Wananchi ni mfano mzuri zaidi wa wadai haki kwasababu wao ndio wanaoipa Mamlaka Wawajibikaji na mara nyingi wanalipia huduma wanazopata

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Tunaweza kusema kuwa kuna uwajibikaji wa kidemokrasia katika utoaji huduma pale ambapo wananchi au wawakilishi wao wanahoji au kutoa mrejesho kuhusu huduma za umma halafu watendaji wa kisiasa na watoa huduma ama wayafanyie kazi maoni hayo au wawajibishwe.

Kutokana na dhana hiyo ya msingi, uwajibikaji unabeba uhusiano kati ya watendaji wa aina mbili:
• Wawajibikaji ni maafisa wa kuchaguliwa na wasio wa kuchaguliwa au watoa huduma wa sekta binafsi wenye mamlaka na wajibu wa kufanya kazi yao na kutoa maelezo na kuhalalisha matendo yao na pia wanaoweza kuwajibishwa kwa matendo yao, mazuri au mabaya.

• Wadai haki ni wananchi au taasisi za kisiasa zinazowawakilishawananchi na zenye haki au mamlaka ya kuangalia/kusimamia utendaji wa wawajibikaji, kuwahoji na kuwahukumu pamoja na kutoa adhabu inapohitajika.

Wawajibikaji wanaweza kuwa serikali ya nchi au ofisi ya manispaa, wizara, ofisi ya uchunguzi wa malalamiko, kamati ya bunge, bunge lenyewe, shirika binafsi, au ofisi yoyote ya umma au binafsi au shirika lililopewa mamlaka ya kutoa huduma. Kwa kawaida
mamlaka hayo yanakuwa chini ya zaidi ya mdau mmoja.

Kwa upande mwingine, wananchi ni mfano mzuri zaidi wa wadai haki. Kwa sababu wao ndio wanaoipa Mamlaka Wawajibikaji na pia mara nyingi wanalipia huduma wanazopata. Mifano mingine ya wadai haki ni vyama vya kisiasa vya upinzani, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, kamati ya bunge yenye wajibu wa kusimamia utekelezaji wa sera za serikali, au watendaji mbalimbali wa kisiasa na kijamii wenye mamlaka ya kuwasimamia wale wenye wajibu wa kutoa huduma.
 
Back
Top Bottom