Wanafunzi wachoma moto pikipiki ya mwalimu, wafyeka shamba kisa adhabu ya kukutwa na simu shuleni

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida linawashikilia wanafunzi sita wa Shule ya Sekondari Mwenge iliyopo Kata ya Majengo Wilaya ya Singida kwa tuhuma za kuchoma moto pikipiki ya mwalimu yenye namba za usajili MC 653 BFS pamoja na kufyeka mahindi yaliyooteshwa katika shamba la mwalimu huyo lenye ukubwa wa ekari moja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, ACP Stella Mutabihirwa amezungumza mbele ya waandishi wa habari na kusema tukio hilo limetokea baada ya kuadhibiwa kwa mwanafunzi wa Kidato cha Nne kwa kosa la kumiliki simu kinyume na taratibu za shule hiyo.

“Taratibu za shule hiyo haziruhusu mwanafunzi kuwa na simu, wakati upekuzi wa walimu unaendelea kuna mwanafunzi mmoja alitoka kwenda kuficha simu darasani, ndipo mwalimu baada ya kugundua akamuadhibu huyo mwanafunzi.

“Jioni yake wanafunzi hao wakajipanga na kwenda kuchoma pikipiki na shamba, Jeshi la Polisi limefika eneo la tukio na kujiridhisha juu ya pikipiki hiyo kuchomwa na shamba kufyekwa. Hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao kwa kusababisha uhaibifu,” anasema ACP Stella Mutabihirwa.


Source: Wazo Huru TV
 
aina hii ya wanafunzi ilipigwa fimbo za matako na chalamila,halafu wazazi wakachangishwa gharama kesi ikaisha.
wenye mtindio wa akili wakaloloma kwamba ni uonezi,sasa nategemea sheria ichukue mkondo wake,wafukuzwe shule,na gaharama zilipwe.
 
Heheh pamoja sikubaliani na utovu wa nidhamu Ila Hawa vijana ndio wa enzi zetu. Mwalimu akitaka kutoa adhabu alikuwa anajikagua mara mbili mbili maana anajua tukitoroka na tikakutana nae mtaani ajue ameumia.

Waliacha hadi kutufundisha eti tumekuwa watukutu na tukapasua almost wote wa mwisho alikuwa na 2.12 A level huyo ndio failure.

Ila Sasa tumeshakuwa watu wazima lakini mie Kama ni mwanangu hapo najua nimezaa dume sio Hawa wavaa kata K anakuja kuoa anapigwa makofi na mwanamke na anashangilia tu.
 
Kuna unoko gani sasa hapo...

Sheria za shule haziruhusu kumiliki simu huyo mwanafunzi anatumia Ili iweje,🤞🏾🙏🏿
Sheria za kipumbavu tu watu wapo smart world nyie mnaendelea kushikilia masheria ya kikoloni zama hizi wanafunzi wa secondary waruhusiwe kumiliki smart phone ziwasaidiek masomo Yao nchi nyingi tu hasa za Asia mfano Philippine,Hongkong,Thailand watoto wa sekondary kumiliki Simu ni kitu Cha kawaida tu Tena Zina msaada mkubwa sana huko ndiko kinakotoka kizazi Cha smart world wanajua Kila kitu wale sisi huku kijana wa Miaka 17 hajui hata kuwasha computer Wala hajui google ni Nini
Halafu ndio utegemee mageuzi ya kisasa Kwa Jamii kalagha bhaho
Tutaendeshwa na wachina na wahindi mpaka kiama!
 
Back
Top Bottom