Polisi wamng'ang'ania mwanafuzi aliyemjeruhi mwalimu wake

Kikwajuni One

JF-Expert Member
Mar 18, 2013
13,142
6,947
Mwanafunzi wa shule ya sekondari Tamabu wilayani hapa Mkoa wa Mwanza, Alex Butawantemi aliyejemruhi mwalimu wake kwa panga anaendelea kusota rumande hadi uchunguzi ukamilike.

Tukio la mwanafunzi huyo Alex Butawantemi kumjeruhi mwalimu wake Stanford Mgaya kwa panga kichwani na mkono lilitokea Sepetemba 25, 2023 wakati mwalimu huyo akiwa ofisini akitekeleza majukumu yake.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi leo Septemba 28, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mtafungwa ameliambia Mwananchi kuwa bado wanamshikilia mwanafunzi huyo na wanaendelea na uchunguzi kabla ya kumfikisha mahakamani.

"Bado tunamshikilia na tutaendelea na uchunguzi juu ya tukio alilofanya mwanafunzi huyo uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani,” amesema Mutafungwa.

Septemba 26, 2023 Mwananchi lilifika Hospitari teule ya Wilaya ya Sengerema kumjulia hali mwalimu Stanford Mgaya aliyekuwa amelezwa akipatiwa matibabu na alisema hali yake inaendelea vizuri.

Leo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema, Mwita Waryoba amesema mwalimu huyo kwa sasa anaendelea vizuri na ameruhusiwa kutoka hospitali Septemba 27, 2023 na kujerea nyumbani huku akiuguza majeraha yake.

"Jana Ndiyo ameruhusiwa na nyumbani kwake akiendela kuuguza majeraha tunaimani ndani ya muda mfupi atajerejea kazini na kuendelea kutekeleza makumu yake alisema Waryoba.

Mwanafunzi huyo ni moja kati ya wanafunzi 17 waliokuwa wamepewa adhabu shuleni hapo kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu, hata hivyo mwenyewe hakukubaliana na adhabu hiyo na kudaiwa kumshambulia mwalimu wake.

Mwanafunzi huyo kabla ya kutenda kosa hilo alimufuata mwalimu ofisi huku akimweleza kuwa mwalimu nimefika leo ofisini kwako ili tumalizane juu ya adhabu uliyokuwa umenipa.

Shule ya sekondary Tabamu imekuwa ikikumbwa na majanga ndani mwaka huu, likiwemo tukio la kuchomwa moto kwa baadhi ya vyumba madarasa kutokana na mabweni ya mtu binafsi walivyokuwa wanatumia wanafunzi.

Chanzo: Mwananchi
 
Unafikiri wasipozingua kwa watoto mlionao majumbani kutakuwa na shule hapo
Pia mwanao akiuliwa kupitia ukatili wa walimu wapumbavu ushangilie.

Hivi unaamini huyo mwanafunzi ni kichaa from nowhere aende kumshambulia mwalimu?

Hapo ukute mwalimu katoa adhabu ya kudhalilisha utu wa mwanafunzi akaona hapana siwezi kudhalilika kiasi hiki ndo akachukua uamuzi aliochukua.

Kila mara unasikia mtoto kauliwa na mwalimu kupitia adhabu za kipumbavu na wengine kupata ulemavu wa kudumu.

Walimu wengi ni failures kwahiyo matumizi ya nguvu ni makubwa kuliko akili.
 
Sema walimu na nyie badilikeni aisee, kuna walimu shule ni wanoko sana.

Mwalimu kama mshahara wako unaingia kila mwezi unahangaika na toto la mtu ili iweje? Watoto wengine wana male mabovu na vichaa unahangaika nae wa nn?

Mambo mengine mnajitafutiaga matatizo tu
 
Back
Top Bottom