Wanafunzi wengi wa msingi wanaishi na mzazi mmoja na hali zao ni duni

Nipo shule ya msingi X jijini Daslamu najitolea, nimepita shule tatu za secondary(moja A level) na mbili za msingi zote zikiwa ni za serikali. Hivyo basi nina uzoefu wa kutosha wa hii jamii ya wanafunzi wa shule za Serikali.

Nilichojionea ni kuwa watoto wengi wa shule ya msingi wengi wao wanaishi na mzazi mmoja na wengine ni wa michepuko yahn Baba ana ndoa lakini ana mtoto nje so anamuhudumia kimya kimya kwa kuja shule na kutoa mahitaji ya hapa na pale ila mtoto anaishi na mama yake.

Kwa utafiti wangu mdogo nimegundua watoto wengi wa darasa la sita ambao mwakani wanaingia darasa la saba wamezaliwa 2009,2010,2011,2012 wengi wao ni watoto wa kwanza ambao walizaliwa bila wazazi kutarajia,hivyo wazazi wengi wao huwa hawadumu kimahusiano na kupelekea mtoto kulelewa na mzazi mmoja.

Siku hizi mashuleni kuna utaratibu watoto kuchangia pesa ya chakula ili wawe wanakula shuleni kuanzia asubuhi na mchana na kwa hapa nilipo mchango ni Tsh 1500.huwezi amini hii pesa kuna watoto wengi tu wazazi wao pesa hii inawashinda na kupelekea kushinda njaa kutwa nzima kila siku kwa week nzima maana wanatoka jioni saa 11.Hapa maana yake ni mtoto anakula kwao tu chakula cha usiku tu,masikitiko.

Miaka ijayo naliona pengo la aliye nacho na asiye nacho likiongezeka katika jamii kwani watoto hawa wanatokea mazingira duni,wanakosa maadili kwa kulelewa na mzazi mmoja, na wengine wakiwa wametelekezwa kwa ndugu. Hiki kizazi lazima kitaongozwa na watoto wa walamba asali ambao wanapata elimu bora na wana mazingira mazuri.

Miaka 15 ijayo tutaanza kujionea matunda ya hiki kizazi.

Picha watoto wakiwa wanafanya mtihani wa kujipima dawati moja wanafunzi watatu mpaka wanne....

Niambie mzazi hapo unasimamia vipi watoto wasiibiane majibu.????
View attachment 2771561
Enzi ya Rais aliyepita si alipiga marufuku michango mashuleni! Na pesa ipo! Leo imetokea nini haya majanga??
Wizard ipo je inalijua hili !
 
Elimu inahitajika sanaa watu awaelewii ni Kama tumevurugwa planned birth ni chache bongo, mambo ya kila mtoto anakuja na baraka zake
Kuna demu wangu ana miaka 22 kamaliza diploma mwaka juzi sahivi kashabeba mimba ya Mwana mwengine sahivi yuko kwao analea mimba naamini huyu lazima awe single maza.
 
Nyinyi mmefanya tathmin juu hilo buku jero unalolizungumzia, Kwanza watoto sikuiz wanakaa sana mashulen mtoto akitoka sa kumi na mbili had kumi na mbili jioni sijui wanafanya nn na kufeli bado wanafeli. Shuleni ni sehem kujifunza tena kwa ratiba fupi tena iliyovunjwa vunjwa( sio kujifunza all day) waaachien watoto warud nyumbani mapema wapate misosi ya nyumbani. Mnafanya miradi yenu binafs. MNAIJUA
Mradi gani ebu tutajie.
 
Kuna watoto wanakaa kwa ndugu wenye maisha ila mtoto anaishi kama kaokotwa.

Kuna dogo mmoja wa kike kipind hiko yupo kidato cha tatu hawa waliomaliza mwaka jana alitoa mimba ya mienz mitano au minne ila kwao hakuna aliyejua wala shule maana muda wote alikuwa anavaa sweta....alitoa mimba kitoto akakitupa chooni mashoga zake wakaja kureport.......Yule dogo alikuja shangazi yake anayemlea pale shule na V8 private mpaka nikashangaa yule dogo kusoma pale na shangazi ake na mtoto wa kike siku zote asijue.
Kila mtu anangalia familia yake.
 
Kwa kweli ni aibu Mkuu

Yaani unashindwa hata viatu shilingi 3,000 pale Karume ama Nguo zipo za shilingi 1,500 ukienda asubuhi hapo Karume

Aibu Mzee
Point kuu ni uli plan kuleta kiumbe? Kama uliplan mtt awez pitia hayo mazngira.
 
Bora hao wanafunzi wanakaa kwenye madawati shule nyingi wanakaa chini ya miti. Suala la watoto kuwa na malezi ya mama pekee ni hao wanawake kutaka kumkomoa mwanaume kuondoka na watoto. Kutokana na shuruba ya maisha mwanaume hupata unafuu wa maisha na kupotezea kumrudisha mke wake na watoto.
 
Wanapoga majungu shule za private primary(english medium) hawana hoja zaidi zaidi waseme mfuko hautoshi ingawaje kuna shule za english medium pasua kichwa.
Hawana hoja ..
Ungewaacha tu maana ukweli wanao..
 
Point kuu ni uli plan kuleta kiumbe? Kama uliplan mtt awez pitia hayo mazngira.
Hili ni muhimu kulijua kabla hujaenda kumwagia ndani.

Ingawa kuna binti unakuta yupo siku za hatari lakini anakubana miguu wakati unakaribia kufika mlima kilimanjaro, mwisho wa siku mnapata naye mtoto anakosa hata hayo matunzo
 
Wazungu wenzetu wanawafungia watoto lunch box, watoto wajibebee vyakula wakale mashuleni. Kwanini serikali ama shule haijaweka option hiyo? Kwanini inalazimisha watoto wachange hicho kiasi Cha pesa ambacho mtoto hawezi kukimudu?.siwawaagize watoto waje na vyakula vyao?
Kuna shule moja private walikuwa na huu utaratibu, mtoto mmoja mama yake akawa anampa chakula anamwekea majitu gani halafu anamwambia akawape wenzake ila yeye asile, ikawa watoto wote wanakula kile chakula baada ya shku kadhaa wanaweweka na kuanguka, uchunguzi ulivofanyika yule mtoto akagundulika, wakamfukuza na wakaachana na ule utaratibu. hii ni africa mkuu.
 
Nipo shule ya msingi X jijini Daslamu najitolea, nimepita shule tatu za secondary(moja A level) na mbili za msingi zote zikiwa ni za serikali. Hivyo basi nina uzoefu wa kutosha wa hii jamii ya wanafunzi wa shule za Serikali.

Nilichojionea ni kuwa watoto wengi wa shule ya msingi wengi wao wanaishi na mzazi mmoja na wengine ni wa michepuko yahn Baba ana ndoa lakini ana mtoto nje so anamuhudumia kimya kimya kwa kuja shule na kutoa mahitaji ya hapa na pale ila mtoto anaishi na mama yake.

Kwa utafiti wangu mdogo nimegundua watoto wengi wa darasa la sita ambao mwakani wanaingia darasa la saba wamezaliwa 2009,2010,2011,2012 wengi wao ni watoto wa kwanza ambao walizaliwa bila wazazi kutarajia,hivyo wazazi wengi wao huwa hawadumu kimahusiano na kupelekea mtoto kulelewa na mzazi mmoja.

Siku hizi mashuleni kuna utaratibu watoto kuchangia pesa ya chakula ili wawe wanakula shuleni kuanzia asubuhi na mchana na kwa hapa nilipo mchango ni Tsh 1500.huwezi amini hii pesa kuna watoto wengi tu wazazi wao pesa hii inawashinda na kupelekea kushinda njaa kutwa nzima kila siku kwa week nzima maana wanatoka jioni saa 11.Hapa maana yake ni mtoto anakula kwao tu chakula cha usiku tu,masikitiko.

Miaka ijayo naliona pengo la aliye nacho na asiye nacho likiongezeka katika jamii kwani watoto hawa wanatokea mazingira duni,wanakosa maadili kwa kulelewa na mzazi mmoja, na wengine wakiwa wametelekezwa kwa ndugu. Hiki kizazi lazima kitaongozwa na watoto wa walamba asali ambao wanapata elimu bora na wana mazingira mazuri.

Miaka 15 ijayo tutaanza kujionea matunda ya hiki kizazi.

Picha watoto wakiwa wanafanya mtihani wa kujipima dawati moja wanafunzi watatu mpaka wanne....

Niambie mzazi hapo unasimamia vipi watoto wasiibiane majibu.????
View attachment 2771561
Mbona nyumba nyingi hata zenye baba na mama mlo ni mmoja nao kati ya saa 9 na saa 10 jioni, hali hii imezoeleka na ni ya ya kawaida sana.
 
Back
Top Bottom