Rwanda yapokea wanafunzi wa udaktari kutoka Sudan

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,042
49,727

Screenshot 2023-08-04 112752.png
Kundi la wanafunzi wa udaktari kutoka Sudan wamekaribishwa nchini Rwanda kuendelea na masomo baada ya vita ya wenyewe kwa wenyewe kuibuka katikati ya mwezi Aprili, mwaka huu.

Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba na Teknolojia cha Sudan kilizidiwa na kugeuzwa kambi ya wapiganaji katika mji mkuu, Khartoum, ambapo vikosi vya kijeshi na jeshi vinahusika katika vita ya kuwania madaraka.

Wanafunzi 160 wa shahada ya kwanza, ambao walikuwa wamebakisha miezi minane kumaliza kozi yao, wamepewa nafasi pamoja na wahadhiri wao katika Chuo Kikuu cha Rwanda.

Kikundi hicho ambacho kinaundwa na wanawake, pia kitakuwa kikifanya mazoezi katika hospitali za mitaa.

Mmoja wa wanafunzi, Dina Abdalrahim Obaid, wakati akizungumza katika hafla ya kuwakaribisha, aliishukuru Rwanda kwa kuwapatia hifadhi na fursa ya kuendelea na masomo yao.

Profesa Mamoun Mohamed Ali Homeida, ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sudan, alisisitiza jinsi walivyo na bahati, kwani wanafunzi wengine wengi walikimbilia nchi tofauti bila nafasi ya kuendelea na masomo.

“Tuliomba kuja Rwanda kwa sababu tunatarajia kwamba vita vitakapomalizika, nchi yetu itahitaji madaktari,” alieleza.

Wakiwa nchini Rwanda, wanafunzi hao wataendelea na mtaala wao wa Sudan lakini watafanya mafunzo katika hospitali za ndani, alithibitisha Didas Muganga Kayihura, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Rwanda.

Mwaka 2021 shule ya bweni ya kibinafsi ya wasichana ilihamisha wanafunzi na wafanyakazi wake hadi Rwanda baada ya Taliban kuchukua madaraka nchini Afghanistan kupiga marufuku elimu ya juu kwa wasichana na wanawake.

Habari Leo

Pia soma:
Wanafunzi wa vyuo vikuu vya Sudan wahamishiwa vyuo vikuu vya Tanzania. Hongera kwa Serikali ya Tanzania
 
Back
Top Bottom