Wanaku-Delude Kuwa Umeelimika, Ila Wewe Ni Robot Lao Tu, Maana Nje Ya Mfumo Wao Vyeti Vyao Vya Degree Ni Vifungashio.

Wanaku-Delude Kuwa Umeelimika, Ila Wewe Ni Robot Lao Tu, Maana Nje Ya Mfumo Wao Vyeti Vyao Vya Degree Ni Vifungashio.

SankaraBoukaka

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2019
Posts
2,603
Reaction score
4,028
Katika jamii ya leo, elimu imekuwa kama kipimo cha thamani ya mwanadamu. Certificate, Diploma na Degree vimechukua nafasi ya heshima, ajira na hadaa kubwa ya kijamii.
Hata hivyo, ukweli ni kwamba hiyo ni chicanery tu, unaambiwa na unajiona umeelimika kwa sababu umepokea uthibitisho wa kataratasi, ila hakika, wewe si kitu kingine zaidi ya roboti lao uliyesanifiwa kufuata mfumo uliowekwa na wao.

Vyeti tunavyotunukiwa havina maana ya kweli nje ya ule mfumo uliokutunuku. Vifungashio hivyo vya karatasi hatuvimiliki kimsingi, bali ni mali ya wale waliotuuzia maarifa, waliotupangia mtaala na kutuaminisha kwamba bila mfumo wao hatuwezi kusonga mbele.
Ndiyo maana, mtu mwenye degree katika chuo kikuu fulani hawezi kusimama na kujitegemea kwa maarifa hayo nje ya mfumo wa kisheria, vyeti na ajira uliojengwa na wale waliomfunza.

Mwanafunzi wa tiba anapewa mafunzo makali kwa miaka mingi, lakini vyeti vyote, uhalali wa taaluma yake, na heshima anayopewa hutegemea mamlaka za vyuo vikuu na baraza la kitaaluma. Nje ya mfumo huo, bila barua rasmi au leseni, maarifa yake hayana thamani.
Hata mgonjwa akifa mbele yake, hana uhalali wa kutumia elimu yake bila vibali vya mfumo. Huu ni utapeli. Ni kuta za chuma zilizojengwa ili kutufanya tuamini kwamba elimu ni mali yao, na sisi ni wapangaji wa muda tu katika nyumba yao.

Vyeti hivyo havina uhalali nje ya mfumo kwa sababu havikutokana na asili ya mtu. Hakuna anayemiliki elimu yake kikamilifu, inabaki kuwa rehani mikononi mwa wale waliopanga muundo wa maarifa. Ndio maana mtu mwenye ujuzi anaweza kuonekana hana maana bila cheti. Hii ndiyo picha ya wazi kwamba vyeti hivyo si vya kwetu. Ni vifungashio vilivyowekwa kwenye rafu zao, na sisi tumebaki kuwa watunza rafu hizo.

Kwa mtazamo mpana zaidi, mfumo wa elimu wa sasa ni chombo cha kuzalisha nguvu kazi inayotii. Ni kiwanda cha kuzalisha maroboti ambayo yanapewa elimu ili yaje kutumia vifaa vya ya hao hao waliowatengeneza.
Kwamba mnakuwa wateja wa milele.
Unalazimishwa kuamka mapema, kuingia darasani, kuhangaikia walivyopanga, kusoma vitabu walivyovichagua, na hatimaye kupewa karatasi wanayoiita degree.
Huo ndio mnyororo wa utumwa wa kiakili. Wanaoku-delude kwamba umepata mwanga wa elimu lakini wanakupumbaza. Ukweli ni kwamba umepokea programming na kubandikwa kwenye mfumo wa mawazo na sasa unafanya kazi kama sehemu za mashine zao unazotumia.

Lakini si kwamba elimu haina maana? . Tatizo si maarifa yenyewe, bali ni uhalali unaotolewa na mfumo. Maarifa ni nguvu, lakini yanapowekwa ndani ya sanduku la vyeti, yanageuzwa kuwa bidhaa. Ni bidhaa ambayo haina maana nje ya soko lao. Na sisi, badala ya kuwa wabunifu na waasi wa kifikra, tumekuwa watumishi wa mfumo huo.

Kwa hiyo, tunapaswa kujiuliza ni nani anayemiliki elimu yako. Ni wewe, au ni mfumo uliokupangia maudhui na kukupa cheti? Ikiwa nje ya mfumo huo huwezi kutenda kwa uhuru kwa kutumia maarifa yako, basi hujamiliki kitu chochote.
Wewe ni roboti lao. Na vyeti vyao vya degree, vyenye mihuri na nembo, ni vifungashio tu na si mali yako, bali ni mali ya waliokuletea hiyo Subterfuge.

Kwaherini Maroboti Wenzangu.
 
Back
Top Bottom