Wanafunzi wa Kidato cha 5 wanaanza lini Kusoma?

Poisonous

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,477
2,000
Tafadhali Wizara husika na Serikali iliangalie hili tena ( Upya ) kwani Wanafunzi wa Kidato cha Tano ( 5 ) Kumaliza Shule November na kukaa Idle ( Mtaani ) mpaka July mwaka unaofuata ni Kuhatarisha sana Ustawi wao wa Kitaaluma na Kuwaathiri Kimaadili na hata Kisaikolojia pia.

Kiukweli 24/7 tunapishana nao sana katika Nyumba za Kulala Wageni ( Gesti na Loji ) wakienda ' Kungonoliwa ' huku wengine tukikesha nao 24/7 pia katika Vijiwe vyetu vya Kulanduka ' Bange ' hali ambayo kama Kaka na Wazazi watarajiwa inatukera na kutuumiza zaidi.
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,959
2,000
Tafadhali Wizara husika na Serikali iliangalie hili tena ( Upya ) kwani Wanafunzi wa Kidato cha Tano ( 5 ) Kumaliza Shule November na kukaa Idol
Bila shaka ulikuwa unamaanisha Idle. Idol yalikuwa mashindano ya Coca Cola ambayo Langa, Witness pamoja na Sha waliibuka washindi kule Sauzi.
 

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,959
2,000
Kiukweli 24/7 tunapishana nao sana katika Nyumba za Kulala Wageni ( Gesti na Loji ) wakienda ' Kungonoliwa ' huku wengine tukikesha nao 24/7 pia katika Vijiwe vyetu vya Kulanduka ' Bange ' hali ambayo kama Kaka na Wazazi watarajiwa inatukera na kutuumiza zaidi.
Wewe kama mzalendo unachukua hatua gani kuhakikisha taifa la kesho halivuti bangi au kujihusisha na ngono wakiwa wangali wanafunzi? Umetoa taarifa serikali ya mtaa au Polisi?
 

LUBEDE

JF-Expert Member
May 7, 2013
4,269
2,000
Oyaa,waacheni watoto wafanye na kufanywa,unataka waanze lini?
hiyo pia ni life experience,hakuna ubaya wowote..usiumie wala usiwaonee huruma,kwani ndio maisha...
 

Beberu

JF-Expert Member
Jan 26, 2017
971
1,000
Hii shida ya kulilia serikali kila kitu itatuua kama taifa

Sasa wew mzazi ni kichwa panzi hadi ushindwe kumlea mtoto wako ? Yani kumuongoza mtu mmoja mzazi unashindwa ? Duuu tunapotea aiseeee

Wazazi wapambane kuhakikisha maadili na mienendo ya watoto wao ipo sawa sio kuwaachia serikali

NB hatupo ujamaa tena ndugu zangu
 

MWANDENDEULE

JF-Expert Member
May 24, 2015
3,057
2,000
JKT kwa mujibu wa sheria iwashukue wao badala ya kidato cha vi ili huo muda wa toka Novemba hadi Juni) wakafunzwe uzalendo kama hakuna uwezekano wa kupunguza muda wanaokaa bila kusoma (Novemba - Julai)
 

mwita ke mwita

JF-Expert Member
Aug 13, 2010
7,673
2,000
Wakae kufanya kazi pamoja wazazi kama wazazi wanajihiusisha na kilimo nao walime na kuangalia ng'ombe kama baba ni muuza duka wake dukani wauze, kama baba ana ofisi binafsi wawahi maofisini wakafagie na kukaa kama receptionist, kama ni mama ntilie wakaoshe vyombo na kuhudumia, kama wazazi ni fundi mchundo waende huko kujifunza, kama mzazi unajiweza huu ndio muda wa kuwapeleka hawa watoto wakasilimie ndugu, vijijini na kwa wajomba mijini, wakajifunze kulala sebuleni kwa watu,
vijana ni muda pia wa kujifunza kuwafanya ma hausigeli wasiliwe na bodaboda
 

MEXICANA

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
1,612
2,000
Pamoja na kwamba technologia imerahisisha utendaji kazi wa shughuli mbalimbali,mpaka sasa wizara ya elimu haijatoa selections za watoto wetu kuingia kidato cha tano.

Kuna generation ipo kwenye system ambayo haitaki kabisa kuendana na kasi ya technolojia (TEHAMA).
Haingii akilini kabisa,matokeo mmetoa Mwaka Jana,mpaka tunaingia nusu ya Mwaka mwingine selections hamtangazi.
 

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
1,430
2,000
Ni mwezi Wa sita sasa kasoro siku moja. Majina ya waliochaguliwa kujiunga kidato cha tano bilabila.

Kwa kawaida mwezi Wa saba zinapofunguliwa Shule nao yawapasa kujiunga (sijui kuhusu mwaka huu) imekuaje wadau? Hivi mwaka jana ilikuwa hivihivi?
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
29,077
2,000
Kun kitu, I guess kinapikwa. Maana Jiwe alikuwa na tabia ya kuzifanya shule za Kata zionekane zinafaulisha kama private.
 

Demi

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
25,349
2,000
Wanatoa selection bado wiki moja kufungua shule, pambavu sana.
 

MEXICANA

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
1,612
2,000
Mm nikiangalia technolojia ilivyo sasa na huu upuuz wa wizara ya elimu napata hasira sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom