Swali kwa wanawake wajawazito na waliopita kipindi cha ujauzito

Sheillah Sheillah

JF-Expert Member
Jun 17, 2020
583
1,478
Habari.

Huu ni ujauzito wetu wa kwanza. Mimi na mpenzi wangu hatujawahi kupitia kipindi cha ujauzito kabla. Jamani shemeji yenu ana shauku sana. Ameshampenda huyu mtoto hata kabla hajazaliwa. Tayari naona mahaba yake moto moto kwa huyu mtoto wetu. Tunamuomba Mungu aendelee kutulinda na kumlinda huyu mtoto hadi siku atakapoamua aje katika ulimwengu huu.

Tangu wiki ya 14 ya ujauzito mimi kama mama nimekuwa nikisikia harakati( flutters) za mtoto tumboni. Na sasa hekaheka(kicks) zake kwa sasa zimekuwa na nguvu nazisikia kabisa.

Huyu shemeji yenu ananionea wivu anahisi nafaidi pekee yangu anatamani na yeye aanze kuzisikia. Ila mpaka sasa hazijawa na nguvu ya kuonekana kwa nje ya tumbo. Nazihisi kwa ndani ila nikiliangalia tumbo sioni likitikisika.

Swali langu ni hili, ni wiki ya ngapi katika ujauzito mwenza wako aliweza kuhisi au kuona kucheza kwa mtoto tumboni? Nimeuliza kwa watu wanaopitia kipindi hiki au waliokwisha kupitia kwa sababu nataka kusikia kutoka katika uzoefu halisi.

Asante.
 
Back
Top Bottom