benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,034
Wanafunzi 88 waliojiunga na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) mkoani Arusha, wameshindwa kumaliza mafunzo kwa sababu mbalimbali ambapo kati yao, 14 wadaiwa kuyakimbia ambapo mhitimu hutunukiwa “Shahada ya Kijeshi.”
Hayo yamebainishwa katika mahafali ya leo Jumamosi Novemba 18, 2023 ambapo maofisa wanafunzi 575, wametunukiwa Kamisheni na Amiri Jeshi Mkuu, Rais Samia Suluhu Hassan na hivyo kuvishwa vyeo vya Luteni Usu.
Akitoa taarifa ya mafunzo hayo, Mkuu wa chuo hicho, Brigedia Jenerali Jackson Mwaseba amesema kulikuwa na makundi mawili wa wanafunzi ambapo katika kundi la 04/20 la maofisa wa wanafunzi wa shahada ya Sayansi ya Kijeshi, waliojiunga na chuo walikuwa 73 huku 62 ndiyo walifanikiwa kuhitimu.
Chanzo Mwananchi