Wanaharakati: Ziachieni simu za VodaCom!


Mushi,
Yaani hii nchi yetu ni ajabu sana. Yaani mhalifu ndo yuko salama na raia mwema ndo amegeuzwa kuwa mhalifu wa kuwindwa kisa anaingilia ulaji wa mafisadi. Ooooooh, MUNGU atusaidie.
 

I am not sure about his reffred price but your price you reffering to is excluding VAT and other excise duty which could justify his pricing urgument.

The way foward we just need to restrict all unethical people to own a pie in Telecommunication companies due to security resorns
 

kaka nadhani umeshajifanya mjinga...kwenye link yako kuna hayo maneno yanasema;
All rates quoted are in TSH exclusive of taxes, applicable 24 hours a day or as per indicated Time Bands.
 

This is a public forum kwa maana uki bandika kitu hapa ume kubali ijadiliwe na kila mtu. Kama ujumbe alikua na nia ya kuwapa watu fulani tu kwa nini ameiweka kwenye public forum? If it was meant to be a message to a few people basi ange watume ujumbe binafsi. Nakubaliana na wewe kuwa wengine hatuja muelewa kwa maana haja toa sababu, sisi wengine hatupo kwenye hiyo "inner circle" ya wenzetu mlio elewa bila ufafanuzi ndiyo maana tunauliza. Ila uzuri ni kwamba Mwanakijiji mwenyewe yupo na anaweza kuji tetea bila third party, maswali yapo directed kwa Mwanakijiji ambae sidhani kama kaku chagua wewe kama msemaji wake. Ngoja Mwanakijiji mwenyewe atueleze vizuri. Sisi wengine siyo tuna fuata tu mkumbo na kumfuata mtu kama vile yeye ni Yesu, sija kataa alicho kisema wala sija kikubali, cha msingi ni maswali yameulizwa na ni maneno yake mwenyewe Mwanakijiji yatakayo conince doubters wote. Mtu hawezi kusema tu fanya hichi au fanye vile na watu wafuate tu bila kuuliza maswali if you are one of them basi nyie ndiyo wale wale ambaoo hawaangalii hoja bali wana fuata mkumbo. Wewe umeelewa kama madai yako yanavyo sema basi ngoja na sisi ambao hatuja elewa tuulize tufahamishwe.
 
kaka nadhani umeshajifanya mjinga...kwenye link yako kuna hayo maneno yanasema;
All rates quoted are in TSH exclusive of taxes, applicable 24 hours a day or as per indicated Time Bands.

Nafikiri wewe ndo mjinga kwa kutofanya mahesabu. Fanya mahesabu uweke na VAT uone kama kilichosemwa hapo juu ni sahihi.
 
Nafikiri wewe ndo mjinga kwa kutofanya mahesabu. Fanya mahesabu uweke na VAT uone kama kilichosemwa hapo juu ni sahihi.

ukitaka kuwa mwelevu lazima upitie kwenye ujinga,kubali ujinga wako kwa kile ulichopost ili ueleweshwe sio kukimbilia kuweka link wakati kilichoandikwa not reachabe
 

Mkuu Leokweli,
Kwenye rates za simu inaongezeka VAT tu. Kwahiyo ukiweka na VAT utakuta kuwa kilichosemwa kwenye hiyo post ya jamaa ni uongo. Kama huyu fisadi RA ameamua kutumia Vodacom kwa kuwashirikisha vibaraka wake (IGP, DCI etc) kunasa maongezi ya watu wanaopambana na ufisadi nchini, basi hii iwe ni sababu kubwa na ya msingi sasa kuuhama huu mtandao. Kama iko hivyo iwekwe wazi watu tuelewe issue isiwe gharama maana hiyo itakuwa ni kibiashara zaidi na hapo mtu ana uhuru kuchagua anachopenda.
 
Nafikiri wewe ndo mjinga kwa kutofanya mahesabu. Fanya mahesabu uweke na VAT uone kama kilichosemwa hapo juu ni sahihi.

You know mkuu kuna msemo wa kingereza unaosema "Give the devil his due". Kwa maana kwamba hata kama kitu kina ubaya uzuri wake uangaliwe na pande zote za shilingi ziangaliwe. Hapa kisa RA is involved hata useme nini dhidi ya thread wata sema oh una tetea ufisadi au oh uko kwenye payroll ya mafisadi. Kuna makampuni mengi sana yana element ya ufisadi, kwa sababu Mwanakijiji kasingle out Vodacom lazima tumuulize sababu za kusema hivyo. Muanzisha thread mwenyewe bado hajajibu chochote I'm sure ana soma upepo unapoenda kwanza ili ajipange vizuri kujibu. Mimi sitetei ufisadi lakini kutokana na alicho kiandika aliye anzisha thread bado sijaona ni sababu gani zimem pelekea yeye kusema kuwa watu wana takiwa kuisusia Vodacom. Mimi naona tatizo ni mmiliki au wamiliki wa Vodacom na ufisadi wao lakini siyo Vodacom na huduma zake. Kama Vodacom inatoa huduma ninayo hitaji kwa nini nisiitumie? Kama Mwanakijiji ana sababu nzuri ya kwa nini nisiitumie basi abainishe. Ila nisha gundua kuna watu humu ndani wanaendeleza ushabiki tu na ukisema chochote kinacho pingana na wengi basi watadai una side na upande wa ufisadi. Lets not use "ufisadi" as a scapegoat kama una hoja toa ila mtu kama mimi siwezi kuacha kusema ukweli kisa tu kitu fulani ume kitaja basi kuna fisadi involved. Kama nilivyo sema mwanzo ni kwamba sija kataa Mwanakijiji alicho sema lakini bado hajatoa sababu ya kwa nini tuisusie Vodacom. Ngoja mkuu Mwanakijiji asome upepo nina uhakika atakuja kujibu maswali na hao walio jipa uspokesmen kwa niaba yako wata nyamaza tusikie everything from the horses mouth.
 

Na ndiyo tunacho taka hicho. Kama ulivyo sema kama ni wana tumia mtandao wao kuingilia privacy za watu basi hiyo ni hoja nzito lakini kuhusu gharama ni maamuzi ya mtu. Sema hata huyo mwanakijiji mwenyewe hajasema kama sababu yake ya kusema tususie Vodacom ina husiana na privacy issues au la. Aliye anzisha mjadala yupo ngoja tumsikie na wengine waache kujidai ni wasemaji wake. Tunacho taka ni sound reasons tu lakini hilo la rate siyo sababu.
 

Yes mkuu,
Mwanakijiji nafikiri pengine ana sababu nzito ambayo alitaka kuiweka hapa ila hajaiweka hadharani. Tunaomba atuwekee, maana watu wengine hapa wameigeuza mada kuwa ya kibiashara zaidi na hilo ni uamuzi wa mtu binafsi. Hapa TZ ndugu yangu kila mahali tumezungukwa na biashara za mafisadi tu na ukitaka kususia kila kitu yakubidi uondoke katika hii dunia. Ila pale panapokuwepo na sababu ya msingi basi twaweza kabisa kususia huduma fulani, hilo sikatai hata kidogo.
 

In tanzania we charge 10% as excise dute because kupiga simu ni starehe. Ninazani sababu ya msingi ni kumwuliza tu aliyeanzisha mada afafanunue zaidi ili mada yake isionekane kama ina motive za ushindani wa kibiashara.

But i dont think aliyeanzisha mada analenga ushindani wa kibiashara because Makampuni mengi yanapenda kukata cost kwahiyo swala la bei lingekuwa tatizo wangekuwa wamehama siku nyingi I gues they are happy with the products and for that we will let the free market to work.

Kwasasa serikali inatakiwa itoe order kwamba wale wote wanaotuhumiwa na ufisadi wasiluhusiwe kufanya any transfer of Capital nor share until their name are cleared

On other way kama Vodacom iki lose 50% ya market share yake itakuwa lahisi kwa majority shareholder kumshinikiza RA atoke kwenye Biashara so I think this might be mwanakijiji urgument to boycott Vodacom but I think Usilo lijua ni kama usiku wa Giza so mwankijiji atufafanulie
 

Nilichomwelewa Mwanakijiji hapa kama nitakosea anikosoe ni kwamba, anawaonya wanaharakati walio katika mapambano dhidi ya ufisadi juu ya kutumia mtandao wa Vodacom huenda kuna namna imetengenezwa kuwanasa na kuna mkuu mmoja hapa amedokeza kuwa kuna mitambo ya kunasa maongezi ya watu huko kwa DCP, IGP n.k. Sasa hapa sijaelewa kama hivyo vinasa maongezi ni kwa ajili ya mtandao wa Vodacom tu au ni mitandao yote. Mwanakijiji tafadhali tunaomba maelezo zaidi.
 
If this was a matter of a financial boycott then you should have put it expressly. There are not enough wanaharakati to achieve that at the moment maana market share ya voda ni balaa.. Lakini if its a matter of invasion of privacy then that is another issue.. Naomba utusaidie kidogo ndugu, kuwa more clear.

K out.
 

MM, its of no use kutoa vipisi vya habari expecting kila mtu arespond kama tuko kwenye gwaride la KK Security; this is a home of great thinkers and not wanajimu wa kuota una maana gani.... JUST DARE TO TALK OPENLY on this matter...

Surprisingly though, hata wazee wa USAID Tanzania wamehama Voda kwenda ZAIN sijui ni cost au nini?

Please elaborate more or tutafikiri una agenda tofauti... Kuna wake zetu kule Voda wakikosa kazi sijui itakuwaje
 



Mzee Mwanakijiji!

Kama ukimnyanganya mtoto kiwembe ni vizuri ukampatia toy mbadala!! This goes without saying.Kwa hiyo basi ukiwaambia wahame VODA basi waambie wahamie TIGO au Zantel!!

Kwa taarifa zilizo wazi you don't need specs!! Vodacom iliingizwa hapa Tanzania na mafisadi wa CCM na walishinikiza Tanesco kuwawekea umeme kwenye minara yao bure Tanzania nzima na a lot of other logistical support whose cost is worth billions of Tanzania shillings!
Zainab (Zain)formerly ka Celtel is another monster of dirty money laundering!!

Tunakumbuka CCM chini ya Che-Mkapa walivyoipatia hiyo kamapuni TTCL bure na hata pesa inayosemekana walilipa USD 60million walipewa kuongezea mtaji and we all know what happened nao walipata ubwete kwa kudandia infrastructure ya TTCL na baada ya kupata nguvu wakaiacha solemba the dying TTCL !

Actually ukiwa sober we need to nationalize ZAIN bila woga!!

Vinginevyo mimi sio mteja wa hayo makampuni siku nyingi!! Tigo GOT no favors from CCM I don't know exactly why!!
 

Ebu weka price za ZAIN jamvini;

NANI ANA HISTORIA NZURI YA K UANZA KWA CELTEL->ZAIN ya sasa atujuze; nakumbuka wakati ule wa makaburu yakiingizwa kwa nguvu na FFU ofisini then CELTEL after short while ikazaliwa tokana na hawa majamaa? ebu nipeni kidogo;

Naona twataka kuishi kwa frustration sasa vile

NAONA UBAGUZI NDIO UNAANZIA JF TARATIBU? SABABU BADO HAZIKO WAZI SANA KIASI CHA MTU KUTUPA LINE ALIYONUNUA 2001 kabla ya zantel/celtel kuzaliwa; Mmh I BUY QUALITY OF SERVICE; I KNOW QUALITY HAS COST AS WELL
 
Nafikiri kuhama mtandao wa voda siyo ubaguzi wa aina yeyote ile ila ni kupambana na mafisadi mpaka wasalimu amri! waiache Tanzania istawi kama ilivyobarikiwa kuwa na rasilimali tele! wewe kama kweli unataka kupambana na mafisadi huna budi kuacha kutumia bidha zao zote! mwenye kujua bidha za mafisadi azitaje ili tusinunue. Kwa kweli inauma sana na ni aibu kwa nchi yenye kila rasilimali halafu wananchi wake wamechoka mbaya! huduma za jamii aibu tupu!
 

Nakubaliana na wewe . Bei ya bidhaa nayo ikiwa juu mno zaidi ya wengine ni wizi. KWa nini bei zitofautiane kiasi hicho?

Mawasialiano ni muhimu ,lakini fedha yetu tunayoipata kwa jasho la damu ni muhimu zaidi maana ndio zimewafanya wawepo. A reasanable consumer would mind about the price of the product vis vis the available alternatives.

Let us go for better price. After all Tigo ndio walitutoa tongotongo kwenye hili la mobile phone, japo na wao mwanzo walitulamba kweli kweli. Nilikuwa voda toka walivyoingia TZ lakini nimehama mwaka jana tu na sasa naona nafuu kweli kweli.

Kwa wale wasioweka kumbukumbu , hebu tunza vocha zako kwa mwezi mzima uone matumizi yako. Unaweza kufanya maamuzi sahihi ukiwa na data, na kwa hili ni rahisi mno. Voda is damned expensive full stop.
 
kaka leo umechemsha sana,
nilikuona wa maana sana hapa juzi kati lakini kwa hili umenikera sana
 
Je na vyombo vya habari kama Vya IPP,Mwanahalisi nk wanapokea matangazo ya Vodacom vipi nao wasusie matangazo hayo????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…