Wanafunzi wengi wa msingi wanaishi na mzazi mmoja na hali zao ni duni

Mnyunguli

JF-Expert Member
Dec 21, 2020
1,570
3,906
Nipo shule ya msingi X jijini Daslamu najitolea, nimepita shule tatu za secondary(moja A level) na mbili za msingi zote zikiwa ni za serikali. Hivyo basi nina uzoefu wa kutosha wa hii jamii ya wanafunzi wa shule za Serikali.

Nilichojionea ni kuwa watoto wengi wa shule ya msingi wengi wao wanaishi na mzazi mmoja na wengine ni wa michepuko yahn Baba ana ndoa lakini ana mtoto nje so anamuhudumia kimya kimya kwa kuja shule na kutoa mahitaji ya hapa na pale ila mtoto anaishi na mama yake.

Kwa utafiti wangu mdogo nimegundua watoto wengi wa darasa la sita ambao mwakani wanaingia darasa la saba wamezaliwa 2009,2010,2011,2012 wengi wao ni watoto wa kwanza ambao walizaliwa bila wazazi kutarajia,hivyo wazazi wengi wao huwa hawadumu kimahusiano na kupelekea mtoto kulelewa na mzazi mmoja.

Siku hizi mashuleni kuna utaratibu watoto kuchangia pesa ya chakula ili wawe wanakula shuleni kuanzia asubuhi na mchana na kwa hapa nilipo mchango ni Tsh 1500.huwezi amini hii pesa kuna watoto wengi tu wazazi wao pesa hii inawashinda na kupelekea kushinda njaa kutwa nzima kila siku kwa week nzima maana wanatoka jioni saa 11.Hapa maana yake ni mtoto anakula kwao tu chakula cha usiku tu,masikitiko.

Miaka ijayo naliona pengo la aliye nacho na asiye nacho likiongezeka katika jamii kwani watoto hawa wanatokea mazingira duni,wanakosa maadili kwa kulelewa na mzazi mmoja, na wengine wakiwa wametelekezwa kwa ndugu. Hiki kizazi lazima kitaongozwa na watoto wa walamba asali ambao wanapata elimu bora na wana mazingira mazuri.

Miaka 15 ijayo tutaanza kujionea matunda ya hiki kizazi.

Picha watoto wakiwa wanafanya mtihani wa kujipima dawati moja wanafunzi watatu mpaka wanne....

Niambie mzazi hapo unasimamia vipi watoto wasiibiane majibu.????
Screenshot_20231004_132305_GBWhatsApp.jpg
 
Mbaya Zaidi mzazi mmoja anayemlea anatembeza mboga mboga ,anakaanga mihogo kijiweni ,anauza sambusa ,anachoma chapati ...kuweza kupata hata nauli ya mtoto kwenda Shule ,,,hio 1500 ya Kula mnayotaka mama anaisotea toka asubuhi mpaka jion anachoma mihogo ,vitumbua ,sambusa ili aipate na kuna muda haipati .....

Life is not fair..
 
Masikitiko sana ila hii imechangiwa na elimu bure ambayo imepelekea wazazi wanabweteka sana.

Sio tunayotaka ni utaratibu umeletwa na serikali watoto wote wale mashulen
 
Wazungu wenzetu wanawafungia watoto lunch box, watoto wajibebee vyakula wakale mashuleni. Kwanini serikali ama shule haijaweka option hiyo? Kwanini inalazimisha watoto wachange hicho kiasi Cha pesa ambacho mtoto hawezi kukimudu?.siwawaagize watoto waje na vyakula vyao?
Nashangàa hata mimi kuhusu hili, watakwambia uchafu au usumbufu utakuwa mkubwa kusimamia biasness italeta shida mwingine anakula wali mwingine ugali watoto watajisikia vibayaa ,wakatii tunaweza weka utaratibu mzuri tuu hili likawezekana.
 
Hivi unaelewa maana ya duni.....watoto hawa kama siku mwalimu hana mood na msosi ndio hupewa chakula cha walimu na wapo wengi hujui umpe yupi umtose yupi so inabidi uweke ka zamu.
 
Mbaya Zaidi mzazi mmoja anayemlea anatembeza mboga mboga ,anakaanga mihogo kijiweni ,anauza sambusa ,anachoma chapati ...kuweza kupata hata nauli ya mtoto kwenda Shule ,,,hio 1500 ya Kula mnayotaka mama anaisotea toka asubuhi mpaka jion anachoma mihogo ,vitumbua ,sambusa ili aipate na kuna muda haipati .....

Life is not fair..
Kabisa mkuu.iyo 1500 Tsh unawez ona ni ndogo ila ni kubwa kwa watu wengi.
 
Hivi unaelewa maana ya duni.....watoto hawa kama siku mwalimu hana mood na msosi ndio hupewa chakula cha walimu na wapo wengi hujui umpe yupi umtose yupi so inabidi uweke ka zamu.
Nafikili kwa dar ni ngumu ila kwa maeneo ya vijijini kama baadhi ya mikoa kama iringa wachapakazi sana amna kaya itashindwa kumpa mtoto bakuri la viazi au ugali aende nalo shule, ila ela awanaa
 
Kabisa.chamuhimu tujipange before atujaleta kiumbe na kuacha kuzaa hovyo hovyo ka mbwa na haudumii mtoto anakaa na njaa mpka saa 11 jion si ulcers unamtengenezea.

Unasababisha mateso kwa mtoto.
Mzee mitaa nayoishi katika watoto kumi labda mmoja ndo anaenda sekondari, sio kwamba awafaulu la hasha ila awaendi na wazazi awana habari nao wanajali ya watoto wanaokuwa wadogo kwa muda huo sjui hasa shida ni nini mana wengine wanakuwa maskini ila wazazi wanawatia na kusimamia wapate ata form 4 ,elimu kubwa inahitajika iwaingie watu uswahilini na vijijini wazae kwa kupanga
 
Back
Top Bottom