Enzi ya Rais aliyepita si alipiga marufuku michango mashuleni! Na pesa ipo! Leo imetokea nini haya majanga??Nipo shule ya msingi X jijini Daslamu najitolea, nimepita shule tatu za secondary(moja A level) na mbili za msingi zote zikiwa ni za serikali. Hivyo basi nina uzoefu wa kutosha wa hii jamii ya wanafunzi wa shule za Serikali.
Nilichojionea ni kuwa watoto wengi wa shule ya msingi wengi wao wanaishi na mzazi mmoja na wengine ni wa michepuko yahn Baba ana ndoa lakini ana mtoto nje so anamuhudumia kimya kimya kwa kuja shule na kutoa mahitaji ya hapa na pale ila mtoto anaishi na mama yake.
Kwa utafiti wangu mdogo nimegundua watoto wengi wa darasa la sita ambao mwakani wanaingia darasa la saba wamezaliwa 2009,2010,2011,2012 wengi wao ni watoto wa kwanza ambao walizaliwa bila wazazi kutarajia,hivyo wazazi wengi wao huwa hawadumu kimahusiano na kupelekea mtoto kulelewa na mzazi mmoja.
Siku hizi mashuleni kuna utaratibu watoto kuchangia pesa ya chakula ili wawe wanakula shuleni kuanzia asubuhi na mchana na kwa hapa nilipo mchango ni Tsh 1500.huwezi amini hii pesa kuna watoto wengi tu wazazi wao pesa hii inawashinda na kupelekea kushinda njaa kutwa nzima kila siku kwa week nzima maana wanatoka jioni saa 11.Hapa maana yake ni mtoto anakula kwao tu chakula cha usiku tu,masikitiko.
Miaka ijayo naliona pengo la aliye nacho na asiye nacho likiongezeka katika jamii kwani watoto hawa wanatokea mazingira duni,wanakosa maadili kwa kulelewa na mzazi mmoja, na wengine wakiwa wametelekezwa kwa ndugu. Hiki kizazi lazima kitaongozwa na watoto wa walamba asali ambao wanapata elimu bora na wana mazingira mazuri.
Miaka 15 ijayo tutaanza kujionea matunda ya hiki kizazi.
Picha watoto wakiwa wanafanya mtihani wa kujipima dawati moja wanafunzi watatu mpaka wanne....
Niambie mzazi hapo unasimamia vipi watoto wasiibiane majibu.????
View attachment 2771561
Wizard ipo je inalijua hili !