Wananchi wa Rorya Watalipwa Fidia ya Kupisha Mradi wa TANESCO

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944

WANANCHI WA RORYA WATALIPWA FIDIA YA KUPISHA MRADI WA TANESCO

"Tayari TANESCO imekamilisha uthamini na uhakiki wa marudio ya mali zilizoathiriwa na mradi kwa sasa ipo katika hatua ya maandalizi ya Malipo. Malipo yanatarajiwa kuanza Novemba 2023 na kukamilika Disemba 2023. Tunaomba wananchi wanaosubiri kulipwa fidia wawe na subira wakati maandalizi ya Malipo yakiwa yanaendelea" - Mhe. Judith Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati

"Sheria ya Uthamini inatamka kuwa Thamani ya Ardhi inapaswa kulipwa Ndani ya miezi 6 lakini wananchi wamedai Malipo yao tangu mwaka 2011 na hawajalipwa. Itakapofika Novemba 2023 kama wananchi hawajalipwa Uthamini wa Ardhi yao Serikali itakuwa tayari kurudia Uthamini kwa mujibu wa sheria inavyotamka?" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Jambo hili limekuwa la muda mrefu toka mwaka 2011 na sasa lipo Ndani ya Ofisi ya Mkurugenzi, Ofisi ya TAMISEMI ni lini wanalipa fedha ili wathamini warudi kufanya Uthamini na upande wa TANESCO waweze kulipa fidia kwa wananchi" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Serikali imeshatenga fedha kiasi cha Shilingi Milioni 350 ili wananchi 231 wanaodai fidia walipwe ikifika Novemba 2023 na tutalifuatilia kwa ukaribu kuhakikisha linakamilika" - Mhe. Judith Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati

"Tayari Serikali kupitia TANESCO imeshatoa fedha kiasi cha Shilingi Milioni 15 kwaajili ya kukamilisha zoezi la Uthamini. Tutafuatilia kuhakikisha Halmashauri ya Rorya inakamilisha taratibu kwa wakati ili zoezi likamilike kama ilivyopangwa" - Mhe. Judith Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati

 
Mbunge wa Rorya, mbona unaleta mambo ya ovyo? vipi kuhusu wananchi wa Utegi wanaohamishwa kwa nguvu kama wamasaai kupisha Utegi Farm?

Vipi kuhusu kufidiwa ardhi yao? yaani mmelipe nyumba tu lakini ardhi msilipe huo ni unyonyaji na uonevu wanaofanyiwa wananchi wa Utegi.
 
Sioni umuhimu wako kama mbunge wa Rorya katika kutetea wananchi wapiga kura wako wa utegi.

Utegi tumeonewa sana na tunanyanyaswa na utawala wa CCM. Mbunge na madiwani mmehongwa na BARRICKS na mkaamua kuwauza sisi wapiga kura wenu wa Utegi subirini uchaguzi ujao
 
Back
Top Bottom