DOKEZO Mwanza: Wananchi Sengerema wapinga kubomolewa nyumba zao bila fidia

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Pfizer

JF-Expert Member
Mar 25, 2021
305
519
Leo majira ya asubuhi hapa Wilayani Sengerema mkoani mwanza tulialikwa kwenye kikao cha watu kutoka TANROADS Mwanza wakielezea kuhusu mradi wa barabara ya Sengerema Buchosa agenda zao zilisema yafuatayo:

1. Watafanya upimaji hivi karibuni
2. Upimaji wa eneo la barabara ambao utajumuisha mita 22.5 kwa sheria ya mwaka 1932
3. Nyumba ambazo ziko ndani ya mita 22.5 zibomolewe bila kulipwa fidia
4. Zile mita 7.5 ambazo ziliongezwa miaka ya karibuni kukamilisha mita 30 kila upande wa barabara zisibomolewe lakini pia hazitalipwa fidia kwa sasa na nyumba isiendelezwe kwenye eneo hilo.

Hapo ndipo ikaibuka vurugu na kujibizana maneno Wananchi tukipinga suala hilo tukidai kuwa kama TANROADS wameamua kubomoa nyumba zetu kupisha utanuzi wa barabara basi watulipe fidia wasituletee Sheria ya Mwaka 1932 ambayo ilifutwa Mwaka 1999 na kufanyiwa marekebisho Mwaka 2007.

Hivyo, wafuate sheria ya fidia iliyopo wasilete za kwao za mwaka 1932, hayati Magufuli alikuwa akuhubiri karibu nchi nzima na hata hapa Sengerema alisimama Mapinda na kueleza kuwa Sheria ya fidia kwa kupisha utanuzi wa barabara itamuhusu aliyejenga kuanzia mwaka 2007 kurudi nyuma.

Wananchi tumepinga maelekezo ya TANROADS ambayo wameyatoa Leo hapa Sengerema na tunaitii Serikali kwa Sheria ya mwaka 2007 ya kulipwa fidia kwa utanuzi wa barabara.





 
Back
Top Bottom