Simon Msuva basi hata kama uliamua Kumpigia pande huyo Shemeji yako Mzungu Taifa Stars, mbona ana Kiwango kibovu hivyo?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,572
108,927
Halafu hapo hapo tena tukaambiwa kuwa huyo Shemeji yako ( Mchezaji Mweupe kutokea Uingereza ) anacheza Ligi Daraja la Tatu wakati kumbe anacheza Ligi Daraja la Tano Uingereza ambalo kwa huku Kwetu Tanzania ni sawa tu na Ndondo Cup ile ya Shaffih Dauda.

Kwahiyo Simon Msuva ( Shemeji Mtu ) na TFF mlidhani kabisa kuwa mtawafichq Watanzania wote ( hasa Waandishi wa Habari za Michezo ) Tanzania na mpaka Mimi GENTAMYCINE bingwa wa kupata Taarifa za Ndani na za Hatari nisingezijua kabisa?

Haya sasa kama kawaida najua wale ambao Exclusives zenu zote huwa mnazipata Kwangu Mimi GENTAMYCINE hapa JamiiForums na hii mtaichukua na kuitumia huku mkijifanya ni yenu au mmeitafuta nyie wakati kumbe mmeipata kutoka Kwangu The King.

Tafadhali mkiitumia huko katika Kurasa zenu au Mitandao yenu au kokote kule msione Aibu au Wivu kusema tu kuwa Taarifa hii ya Simon Msuva kumpigia pande Shemeji yake Mzungu ( Taifa Stars ) mmeitoa Kwangu GENTAMYCINE sawa?

Na nina Exclusives zingine kama Tatu hivi kabambe kweli kweli na hakuna cha Mwandishi wa Habari za Michezo au Mchambuzi wa Michezo Tanzania anazo isipokuwa ni Mimi tu GENTAMYCINE.

HATERS mliokuwa hamtaki nifunguliwe Jukwaa langu hili la UFALME la Michezo hapa JamiiForums mpo? Mnajisikiaje baada ya Mwamba na Mfalme Kurejea rasmi kwa Hekima na Busara za Moderators Wapendwa wa JamiiForums na JamiiForums Founder Maxence Melo?

Ni matumaini yangu kwamba HATERS Wote hamtokuwa mnasoma Exclusives zangu na Analysis zangu mbalimbali za Michezo hapa JamiiForums bali mtawapisha / mtawaacha tu wale ambao Wananikubali, Wananiamini na Wananiheshimu ndiyo wawe Wananisoma na Kuburudika nami "Purely Talented, Charismatic Fella, Game Changer and Entertainer" GENTAMYCINE sawa?

HATERS wangu wote nawaacheni na hii Zawadi yangu Kubwa Kwenu ya Yeremia ( Jeremiah ) 1:19.
 
Harakati za mtu mfupi kibonge
1704621171281.jpg
 
Exclusive hapo ni ushemeji wa msuva ama hiyo timu ya daraja la tano england?

Inamaana Taifa stars walitanganza jina la mchezaji ambaye hajulikani anacheza timu gani aje kushiriki Afcon? Hivi watu wote walikuwa hajui kuwa wealdstone fc inashiriki national league pale UK?
 
Amrouche mnamsingizia tu katika hili. Nimemsikia hadi Jemedari anamlaumu katika hili wakati ukweli wanaujua. Ubaya wa nafasi ya kocha, hauwezi kutoka kujibu tuhuma ndiyo maana wale wazoefu kina Amrouche, Benchikha na huyu wa Yanga huwa hawaogopi kusema shida ilipo.

Tunalilia kupata wachezaji wenye misingi mizuri ya mpira halafu leo tunawadharau tunaowapata kisa wanacheza madaraja ya chini huko nje. Kuna wachezaji hawakupewa nafasi ila walikuwa na uwezo wa kutupa matokeo.

Pia kuhusu issue ya Mzize nashangaa watu bado wanamlaumu kwa kutomchagua wakati aliitwa na hakwenda halafu cha kushangaza TFF hawakumchukulia hatua mmebaki kumlaumu tu kocha.
 
Unaweza kunionyesha ni wapi katika Thread Content yangu nimemtaja Kocha wa Taifa Stars Adel Amrouche?

Nachukia mno Mijitu Mijuha na inayopenda Kukurupuka kutokana na Kuwashwawashwa Kwao.
 
Uandishi wako ni wa kitoto sana

Mimi sio mwandishi wa habari lkn taarfa yako imejaa mapungufu mengi mno,kwa nchi zilistaarabika ungeweza kumlipa mtu mamilion ya pesa kwa kumtuhumu

Huna uhakika wowote wa jambo unalolisema zaidi ya kuokoteza mtaani

Hujamuhoji wala kumpa nafasi unayemtuhumu kujitetea

Km hii habari imeandikwa na kijana wa sekondari sawa lkn km imeandikwa na mtu mzima ni upumbavu wa hali ya juu
 
Umemaliza au bado?
 
Kwa Sasa Wanamsimbazi Wana-confidence Sana Ila Ligi Kuu Ikianza Na Vipigo Vyenu Vikaendelea Thread Zote Zitakuwa Za Kuilalamikia Timu Yenu.
 
Amrouche mnamsingizia tu katika hili. Nimemsikia hadi Jemedari anamlaumu katika hili wakati ukweli wanaujua. Ubaya wa nafasi ya kocha, hauwezi kutoka kujibu tuhuma ndiyo maana wale wazoefu kina Amrouche, Benchikha na huyu wa Yanga huwa hawaogopi kusema shida ilipo.

Tunalilia kupata wachezaji wenye misingi mizuri ya mpira halafu leo tunawadharau tunaowapata kisa wanacheza madaraja ya chini huko nje. Kuna wachezaji hawakupewa nafasi ila walikuwa na uwezo wa kutupa matokeo.

Pia kuhusu issue ya Mzize nashangaa watu bado wanamlaumu kwa kutomchagua wakati aliitwa na hakwenda halafu cha kushangaza TFF hawakumchukulia hatua mmebaki kumlaumu tu kocha.
Ligi daraja la 5 ni chini sana, mchezaji huyo hana Kariba ya kucheza Afcon.
 
Ligi daraja la 5 ni chini sana, mchezaji huyo hana Kariba ya kucheza Afcon.
Msichoelewa hao mnaowasema hawafai, wangecheza vizuri wakaonekana baada ya mashindano wangepata timu za daraja la 3 au hata la 2. Ile tunatakiwa kuitumia kama platform ya kukuza thamani ya wachezaji. Tunataka wachezaji ambao tayari wana thamani ya juu ila hatuoni nafasi yetu kukuza hizo thamani. Hivi hamuoni jinsi AFCON ilivyomsaidia Msuva kupata timu wakati ameenda huko hana ajira? Wewe unadhani yule Haji Mnogwa thamani yale sokoni iko kama ilivyokuwa kabla ya kucheza na timu kama Morocco mara mbili ndani ya miezi miwili na kucheza AFCON?

Yale yale ya ujinga waliofanya Simba kwenye AFL, tunawapa platform wazee ambao nafasi ya kuuuzika nje ni finyu, mashindano yanakwisha mnarudi kuangaliana, wote mko pale pale. Wakati mwingine mahaba binafsi kwa wachezaji yanatupa upofu sana tunafanya maamuzi ya kijinga.

Dunia hii ya mpira wa kulipwa inahitaji upate vitu viwli, platform ya kuonekana na wakala mjanja basiiii. Wakati mwingine hata uwezo unaweza kuwa wa kawaida lakini bado ukatoboa kama una hivyo vitu viwili.
 
Back
Top Bottom