Wananchi Bagamoyo Waunga Mkono Uendeshaji Bandari Dar es Salaam

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Wananchi wa Bagamoyo mkoani Pwani, wataendelea kusimama na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha Bandari ya Dares Salaam inaleta tija zaidi kwa Watanzania wanufaike kichumi.

Hayo yalisemwa na Mbunge Viti Maalumu (CCM), Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, wakati akizungumza na wananchi katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la Shina Namba 4 la CM Magulumatali, Kata ya Talawanda ambapo mbio za
Bendera ya CMM zilifika kijijini hapo.

Subira alisema uwekezai huo wa Bandari ya Dar es Salaam, unatarajia kuiingizia nchi sh. trilioni 27 kwa mwaka, fedha ambazo zitaisaidia chini kwa kiasi kikubwa kutimiza malengo ya bajeti ya nchi. "Sisi wana Bagamoyo, tunatoa
salamu kwa wanaoendelea kuibeza serikali, hatupo pamoja nao na wasikanyage kabisa na kwa kuwa kupitia kampeni hii ya mbio za bendera, Chama kimeendelea kumarika wahesabu huku hawama chao," alisema.

Subira alisema bandari hiyo, haijauzwa bali ipo katika hatua za mwanzo za kuangalia makubaliano ambapo serikali itapata nafasi ya kuangalia na kurekebisha masharti ya mkataba wa bandari hiyo, endane na matakwa ya maslahi ya Watanzania kwa kushirikiana na wawekezaii hao kutoka Dubai. Aidha, aliwataka wana CCM,
wasikubali kupotoshwa na wanasheria uchwara, wanaopotosha umma
 
Hawa wananchi watakuwa na matatizo sana. Hivi hawafahamu DP World wamepewa Exclusive Rights to operate all ports within Tanzania. Hivyo ule mradi mkubwa wa Bagamoyo Mega Project ambao ulilenga kuugeuza Bagamoyo mji wa kibiashara ambao ungekuwa mkubwa hapa Afrika umeshakufa kibudu.

Bandari ya Bagamoyo ingetengenezwa ingekuwa inashindana na bandari kubwa duniani kama Rotterdam Netherlands. Lakini kubwa ni kwamba Bandari ya Bagamoyo ingekuwa ni Transhipment Port kwamba ingetumiwa na bandari nyingine ndogo-ndogo za Afrika. Hili lingepelekea nchi kama Dubai kupata ushindani mkubwa kibiashara.

Kiuchumi, kiulinzi na kidiplomasia tumewatendea vibaya mno watanzania kuingia kwenye mkatabwa wa hovyo kama huu wa Dubai. Ukiuliza serikali ilikuwa na haraka gani, huwezi kupata majibu yanayoeleweka.​
 
Siwashangai hao wabunge, ndio wale waliopitisha ule mkataba wa hovyo kule bungeni, ni mazezeta tu.
 
Wananchi wa Bagamoyo mkoani Pwani, wataendelea kusimama na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha Bandari ya Dares Salaam inaleta tija zaidi kwa Watanzania wanufaike kichumi.

Hayo yalisemwa na Mbunge Viti Maalumu (CCM), Mkoa wa Pwani, Subira Mgalu, wakati akizungumza na wananchi katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la Shina Namba 4 la CM Magulumatali, Kata ya Talawanda ambapo mbio za
Bendera ya CMM zilifika kijijini hapo.

Subira alisema uwekezai huo wa Bandari ya Dar es Salaam, unatarajia kuiingizia nchi sh. trilioni 27 kwa mwaka, fedha ambazo zitaisaidia chini kwa kiasi kikubwa kutimiza malengo ya bajeti ya nchi. "Sisi wana Bagamoyo, tunatoa
salamu kwa wanaoendelea kuibeza serikali, hatupo pamoja nao na wasikanyage kabisa na kwa kuwa kupitia kampeni hii ya mbio za bendera, Chama kimeendelea kumarika wahesabu huku hawama chao," alisema.

Subira alisema bandari hiyo, haijauzwa bali ipo katika hatua za mwanzo za kuangalia makubaliano ambapo serikali itapata nafasi ya kuangalia na kurekebisha masharti ya mkataba wa bandari hiyo, endane na matakwa ya maslahi ya Watanzania kwa kushirikiana na wawekezaii hao kutoka Dubai. Aidha, aliwataka wana CCM,
wasikubali kupotoshwa na wanasheria uchwara, wanaopotosha umma
Huu ndio ukweli.
 
Back
Top Bottom