Wanafunzi wa kike waua mwalimu wao... Adaiwa kutaka kumbaka mwenzao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi wa kike waua mwalimu wao... Adaiwa kutaka kumbaka mwenzao

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by lifeofmshaba, May 28, 2011.

 1. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #1
  May 28, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  [​IMG] Adaiwa kutaka kumbaka mwenzao
  [​IMG] Ni mwalimu wao wa nidhamu

  Wanafunzi wa Chuo cha Uuguzi cha Bulongwa kilichoko Wilaya ya Makete mkoani Iringa, wamemuua kwa kumshambulia kichwani mkufunzi wa chuo hicho, Dk. Jumbe Mafingo, kwa madai ya kupinga jaribio lake la kutaka kumbaka mwanafunzi mwenzao.

  Taarifa za awali za makachero wa polisi zilieleza kuwa mkufunzi huyo aliuawa baada ya kutuhumiwa kwamba alitaka kumdhalilisha kijinsia mwanafunzi wa kike, Jean Laison Mwakabuta kwa kutaka kumbaka.

  Tukio hilo la kuuawa kinyama kwa mkufunzi huyo ambaye ni mwalimu wa nidhamu chuoni hapo, lilitokea juzi usiku nyumbani kwake mjini hapa.

  Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, Dk. Mafingo alifikwa na umauti baada ya mwanafunzi huyo kuamua kwenda nyumbani kwake usiku ili kumkabidhi maelezo yake ya kimaandishi kuhusu sababu zilizomfanya alale nje ya chuo.


  Ilielezwa kuwa muda mfupi baada ya kuingia kwenye nyumba ya mwalimu huyo, mwanafunzi huyo alianza kupiga kelele kuwa anabakwa.


  Alisema kufuatia kelele hizo, wanachuo wengine waliamka katika vyumba vyao na kwenda hadi eneo la tukio na kuanza kumshambulia kichwani mkufunzi huyo hadi kumuua.


  Kamanda Mangalla alisema Dk. Mafingo aliuawa kwa kushambuliwa na kitu kizito kichwani.

  “Huyu Jean Laison Mwakabuta, aliambiwa na Dk. Mafingo ambaye ni mwalimu wa nidhamu chuoni hapo, aandike maelezo ya maandishi kwa sababu gani alilala nje ya chuo,...baada ya kuandika maelezo hayo, aliamua kuyapeleka nyumbani kwa mkufunzi huyo usiku, sasa baada ya kugonga mlango na hatimaye akaruhusiwa kuingia, alianza kupiga kelele kwamba anabakwa…na ndipo wanafunzi wenzake waliposikia kelele wakaamka na kukimbilia eneo hilo na kumshambulia mkufunzi huyo hadi kufa,” alisema Kamanda Mangalla.

  Ilidaiwa kuwa siku moja kabla ya tukio hilo, uongozi wa chuo hicho cha Bulongwa ulitoa ridhaa kwa wanachuo wote kwenda kutembea nje ya chuo kwa lengo la kuwapunguzia msongo wa mawazo ya masomo na Jean Laison Mwakabuta hakurejea chuoni hadi siku iliyofuata.


  Kamanda Mangalla, alisema wanachuo wanne akiwamo mwanafunzi Jean, wametiwa mbaroni kuhusiana na mauaji hayo.


  CHANZO: NIPASHE


  maoni: hivi watu wanashindwa kuoa wake zao wa halali, naona kina dada nao wameshituka sasa
   
 2. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Mkuu naona moja kwa moja umedrive ur own conclusion. Hii story ina masuali mengi ya kujiuliza kabla kutoa hukumu.
   
 3. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mkuu barua za kiofisi na nyumbani kwa DR usiku wapi na wapi?
  kunamchezo wa kuwatumia dada zetu wasio na ujasiri wa maisha na ina dalili zote
  yawezekana katika ili tukio hakuna kitu lakini kama kanuni zingefuatwa sidhani kama haya yangetokea
   
 4. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #4
  May 28, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Huyo mwanafunzi anatakiwa ajibu mengi zaidi. Ni utaratibu wa shule kupeleka barua nyumbani kwa mwalimu usiku? huyo mwalimu alikuwa anaishi na nani? Ukizingatia walimu wengi wa nidhamu huwa wanachukiwa, hakuna uwezekano wa huyo mwanafunzi kuwa chanzo?
   
 5. S

  Son of Alaska JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2011
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 2,813
  Likes Received: 102
  Trophy Points: 0
  HERE for justice to be seen to have been done jail terms are unavoidable-any sane person will condemn this act,mob justice has no place in the modern world. Dr J was innocent,any guiltyness would have to be jurdicated in a court of law.Hopefully the killers will face the full wrath of the law.
   
 6. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #6
  May 28, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,248
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Nimesoma kwa makini habari hii kuna maswali mengi kabla yakukubali kuwa kweli alitakiwa kubakwa!
  1. Mwanafunzi wa chuo ni mtu mzima hawezi kupeleka barua nyumbani kwa mwalimu badala ya ofisini
  2.Inawezekana ulikuwa ni mpango wawanafunzi kumkomesha mwalimu huyo kwa tabia yake yakuwabana!
   
 7. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hapo kuna mengi sana yamejificha. Kwanza mara nyingi walimu wa nidhamu huwa hawapendwi, pili kwanini barua ipelekwe usiku? tena nyumbani kwa mwalimu? Yawezekana ilikuwa setup,kwa sababu huyo mwanafunzi alijua fika kuwa akianza kupiga kelele watu watakuja na kumsaidia ili kumuundia zengwe mwalimu asimfuatilie deal zake. Inawezekana dada hakujua mambo yangegeuka kuwa mabaya kiasi hicho.
   
 8. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Na mkuu wa chuo akamatwe, kwa nini barua zinapelekwa nyumbani?
   
 9. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #9
  May 28, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mimi bado nasimama kweli suhala kwamba walimu wanamchezo wa kupata ngono kwa kutmia ofisi kutoka kwa wanafunzi
  hasa hawa wa nidhamu, sina hakika kama yeye alikuwa kundi hilo maana sikuwa kwenye eneno la tukio lakini , kama mwalimu angelikuwa sio mtu wa totozi
  sidhani kama hata mwanafunzi angepeleka barua nyumbani usiku,
  madaktari na totozi ndio zao BANA mtu dada anakwenda hospitali na jipu chini ya goti anaambiwa atoe nguo zote.
  waliliza hapa wanasema.
  hii inaweza kuwa kokote kuna shida.
  kwanza kwa nini alimkalibisha ndani ?
   
 10. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #10
  May 28, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyo bint Jean Liason ni Mzushi!
   
 11. A

  Aisha Adam JF-Expert Member

  #11
  May 28, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kazi kwelikweli! Huyo mwanafunzi ana kesi ya kujibu na anaweza kufungwa.
   
 12. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #12
  May 28, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Du hii kali.kikawaida haileti maana,kwanini apelekee barua nyumbani kwa mwalimu?kwanini aipelekee usiku?haiwezekani aingie tu alafu mzee ajaribu kumbaaka bila hata ya kumzingua kwa maneno kwanza..huyo dada ana kesi kubwa hapo
   
 13. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #13
  May 28, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Ni mapema sana kutoa conclusion katika jambo hili bila uchunguzi wa kina, kwani kuna maswali inabidi yajibiwe.
  1. Kwa nini aamue kupeleka barua kwa mwalimu usiku?
  2. Kama mwalimu alikuwa mwadilifu na anayesimama katika misingi ya malezi, kwa nini aliamua kumfungulia mlango?
  3. Kama ingekuwa mwanafunzi anawahi deadline ya kuandika na kupeleka maelezo, kwa nini mkufunzi alimkaribusha ndani?

  Bado hapa kuna kitu inabidi kijibiwe ikiwa ni pamoja na uongozi wa chuo na wa wanafunzi kutoa maelezo kama waliishawahi kupokea malalamiko yanayoonesha dalili za mkufunzi kujihusisha na vitendo vya udhalilishaji kijinsia, isijekuwa ni mgogoro asili kati ya wanafunzi na walimu wa nidhamu ambao daima huwa hawapendwi.
   
 14. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #14
  May 28, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Wakawanaza kuandika hiyo habari alisema hivi

  --------
  BRECKING NEWS: DAKTARI AUAWAWA MAKETE KISA MAPENZI!!!

  Usiku wa kuamkia jana wanachuo wa Taasisi ya Afya cha Bulongwa Hospitali (Maarufu kama chuo cha Dental na Nursing) wamemvamia, kumpiga, kumjeruhi na hatimaye kumuua daktari wa hospitali ya Bulongwa Dr. Jumbe.

  Taarifa zilizoufikia mtandao wa indaba africa zinaeleza kuwa Daktari Jumbe amesomea udakatari wa?tiba ya binadamu nchini?Urusi na aliletwa na wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kufuatia upungufu wa madaktari katika hospitali ya Misheni Bulongwa.

  Chanzo?cha mauaji hayo inadaiwa ni wivu wa mapenzi. tutazidi kuwaleteeni kadili tunavyopata kutoka makete

  Kutoka kwa mdau Jackson Mbogela aliyeko Makete
  --------
  Source: INDABA AFRICA: BRECKING NEWS: DAKTARI AUAWAWA MAKETE KISA MAPENZI!!!

  Anyway we tend to think we know each other on face value, kwa Dr. Jumbe hukumu yake iko kwa mungu haki yake ya kuzulumiwa uhai wake hawezi ipata hapa duniani!!!
   
 15. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #15
  May 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Safi sana tablet....

  There is more inside story kuliko hiyo
  jiulize kwa culture ya bongo, tena vijijini kama Bulongwa, inakuaje mtoto wa kike aliyelala nje ya shule anakwenda kwa mwalimu wa nidhamu ambaye alikua mnoko sana shuleni billa woga?
  Huyu mwalimu kwa nini alifungua?
  How long didi it take from binti kuingia ndani hadi kelele?
  Inakuaje wanafunzi wote wawe tayari ready and armed kumvamia mwalimu?

  Tuelewavyo sisi, ni kwamba hii kitu ilisukwa na ina mtu mwingine ambaye si mwanafunzi ana atajulikana very soon
   
 16. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #16
  May 28, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Hayo ni mauwaji ya kukusudia, kabla sijasome i thought ni wanafunzi
  wa primary (maana hata ufikiri upo chini kidogo) hao sasa ni bifu zao likely,
  kweli inasikitisha saana....

  R. I. P. Mafingo...
   
 17. Mpenda Siasa

  Mpenda Siasa Member

  #17
  May 28, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Aaaaah ngumu kuhamini ..inaonekana ni mpango uliopangwa wa kumkomoa mkufunzi...Barua usiku? nyumbani? aah wapi mpango ,RIP Dr J
   
 18. n

  nchasi JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 525
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Huyo mwanafunzi anahatia. Bora mkufunzi asingekufa, kila litakalokuwa judged kuhusu yeye ni wazi kabisa hakuna ubishi kuwa walimuundia zengwe mkufunzi ili awe kwenye safe side. Anajutia uamuzi wake usiokuwa na busara.
   
 19. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #19
  May 28, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hii kitu hii, itauwa wengi.
   
 20. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2011
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama nidhamu ya mtu mbaya yaani kutofuata taratibu za shule pia lazima fikra na upembuzi wa kimawazo wa huyo mtu ni mbovu. Ndoo maana huyu dada starehe zimempoza, alikuwa kanogewa huko hadi kufikia maamuzi kuwa mwl. wa nidhamu kikwazo. Hivyo ili aweze kula raha bac ni kummaliza mwl. Huyo apalekwe gereza la wanaume aipate zaidi hiyo kitu.
   
Loading...