masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,886
- 13,183
Rais Samia akiwa Iringa
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa, ziara ya Rais Mama Samia Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini imevunja rekodi.
Sikumbuki Rais aliyezungukia mikoa ya Mbeya, Njombe, Iringa tena kiwilaya na kuimaliza. Kwetu Mbeya Rais kaenda Chunya, Mbeya vijijini, Rungwe na Kyela.
Marais wengine toka enzi za Mwalimu waliishia aidha kufungua miradi kwa siku moja na kuondoka siyu hiyo hiyo.
Rais Mwinyi, Rais Mkapa, Rais Kikwete, Rais Magufuli wote walikuwa a one day visit presidents. Na kama walikaa zaidi basi ni wakati wa kampeni za Urais tu.
Hivyo Rais mama Samia amejipatia sifa kubwa kwa kuonekana na watu wengi katika mikoa hii.
Kilichobaki sasa ni kutekeleza ahadi zote zilizo ahidiwa na hao marais wengine, na hazikutekelezwa.
Viva Rais Samia.