoa Lindi, Magufuli alipo ingia Madarakani kama Rais akamteua kuwa Mkurugenzi wa Mji Ifakara...
Uko sawa,

Hili si mara ya kwanza kujitokeza katika uongozi wa JPM.Nakumbuka pia ilishawahi kumtokea Mh.Eng.Stella Manyanya,lakini mh Rais alimvumilia hadi akamaliza kiapo chake.

Mimi sina shaka kabisa na mh.Ndulane najua Jpm na wasaidizi wake walimchunguza kwa kina kabla na kumuona anafaa,hivyo mh.rais angempa nafasi tena atumikie taifa lake.
 
Binafsi mimi nakubaliana na wewe kuwa Mh Rais amefanya haraka sana kumtengua bado naona alipaswa kumpa nafasi huyu mtu yaliyotokea pengine yana hakisi ubinadamu.
 
Back
Top Bottom