Siri ya mafanikio ya wakatoliki hawajioni bora, hawaoni makanisa mengine kama watu wa nje, hawaingilii maisha ya ndoa, wamewekeza kwenye elimu, n.k.

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
2,500
Reaction score
7,524
Wana baadhi ya mapungufu yao sio wakamilifu sehemu zote lakini wamejitahidi kwenye hivi vitu

Hawana mtu wa ndani wala wa nje, ukienda kwao huna haja ya kutambulishwa umejiunga, kwamba fulani hebu simama watu wote kanisani wakuone umejiunga.

Hawajioni bora kuzidi wengine, makanisa mengine hutumia muda mwingi kujiona kama wao ndio wapo kwenye kanisa wataloenda mbinguni au wao ndio bora zaidi, ni kawaida kukuta dini nyingine wakibishana hadi mishipa kuwatoka shingoni kwamba wao ndio kanisa bora lakini mkatoliki huwa muda hana

Kanisa la Roma wamewekeza sana kwenye Elimu na ndio maana jamii zilizoendelea zina historia kubwa ya mchango wa kanisa la Roma kuwapa elimu kwenye shule za wamishenari, Elimu hio imejaza wahasibu, Madaktari, Wahandisi, Wanasheria, n.k. kwenye taasisi nyingi sana za serikali na makampuni. shule kama Saint Francis ni kawaida kuongoza kila mwaka na wanafunzi wachache wanabahatika kupata ufadhili kusoma nje ya nchi

hakuna ubaguzi wa ndoa, kuna baadhi ya makanisa wanataka kuoana wao kwa wao, hili limesababisha baadhi ya mabinti kuzalia kwao kwa kukataa kuolewa nje na baadhi ya waumini wa kiume kuzalisha nje ya imani bila kuoa.

Hawaingilii maisha ya ndoa, Hili limekuwa tatizo kubwa kwenye makanisa mengi sikuhizi, wachungaji wamekuwa viongozi wa wake za watu badala ya waume zao, kugeuza majukwaa ya mahubiri yawe majukwaa ya ushauri wa ndoa za watu bila kujali sumu wanayojaza kwa waumini inayochangia ndoa nyingi kuwa na migogoro na hata kuvunjika
 
Elimu gani mkuu?
Elimu kuanzia shule hadi vyuo, Shule ambayo inaongoza kitaifa kwa miaka mingi ni Saint Francis ya wakatoliki, wanafunzi wa hapo wenye ufaulu mzuri hupata nafasi ya kufadhiliwa kusoma Marekani na nchi za ulaya

Nje ya hapo kanisa limesaidia kuweka vyuo mfano jiji la Mwanza hadi leo hakuna chuo kikuu (University) cha serikali ila kipo cha kanisa katoliki SAUT na Bugando, Mbeya kuna Cuom, Moshi kuna Mwekau, Iringa kuna Ruaha, Tabora kipo na wanaendeleo kujenga vingi zaidi.
 
Hawana mtu wa ndani wala wa nje, ukienda kwao huna haja ya kutambulishwa umejiunga, kwamba fulani hebu simama watu wote kanisani wakuone umejiunga.

Hawajioni vora kuzidi wengine, makanisa mengine hutumia muda mwingi kujiona kama wao ndio wapo kwenye kanisa wataloenda mbinguni au wao ndio bora zaidi, ni kawaida kukuta dini nyingine wakibishana hadi mishipa kuwatoka shingoni kwamba wao ndio kanisa bora lakini mkatoliki huwa muda hana

hawajitengi kwenye mambo ya ndoa, kuna baadhi ya makanisa wanataka kuoana wao kwa wao, hili limesababisha baadhi ya mabinti kuzalia kwao kwa kukataa kuolewa nje na baadhi ya waumini wa kiume kuzalisha nje ya imani bila kuoa.

Kanisa la Roma wamewekeza sana kwenye Elimu na ndio maana jamii zilizoendelea zina historia kubwa ya mchango wa kanisa la Roma kuwapa elimu kwenye shule za wamishenari, Elimu hio imejaza wahasibu, Madaktari, Wahandisi, Wanasheria, n.k. kwenye taasisi nyingi sana za serikali na makampuni.
Kwa utafiti upi hata machawa?
 
Hakuna watu makatili kwenyemisiba kama hao ndugu zangu. 1, amejinyonga hatumuombei. 2, hakubatizwa si mshirika wetu japo alikuwa anakuja kitambo kidogo. 3, hatukuwa tukimuona kwenye jumuiya, parokia wala vigango huyu si mtu wetu. Aiseeee nilishangaa sana baada ya babu yangu kufariki tumemuita katekista aje kuongoza ibada, amekuja badala ya kufanya sala anaanza maneno mara "ohoo japo alibatizwa utotoni lakini hakufunga ndoa takatifu na hakuwa akishiliki ibada alitopea katika maisha ya dhambi, sisi hatumuombei ndio maana tunawasihi muishi maisha mema ili mjekupata pumziko la amani.' Si bora asingekuja tu kuliko kuja na kuanza kumsimanga marehemu.
 
mambo kama hayo huwa yanatokea kwa kwa sababu ya watu binafsi, si kanisa lenyewe.
 
Nalijua hilo huwa wanaharibu na kurekebisha wao kwa wao, hata kwa babu yangu baada ya kateksta kuchafua upepo siku ya mazishi, kufika siku ya kumaliza msiba akaja asikofu kutoka jimboni na kuweka mambo sawa, yule mzee kateksta nahisi aliondoka na aibu debe.
 
Hakuna watu makatili kwenyemisiba kama hao ndugu zangu. 1, amejinyonga hatumuombei. 2, hakubatizwa si mshirika wetu japo alikuwa anakuja kitambo kidogo. 3, hatukuwa tukimuona kwenye jumuiya, parokia wala vigango huyu si mtu wetu. Aiseeee nilishangaa sana baada ya babu yangu kufariki tumemuita katekista aje kuongoza ibada, amekuja badala ya kufanya sala anaanza maneno mara "ohoo japo alibatizwa utotoni lakini hakufunga ndoa takatifu na hakuwa akishiliki ibada alitopea katika maisha ya dhambi, sisi hatumuombei ndio maana tunawasihi muishi maisha mema ili mjekupata pumziko la amani.' Si bora asingekuja tu kuliko kuja na kuanza kumsimanga marehemu.

Yawezekana ni fikra za mtu binafsi, na siyo msimamo wa Kanisa.

Msimamo wa Kanisa:
1. Hairuhusiwi kumhukumu binadamu mwenzako.

2. Ambaye hawezi kuzikwa kwa taratibu za kikanisa ni yule aliyeukana ukatoliki wake.
 
Ni kweli mkuu, ila kesi za kutokuombewa kwa wanao jinyonga tumezisikia sana.
 
Hakuna watu makatili kwenyemisiba kama hao ndugu zangu. 1, amejinyonga hatumuombei. 2, hakubatizwa si mshirika wetu japo alikuwa anakuja kitambo kidogo. 3, hatukuwa tukimuona kwenye jumuiya, parokia wala vigango huyu si mtu wetu. Aiseeee nilishangaa sana baada ya babu yangu kufariki tumemuita katekista aje kuongoza ibada, amekuja badala ya kufanya sala anaanza maneno mara "ohoo japo alibatizwa utotoni lakini hakufunga ndoa takatifu na hakuwa akishiliki ibada alitopea katika maisha ya dhambi, sisi hatumuombei ndio maana tunawasihi muishi maisha mema ili mjekupata pumziko la amani.' Si bora asingekuja tu kuliko kuja na kuanza kumsimanga marehemu.
Huyo babu yako hakua na pesa au cheo chochote maybe

Mimi babu yangu alikua anasali ila ana wake wawili na wote wanatambulika, siku amefariki walikuja mapadri watatu kuongoza misa

NB
Babu alikua mtoaji mzuri sana kanisani na alikua kiongozi mkubwa serikalini
 
Sasa hapo kilichowaleta ni ushiriki na utoaji wake na si utajiri wake, mimi babu yangu hakuwa akishiriki wala kutoa michango, tangu ujana wake wote hadi uzee mambo mengi aliyaacha utotoni.
 
Hayo huwa ni matatizo ya watu binafsi ndani ya kanisa, bibi yangu alifariki akiwa na miaka 79 na alikuwa na uchumi wa kawaida sana lakini alizikwa na kanisa kwa heshima zote
 
Sasa hapo kilichowaleta ni ushiriki na utoaji wake na si utajiri wake, mimi babu yangu hakuwa akishiriki wala kutoa michango, tangu ujana wake wote hadi uzee mambo mengi aliyaacha utotoni.
But Kanisa katoliki haliruhusu ndoa za mitala hii nayo alikaaje?

Kwa upande wa babu yako kwa kuwa hakua akishiriki kwa lolote walikua sahihi kutofika japo uyo katekista alizingua kumsema marehemu bora angekausha tu
 
Wako Vizuri kwenye baazi ya Aspect, Pamoja na kutojiona wao ndo Wakamilufu kuliko Dini nyingine.

Wakute Wasabato, Walokole na Mashahidi Utaona kabisa wewe ndo unaenda motoni.
 
Kabisa.
 
na kupenda kuoana wao kwa wao, wana ile aili ya kujiona "sisi ndio tuliochaguliwa" ("we are the chosen ones")
 
Wana baadhi ya mapungufu yao sio wakamilifu sehemu zote lakini wamejitahidi kwenye hivi vitu

Hawana mtu wa ndani wala wa nje, ukienda kwao huna haja ya kutambulishwa umejiunga, kwamba fulani hebu simama watu wote kanisani wakuone umejiunga.

Hawajioni bora kuzidi wengine, makanisa mengine hutumia muda mwingi kujiona kama wao ndio wapo kwenye kanisa wataloenda mbinguni au wao ndio bora zaidi, ni kawaida kukuta dini nyingine wakibishana hadi mishipa kuwatoka shingoni kwamba wao ndio kanisa bora lakini mkatoliki huwa muda hana

Kanisa la Roma wamewekeza sana kwenye Elimu na ndio maana jamii zilizoendelea zina historia kubwa ya mchango wa kanisa la Roma kuwapa elimu kwenye shule za wamishenari, Elimu hio imejaza wahasibu, Madaktari, Wahandisi, Wanasheria, n.k. kwenye taasisi nyingi sana za serikali na makampuni. shule kama Saint Francis ni kawaida kuongoza kila mwaka na wanafunzi wachache wanabahatika kupata ufadhili kusoma nje ya nchi

hakuna ubaguzi wa ndoa, kuna baadhi ya makanisa wanataka kuoana wao kwa wao, hili limesababisha baadhi ya mabinti kuzalia kwao kwa kukataa kuolewa nje na baadhi ya waumini wa kiume kuzalisha nje ya imani bila kuoa.

Hawaingilii maisha ya ndoa, Hili limekuwa tatizo kubwa kwenye makanisa mengi sikuhizi, wachungaji wamekuwa viongozi wa wake za watu badala ya waume zao, kugeuza majukwaa ya mahubiri yawe majukwaa ya ushauri wa ndoa za watu bila kujali sumu wanayojaza kwa waumini inayochangia ndoa nyingi kuwa na migogoro na hata kuvunjika
Chai
 
Back
Top Bottom