Wanafunzi wengi wa msingi wanaishi na mzazi mmoja na hali zao ni duni

Wqzazi hawakushindwa ila hawakuona umuhimu wa kusomesha.

Ujamaa uliiharibu Tanzania na unaendelea iharibu.

Elimu yatakiwa igharamikiwe
Nadhani suala la exposure lilichangia Wazazi wengi kutowapeleka shule Vijana wao.

Siku hizi hadi jamii ya Wafugaji wanawapeleka shule za bei kubwa watoto wao.

Kuna kikao cha Wazazi tulifanya, nilishangaa kuona Wamasai wanawatoto pale shuleni. Baada ya kikao nilifanya nao mazungumzo, wakasema wao wameona kuwekeza kwenye Elimu za watoto wao ni muhimu wakati huu, maana mifugo huwa inakufa kwahiyo ni vyema watoto wasome ili waje waajiriwe ama wajiajiri kupitia ufugaji wa kisasa.

Imagine ada ilikuwa ni 2.8M kwa mtoto na yeye alikuwa na watoto 3 pale wakati huo mimi nina wawili tu 😆
 
Kuna watu wanatoa maoni unajiuliza huyu mtu ana waza nini kichwani kwake!!
Kumbe wengi hawana watoto!
Kwa mtu alie mzazi kuna namna anachangia unaona kabisa haya maoni ni ya mtu mzima.
Kama hamuwezi lea watoto na kuwahudumia acheni kuzaa
 
Hapo sijasema watoto wanavyoanza kubanduliwa wakiwa darasa la5, 6 na 7.
Hiyo haifai boss, mtoto wa shule ya msingi haifai kubanduliwa maana inakuwa ni kama ubakaji.

Tuwaache wasome wafike Elimu ya Juu huko ndiyo wawe huru kushiriki ngono.
 
Na huku mtaani ukiwa na miaka 25 huna mtoto utasikia mbuzi zinasema huna mtoto unasubiri nini! Ukiwa mkubwa mtoto atakusaidia. Na wakati huo mbuzi hizo hizo hazimsaidii mzazi wake kwa lolote, tena unazisaidia kutunza mtoto wake.
 
Kama hamuwezi lea watoto na kuwahudumia acheni kuzaa
Inaweza kuonekana ni kawaida kuzaa au ni vyepesi au ni kuamua tu, lakini ndugu yangu naomba kukuambia tokeo la mwanadamu yoyote dunia si kwa maamuzi ya mtu isipo kua huyo mwenye kutengeneza uhai.
Unapomuona mtoto amezaliwa hata kama ni kwa mazingira ya namna gani amini usiamini si kwa maamuzi ya yule aliyemzaa iwe kwa kutaka ama asitake.
 
Hiyo haifai boss, mtoto wa shule ya msingi haifai kubanduliwa maana inakuwa ni kama ubakaji.

Tuwaache wasome wafike Elimu ya Juu huko ndiyo wawe huru kushiriki ngono.
Haifai vipi huku mzazi analeta malalamiko mtoto wa darasa la saba kafumwa gheto kwa mdau.
 
Inaweza kuonekana ni kawaida kuzaa au ni vyepesi au ni kuamua tu, lakini ndugu yangu naomba kukuambia tokeo la mwanadamu yoyote dunia si kwa maamuzi ya mtu isipo kua huyo mwenye kutengeneza uhai.
Unapomuona mtoto amezaliwa hata kama ni kwa mazingira ya namna gani amini usiamini si kwa maamuzi ya yule aliyemzaa iwe kwa kutaka ama asitake.
Mmhh kwahiyo mambo ya uzazi wa mpango ni uongo?

Umeingia kiimani wakati haya mambo hata hayapo kiimani ni maamuzi ya wazazi.
 
Nipo shule ya msingi X jijini Daslamu najitolea, nimepita shule tatu za secondary(moja A level) na mbili za msingi zote zikiwa ni za serikali. Hivyo basi nina uzoefu wa kutosha wa hii jamii ya wanafunzi wa shule za Serikali.

Nilichojionea ni kuwa watoto wengi wa shule ya msingi wengi wao wanaishi na mzazi mmoja na wengine ni wa michepuko yahn Baba ana ndoa lakini ana mtoto nje so anamuhudumia kimya kimya kwa kuja shule na kutoa mahitaji ya hapa na pale ila mtoto anaishi na mama yake.

Kwa utafiti wangu mdogo nimegundua watoto wengi wa darasa la sita ambao mwakani wanaingia darasa la saba wamezaliwa 2009,2010,2011,2012 wengi wao ni watoto wa kwanza ambao walizaliwa bila wazazi kutarajia,hivyo wazazi wengi wao huwa hawadumu kimahusiano na kupelekea mtoto kulelewa na mzazi mmoja.

Siku hizi mashuleni kuna utaratibu watoto kuchangia pesa ya chakula ili wawe wanakula shuleni kuanzia asubuhi na mchana na kwa hapa nilipo mchango ni Tsh 1500.huwezi amini hii pesa kuna watoto wengi tu wazazi wao pesa hii inawashinda na kupelekea kushinda njaa kutwa nzima kila siku kwa week nzima maana wanatoka jioni saa 11.Hapa maana yake ni mtoto anakula kwao tu chakula cha usiku tu,masikitiko.

Miaka ijayo naliona pengo la aliye nacho na asiye nacho likiongezeka katika jamii kwani watoto hawa wanatokea mazingira duni,wanakosa maadili kwa kulelewa na mzazi mmoja, na wengine wakiwa wametelekezwa kwa ndugu. Hiki kizazi lazima kitaongozwa na watoto wa walamba asali ambao wanapata elimu bora na wana mazingira mazuri.

Miaka 15 ijayo tutaanza kujionea matunda ya hiki kizazi.

Picha watoto wakiwa wanafanya mtihani wa kujipima dawati moja wanafunzi watatu mpaka wanne....

Niambie mzazi hapo unasimamia vipi watoto wasiibiane majibu.????
View attachment 2771561
Kupata mimba bila kutarajia ni kweli kulelewa na mzazi 1 nikweli umealaya ulikithiri ni kweli,ila kuhusu mafanikio ya maisha hapo baadae ni siri ya muumba sio makisio yako wengi walifauru na wengi wakaferi lakini walio fali masomo walikuja kuwajiri walio faulu,kuhusu wanye nacho na wasionacho hili pengo aliwezi kuisha hata huko unakudhani kuwa ndio wajanja pengo hilo lipo,usisahau maisha ya dar yalivyo kuwa magumu sana kwa watu wengi
 
Mmhh kwahiyo mambo ya uzazi wa mpango ni uongo?

Umeingia kiimani wakati haya mambo hata hayapo kiimani ni maamuzi ya wazazi.
Sawa, lakini binafsi naamini hata mtoto azaliwe mazingira ya namna gani si uwezo na matakwa ya kibinadamu, uhai ni moja ya vitu vilivyo nje ya uwezo wa mwanadamu.
 
Wazungu wenzetu wanawafungia watoto lunch box, watoto wajibebee vyakula wakale mashuleni. Kwanini serikali ama shule haijaweka option hiyo? Kwanini inalazimisha watoto wachange hicho kiasi Cha pesa ambacho mtoto hawezi kukimudu?.siwawaagize watoto waje na vyakula vyao?
Ungakuwa kuwa karibu yangu ninge kupa mkono tosheka na hii kauli yangu ya kwamba akili yako ni kubwa tatizo viongozi wa nchi hii awana tabia ya kuchukua mawazo ya watu na kuyafanyia kazi
 
Nyie mnaoponda shule za private za msingi(english medium)na kupigia upatu shule za msingi serikali endeleeni kujidanganya.
Katika moja ya vitu ninavyomwomba mwenyezi Mungu anisaidie ni uwezo wa kuwapa wanangu elimu bora. Kwa nchi yetu Tanzania elimu bora kwenye shule za serikali a.k.a Kayumba inapatikana katika shule chache sana.
 
Kabisa.chamuhimu tujipange before atujaleta kiumbe na kuacha kuzaa hovyo hovyo ka mbwa na haudumii mtoto anakaa na njaa mpka saa 11 jion si ulcers unamtengenezea.

Unasababisha mateso kwa mtoto.
Maisha ya dar pia ni magumu sana mfano mtu mwenye watoto 2 nauli 2000 kula 2000 nauli ya mzazi 2000 hele ya kula na maji 4000 hela ya matumizi nyumbani 10000 haya ndio maisha ya mtu wa hali chini bado kodi ya nyumba matibabu nk unakuta mtu kamomaa heti siwezi kuishi mikoani ukweli mikoani bado kuna unafuu wa maisha
 
Ni kweli mkuu.naona berlyn ajauona umasikini anajaribu kucompare ulaya na bongo kuhusu lunch box?kweli

Mtu anauwezo wakutoa 1500k atawezaje kuandaa lunch box.?
Lunch box ya kiswahili ni vipande via mihogo chapati maandazi vitumbua jambo hili linawezekana tatizo serikali haina uwezo wa kutambua raiya wake waishi vipi wafanya nini
 
Back
Top Bottom