Rais Samia awatunuku Kamisheni wanafunzi wa JWTZ Monduli, leo Novemba 26, 2022

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,979
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi Kundi la 03/19 - Shahada ya Sayansi ya Kijeshi na Kundi la 69/21 Refu Pamoja na Mahafali ya tatu ya Shahada ya Sayansi ya Kijeshi Kundi la 03/19 katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) - Monduli Arusha leo tarehe 26 Novemba, 2022

5F139B90-9050-4F85-B133-078CB78199E7.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan, amewatunuku Kamisheni Maafisa Wanafunzi 724 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kundi la 03/19 wa Shahada ya Sayansi ya Kijeshi na kundi la 69 /21 Refu.

Akitoa maelezo katika sherehe zilizofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Jeshi (TMA) Monduli, Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli (TMA) Brig. Jen. Jackson Mwaseba amesema kati a wanafunzi waliohitimu wanawake ni 89 na wanaume 635.

Kwa upande mwingine, Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Dkt. Cairo Mwaitete amesema JWTZ imekuwa ikishirikiana na Chuo hicho kutoa Shahada a Sayansi ya Kijeshi ambapo kwa kipindi cha miaka 3 va ushirikiano jumla va wanafunzi 313 wamehitimu.

Aidha, Dkt. Mwaitete amesema Shahada hivo inawaandaa maafisa waliohitimu kuweza kuwa mahiri katika kusimamia masuala ya kijeshi, amani pamoja na uongozi kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Dkt. Mwaitete pia amesema Chuo cha Uhasibu kina mpango wa kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa Shahada mbalimbali zikiwemo usalama wa mitandao, usalama na masomo ya kimkakati, masomo ya ulinzi na amani pamoja na ulinzi wa taarifa.

Hali kadhalika, Dkt. Mwaitete amesema Chuo cha Uhasibu kinaunga mkono mpango wa Serikali kupeleka Vuo vya Elimu ya Juu katika mikoa ya pembezoni kupitia fedha za Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET).

Pamoia na kutunuku Kamisheni, Mhe. Rais Samia ametoa zawadi kwa Maafisa wanafunzi waliofanva vizuri katika mafunzo hayo.
 
Tanzania ni salama na Samia na kazi inaendelea
 
Back
Top Bottom