Hodi JamiiForums

Mar 28, 2024
25
63
Bila kupoteza wasaaa, Mimi Heyyouyoungman ni mgeni hapa jamii forum, japo nakili kuifahan JamiiForums toka mwaka 2010 nikiwa kidato cha pili katika shule moja wapo huko Rukwa.

Nimekuwa nikisoma thread mbalimbali za humu jamii forum na kuvutiwa na watu kadha hasa mwanadada To yeye , na Mwandishi wa story Analyse na wengine wengi kama si wote maana kumekuwa na mijadala motomoto hum ndani.

Kwa sasa Jamiiiforums ndio jukwaa pekee la kijamii nililonalo kwenye simu yangu na ndio chanzo changu kikuu cha habari kwan sina Mtandao wowote wa kijamii katika simu yangu tofauti na Jamii forum.

Pia mim ni Jobless wa miaka mingi sasa, maana tangu nimehitim shahada yangu ya kwanza ya Lojistik na usafirishaji toka NIT mwaka 2018 sijabahatika kupata ajira ya kudumu tofaut na ya mkataba ambayo nimefanya kwa zaidi ya miaka mitatu katika taasisi ya Serikali.

Pamoja na kuwa na shahada hiyo ya kwanza ya Lojistik na usafirishaji pia nina COP Ya Insurance niliyopata toka chuo cha Usimamizi wa Fedha ( IFM) Hivyo ninaweza fanya kazi mbalimbali hata kwenye ofisi za Bima. Hivyo basi niombe kwa yeyote anayetaka mtu wa aina yangu katika ofisi yake asisite kunitafuta, Nipo na ntamfanyia kazi vizuri, kwa weledi na uaminifu mkubwa. Natanguliza shukrani
 
Back
Top Bottom