Wananchi Igingilanyi walia na Serikali kuhusu malipo duni ya fidia za nyumba zao kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Iringa

Mantombazane

JF-Expert Member
Sep 7, 2014
572
356
Sisi wananchi wa kijiji cha Igingilanyi kilichopo katika manispaa ya Iringa ambao tunatakiwa kuhama katika makazi na maeneo yetu ili kupisha upanuzi mkubwa wa uwanja wa ndege wa Iringa ulipo katika vijijji vya Nduli na Igingilanyi lakini kwa sehemu kubwa utachukua sehemu ya Ingilangyi ambako ndiko run way imeongezwa, tuna kilio kikubwa cha malipo kidogo sana ya fidia ya nyumba zetu tunazo takiwa kubomoa ili kupisha upanuzi huo.

Mradi huu ulianza miaka zaidi ya minne iliyopita ambapo wana nchi tulielimishwa kuwa tutakapo takiwa kuhama tutalipwa vizuri fidia za mashamba, mazao, makaburi na nyumba zetu. Tena maofisa wa TANROADS ambao ndio wajenzi wa uwanja huu walio kuwa wakitu elekeza kuwa serikali ita lipa vizuri upande wa nyumba zetu ili tukajenge makazi bora zaidi na waliahidi kufuatilia nyumba zitakazo kuwa zimejengwa baada ya fidia eti huhakikisha wanachi tumetumia vizuri pesa tutakazo kuwa tumpewa kama fidia ya nyumba zetu.

Lakini tarehe 17/08/2020 tuliingia simanzi na sononeko kubwa pale tulipo itwa katika ofisi za Tanroads za mkoa zilizopo katika kijiji chetu cha Igingilanyi ili kupokea fidia zetu tayari kwa kuhama. Baada ya kufika katika ofisi hizo wananchi hawatukupewa mchanganuo wa malipo tunayo stahili kabla. Badala yake maafisa wa manispaa chini ya aliye julikana kama Shirima akishirikiana na kiongozi mmoja kutoka Tanroads aliyeitwa Mgongolwa walianza kutuita waathirika mmoja mmoja na kututajia kiwango cha jumla tutakacho lipwa bila kutoa mchanganuo kisha kutakiwa kusaini malipo hayo. Hii ilikuwa ni mbinu ya gawanya ili utawale yaani divide and rule ambapo wananchi baada ya kutoka hatukuweza kujua thamani hasa ya kila kitu na malipo waliyotajiwa yalikuwa madogo sana.

Baada ya baadhi ya wananchi kufuatilia ikagundulika kuwa malipo yaliyo lipwa kama fidia ya nyumba yalikuwa ni madogo sana kiasi kwamba mtu anaweza kununua kiwanja tu na sio kujenga nyumba nyingine kama aliyokuwa nayo. Mfano unakuta mtu mwenye nyumba ya tofari za kuchoma, iliyo ezekwa kwa bati na kupigwa plasta ndani vizuri ikiwa na milango na madirisha yenye vyumba vinne analipwa Sh 2,800,000/= hapo nyumba nyingine katika eneo husika zinakuwa hazija ingizwa kwenye fidia. Mwingine analipwa mil 1.5, mwingine unakuta ana nyumba tatu au nne sehemu moja analipwa jumla mil 7 Vile vile katika malipo hayo hakuna malipo ya waiting time ambayo wana nchi tumepoteza kwa zaidi ya miaka minne tukisubiri kulipwa na kuhama kwani tuliambiwa tusifanye maendeleo yoyote toka 2017 wakati wenzetu wakijenga, kuweka huduma za maji na umeme lakini sisi tume kaa gizani bila maji kwa zaidi ya miaka minne sasa.

Hivi kwa malipo hayo kiduchu ni mwananchi gani anaweza kujenga nyumba kwa mil 1.5 au 2.8 ambayo wao walisema watakuja kukagua hasa ukitilia maanani kupanda kwa bei ya vifaa vya ujenzi? Kibaya ni kuwa maafisa hawa wamekuwa na lugha za kifedhuli na ubabe kila wanapo hojiwa kuhusu malipo hayo kidogo ya nyumba. Vile vile kuna mapunjo makubwa ya fidia ya kodi waliyo dai watalipa kwa miaka mitatu kwa kila chumba ili mtu apate muda wa kujenga nyumba yake nyingine. Malipo ya kodi wametoa kwa wastani wa sh 4,500/= hadi 6,000/= kwa mwezi. Je ni nyumba gani inapangishwa kwa kiasi hicho kwa mwezi?

Kwa ujumla zoezi la malipo ya fidia lina onekana kugubikwa na dalili za ufisadi mwingi au sivyo ni lazima maafisa walio husika kutathimni nyumba za wana nchi hawa watakuw na matatizo. Wananchi tumepaza sauti hadi kwa mkuu wa wilaya Mh. Kasesera lakini haja fika kwenye eneo la tukio umbali wa km 20 tu kutoka mjini kuja kusikiliza kilio chetu. Lakini DC huyu huyu anaweza kuwasha gari la serikali na kuingia nalo mitaani kwenda kusimamisha bajaji na kumshusha abiria aliye zidi katika kutafuta kiki. Alipopigiwa simu alisema wana nchi waandike malalamiko lakini katika mtafaruku ulipo hapa kijijni ili paswa afike kusikiliza kilio chetu na kusaidia kutoa ufumbuzi.

Wananchi sasa tumeanza kuweka matumaini yaetukwa rais tu kuwa ndiko tutakako shitakia kwa kuwa viongozi wa chini hawaoneshi kutu saidia. Tunajiuliza hivi hizo hela mil 1.5 au 2.8 zinaweza kujenga nyumba gani? Tunaomba wana nchi tulipwe fidia ya nyumba itakayo tuwezesha kujenga makazi mapya hatuna tatizo kabisa na mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege.

Kwa upande mwingine uongozi wa kijiji chini ya mwenyekiti na afisa mtendaji nao ukali geuza zoezi hili la ulipaji fidia kuwa ni la kuwapiga waathirika. Kilicho fanyika ni kuwa kila mwaathirika alitakiwa awe na barua ya utambulisho kutoka kwa afisa mtendaji wa kijiji. Walicho fanya ni kuwa waliandika barua ya mkono na kuipiga kopi za kutosha kasha kuanza kutupa au kutuuzia kwa sh. 5,000/= kila barua bila kutoa risiti wakidai ni za mchango wa zahanati. Tunajiuliza kwanini mchango wa zahanati uchangishwe kwa njia hii ambayo ni kilio kingine kwa wananchi? Na je mbona hawa kutoa risiti kama ni mchango unaoingia kwenye mfuko wa kijiji? Kwa mtindo huo viongozi wa kijiji chini ya afisa mtejndaji wametia kibindoni zaidi ya sh 600,000/= Tuna omba uongozi wa wilaya utusaidie viongozi hawa waturudishie pesa zetu kwani huu ni wizi wa kimacho macho. Utambulisho ni huduma kwa mwananchi na sio biashara.

Tuna tegemea kilio chetu kitasikika kwa mkuu wa mkoa, waziri wa ardhi na mbunge wetu mstaafu na wakishindwa wote tuna omba rais aingilie kati ili zoezi la upanuzi wa uwanja wa ndege liendeleee bila bugudha yoyote na sisi wana nchi twende tukata anzishe makazi mapya sehemu nyingine. Tuna omba uhakiki na malipo yafanyike mapema kabla ya mwezi wa kumi ili tuwahi kuanda makazi mapya kabla ya mvua za masika kuanza isije ikachelewa tukaanza kuondolewa wakati wa masika

Ni sisi wana igingilanyi
 
Uchumi wa kati!
Tanzania ya Vi-wonder...
Poleni, waliolipwa kupisha SGR Morogoro, hawakulalamika, walilipwa vizuri..

Mmesaini mmechukua, kimsingi mmekubaliana.. mmechelewa sana kulalamika!

Everyday is Saturday.......................... :cool:
 
Back
Top Bottom