ingawa hakuna ninayemfahamu hapa mmu kwa sura lakini ki ukweli nimeelimika sana kupitia michango yenu. long live mmu na mungu awe nasi ili tuweze kuuona mwaka mpya wa 2014.
Kuna wakati sura na matendo yetu yanaishi katika yale tuyaandikayo.
Panapo fursa watafute watu wawili watatu, onana nao. Naamini kuna jipya utapata zaidi marafiki wapya utawakaribisha maishani mwako.
Nikisema sikupata kitu toka jf nitakuwa sijatenda haki . Nilikua naingia humu kuperuzi mwaka jana na mwisho nilipoona siwezi kuchangia ndipo nilipoamua kujoin.
Nawashukuru sana members wote nimejifunza mengi toka kwenu. Ni vigumu kumtaja kila mmoja lkn wote nawashukuru nimepata mengi toka kwenu. Nimejifunza uvumilivu na kuchukuliana hasa mawazo yanapotofautiana. Kwa kifupi mmenifundisha mengi Mungu awabariki wote.
Nawatakia wote happy holidays nikianza na xmas na mwisho mwaka mpya naamini kwa uwezo wake Muumba tutafika salama kwenye new year. Shukrani zikufikie wewe uliyeanzisha uzi huu napata uzito kukuita babu naomba uniruhusu nikuite mkubwa mwenzangu.
DEMBA muke ya kaka mkubwa Kaizer hivi unaweza amini mfano wa comment yangu hapo juu kuna watu sijawahi onana nao ila the way tunavyointeract mpaka nasema jf ni kwingine kikubwa aina ya watu wa kusocialize nao [si unajua tena umakini muhimu kwenye msafara wa mamba na kenge wapo]yaani mpaka nashangaa madili mengine ya pesa ndefuuuu tunafanya na hatujaonana mawasiliano tu.
Afu nimesoma comment yangu kwa mara ya 2 nikajiona how lucky i am.
Jf imekua sehemu kubwa ya maisha yangu kutokana na michango ya watu humu ndani..
..natamani kukutana na watu na kupata michango yao zaidi ila sijui nianze vipi,nisaidie kwa hili watu8
Asante Mungu asante wana jf kwa kufika hapa. Mwaka ulikuwa mzuri kiasi nimeweza kununua ekari kadhaa mikoa tofauti kazi iliyopo ni kuziendeleza. ...................................... Changamoto ni nyingi hasa kwenye mapenzi. ............................................ Nimeumiss uzi wa NYUMBA NDOGO kila nikiuita siupati.
yaani jf is something else kwa kweli. ikitokea nimeshindwa kuingia jf kwa namna yeyote huwa najihisi kama naumwa.DEMBA muke ya kaka mkubwa Kaizer hivi unaweza amini mfano wa comment yangu hapo juu kuna watu sijawahi onana nao ila the way tunavyointeract mpaka nasema jf ni kwingine kikubwa aina ya watu wa kusocialize nao [si unajua tena umakini muhimu kwenye msafara wa mamba na kenge wapo]yaani mpaka nashangaa madili mengine ya pesa ndefuuuu tunafanya na hatujaonana mawasiliano tu.
Afu nimesoma comment yangu kwa mara ya 2 nikajiona how lucky i am.
ahsante babu!! huko sio nasikiaga eti waja leo warudi leo. hivi huwa mnamaanisha nini kwenye huu msemo?
..natamani kukutana na watu na kupata michango yao zaidi ila sijui nianze vipi,nisaidie kwa hili watu8
Kwanza kabla ya yote napenda sote kwa pamoja hapa MMU tuutunuku uzi huu kuwa uzi bora wa kufungia mwaka kwa pamoja. Ni imani yangu kuwa kili mmoja wetu humu ataelezea namna ambavyo MMU imekuwa nzuri kwa upande wake.
Kwa upande wangu mie. Kiukweli sijawahi kujuta kuwepo humu na kufahamiana na yeyote humu. Nimepata marafiki wengi. Na wengine wamekuwa zaidi ya ndugu kwangu.
Kwa upande wa MMU kwa kweli nimepata mengi sana ya kujifunza. Zamani kidogo ilikuwa ngumu sana kuamini kama itawezekana kuishi na kuelewana na mtu ambaye hamjawahi kuonana hata kwa sura. Naweza kusema kuwa nimefahamiana na wengi humu na tumekuwa tukisaidiana, tukishauriana kwenye mambo mengi. Sasa kupitia MMU nimeamini kuwa jamii hii ya humu mtandaoni haina tofauti na hizi ambazo tuko nazo mitaani tuishipo.
Shukrani ziwafikie Mtambuzi, gfsonwin, snowhite, Dark City, Mentor, Heaven on Earth, KOKUTONA amu, Mwanyasi, YNNAH, Smile, Jiwe Linaloishi, AshaDii, Maxence Melo, watu8, Cantalisia, sweetlady, Preta, Mamndenyi, Madame B, Kijino, cacico, Asprin, @FP, Fixed Point, charminglady, Elizabeth Dominic, Kaunga, Zion Daughter, Arushaone, marejesho, Baba V, MMAHE, Asnam, christine ibrahim, Filipo, Remmy, Nivea, Ruhazwe JR, @c6, Kichwa mbovu, Kaizer, Husninyo ladyfurahia, BAK, nameless girl, @lara1 Arabela, Judgement, BAGAH, Erickb52, Crashwise, Mungi nitonye Kipaji Halisi, Lady doctor, Passion Lady, Ruttashobolwa, Sanctus Mtsimbe Bishanga, The secretary Rejao, n.k. Kwa kweli kutoka moyoni mwangu wanaotakiwa kushukuriwa ni wengi sana. Hao niliowataja ni wachache sana. Ambao sijawataja msidhani nimewasahu. Nikisemaniwataje wote humu basi hii post itakuwa ndefu sana.nawashukuru wote kwa pamoja.
Mungu ibariki Afrika, Mungu Ibariki Tanzania, Mungu ibariki JF, Mungu awabariki viongozi wa JF na members wote.
Asante kwa kushukuru...