Wanafunzi vyuo vikuu waandamane kupinga malipo ya Wabunge? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi vyuo vikuu waandamane kupinga malipo ya Wabunge?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 15, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Badala ya kuandamana kudai ng'ombe atoe maziwa zaidi kwanini wasiandamane kutaka ng'ombe alishwe zaidi ili atoe maziwa zaidi? Au kwanini wasiandamane kupinga maziwa ya ng'ombe kupewa watu wachache zaidi huku wengi wakijitahidi kumlisha ng'ombe huyo?

  Wanafunzi wa Vyuo vikuu na wananchi wengine wana haki ya kupinga malipo ya kifisadi ambayo yanafanyika kwa jina la "ubunge"; kwanza siyo tu wakatwe posho na mishahara ya wabunge wote isitishwe kuongezeka kwa miaka miwili ijayo. n.k n.k n.k Au wanafikiri hizo posho na malipo ya wabunge zinatoka wapi kama siyo katika kodi za watoka jasho wa Tanzania?
   
 2. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  VYUO VIKUU MUONGEE SASA HIVI AU MCHAGUE KUNYAMAZA
  MILELE JUU YA HIZI ANASA ZA SERIKALI KATIKA USO
  WA JAMII ILIOPIGIKA NA KUKATISHWA TAMAA!!


  ... kama hat hilo la milioni 90 kwa mbunge mmoja hawalioni basi sijui wanasoma nini chuo kikuu.

  Hela hii wanaopewa kila mbunge, mbali na mshahara na maruourupu nyinginezo, bima ya afya na nyumba, ni kiasi cha fedha ambacho wakipewa wote mahesabu yake ni sawa na kusomesha chuo kikuu wanafuni wa Masters kwa idadi:

  1. Ada ya Mwanafunzi mmoja wa Masters mpaka kumalia shule ni wastani wa Tsh. 4,500,000/-.

  2. Hivyo Mbunge mmoja anapopewa hela za bwerere Tsh 90,000,000/- ni sawa na kusema kawanyima nafasi ya kusoma chuoni watoto wa walipa kodi 20.

  3. Na pale ambapo zaidi ya wabunge 360 wanatarajia kupewa hela hiyo ni sawa na kusema watoto wa walipa kodi 7,200 hapati haki.

  4. Na ukizingatia ukweli kwamba mfanya kazi mmoja tu hutegemewa ama moja kwa moja au kwa njia nyinginezo na watu wasiokua na kipato cha uhakika wastani wa watu 15; hii inamaanisha kwamba serikali KWA MAKUSUDI inatayarisha bahari la Wamachinga na omba omba wasiopungua 108,000 ambayo nayo itakua ikijiongeza kwa mtindo wake

  5. Nako pia msisahau kwa Dowans ikilipwa leo hizo bilioni 76 (wastani wa Tsh 114 trilioni) kitapeli sasa hapo ndio taifa tutakua tumekosa kusomesha kama hao kwa idadi ya milioni 26 endapo vipaumbele wetu ni kupereka tu watu shule.

  KWA MTINDO HUU TAIFA HILI SI KIPINDI KIREFU KITAVUNA HASIRA ZA AKINA MOHAMED BOUSAZIZI WENGI WENGI SANA endpo katiba mpya, ambayo ndio imebeba majibu haya ma-extravagance yote, itaendelea kuchezewa kama tunavyoona hivi sasa.
   
 3. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mzee Mwanakijiji,

  Nakumbuka 2003 nilikuwa mmoja wa walioongoza mgomo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Zitto alikuwepo pia.

  Bado nakumbuka fikra zetu zilikuwa nini. Tulifikiri zaidi kuhusu sis kuliko nchi! Ndivyo ilivyo leo. Bado tunasafari ndefu. Wasomi hatuwezi kulinganisha au kuoanisha mambo. Malipo ya dowans vs mikopo au malipo ya wabunge vs matatizo ya shule zetu!
   
 4. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  TUNATAKA MCHAKATO WA KATIBA MPYA NA TUME HURU
  YA UCHAGUZI BUNGENI SASA HIVI!!!


  Enyi Ndugu Waheshimiwa viongozi wetu

  akina Kikwete, Dr Slaa, Prof Lipumba, Mbowe, Julius Mtatiro, Zitto Kabwe, Mbatia, Dr Mvungi, Prof Baregu, Prof Mukandala, Dr Bana, Dr Azaveli, Mama Nkya, Ndg Mgaya, Makwaia wa Kuhenga, Jenerali Ulimwengu, Reginald Mengi, Pius Msekwa, Fredrick Sumaye Fredrick Msuya, John Malecela, Mama Anna Makinda, Sheik Issa Bin Simba, Mhe Iddi Simba, Maaskofu na Wachungaji wote nchini, Denis Mwamnyange, Said Mwema, The Othma's, Tundu Lissu, Sitta, Mwakyembe, Mzee Mkapa, Mzee Salim Ahmed Salim, Mzee Sinde Warioba, Mzee Butiku, Prof Sarungi, Selasini, Ole Sendeka, Tido Mhando, Mama Maria Nyerere, Mama Karume, Selelii, Prof Bangu, Dr Matumaini, Bashe, Celina Kombani, Kafulila, Hamad Rashid, Regia, Lukuvi, Mama Maghimbi,Mama Anna Abdala, Pombe Magufuli, Mstaarabu wa Siasa Tanzania - Dr Mohammed Shein, Salmin Amour, Godbless Lema, Mzee Mwanakijiji, Maxence Melo, Candid Scope, Fareed, Mwakalebela, Mnyika, Halima Mdee, viongozi wote wa serikali za wanafunzi vyuoni ... na wengine wengi wengi wengi tu, sisi kama vijana wa nchi hii sasa hivi tunawaulizeni nyote kwa pamoja kwamba ...

  ... suala letu la michakato wa kujiandikia KATIBA MPYA na kuunda Tume Huru ya Uchaguzi ZINAANZA LINI BUNGENI???
   
 5. Samawati

  Samawati Member

  #5
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 90
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 13
  HIVI TANZANIA NI NCHI MASKINI AU WATU WAKE NDIO Maskini? nASHINDWA KUELEWA.WAJUZI MNIPE SOMO.

  HAYA MAPESA YA KUMWAGA HIVI YANATOKA WAPI???BABU YANGU KULE KIJIJINI ATAKUFA BILA HATA KUYAFAIDI MATUNDA YA UHURU!

  NDIO maana wengine siye TUNAPIGA BOX NJE..HATUPENDI LAKINI KULIKO FEDHEHA HII YA KUPIGIKA KIMAISHA NDANI Y ANCHI YETU WENYEWE..BORA TUKAWE WATUMWA WA kazi ugenini!

  Nyie wabunge..hamna tofauti n watumishi wengine.Mnapokwenda kwa waajiri wenu ( wananchi) kuomba kazi ka kura..mnaendaa mikono nyuma na hata kuwapigia hadi watoto wadogo magoti.Mkipata kura/kula mnaweka mikono mfukoni - ishara ya DHARAU!
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Hii nchi hakuna mpigania haki kila mmoja analinda tumbo lake.
  Wabunge wa chadema wa organize kupinga posho ya wabunge nahisi hii itaungwa mkono na wanachi karibu wote, na sio ushagubagu wa diwani wa arusha kwa masilahi binafsi.

  Kwanini wanafunzi wakati wao wanapigana ili wamalize masomo na kwanini isiwe wabunge kwa maana hii ndo inawafanya wawe pale, hii kazi ya wabunge.
   
 7. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Tutavuna tulichopanda
   
 8. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  We acha tu, inakatisha tamaa. Hakuna cha maslahi ya taifa wala nini. Wanafunzi wa kileo kama walivyo malecturer wao (iwe UDASA, Dodoma,nk.) wakiandamana au kugoma, basi ni kwa ajili ya matumbo yao tu.
   
 9. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Wabunge wanachukua milioni 90 kujadili ukosaji wa umeme na pesa za wanafunzi. Vilevile East African newspaper imesema Tanzania haina pesa ya kuendesha nchi kwa sasa. Pesa zote zimetumika kwenye kampeni!!!
   
 10. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #10
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du naunga mkono hoja, km wanavyuo wote wanagoma kutaka nyongeza hadi 10,000/= na maslahi bora pamoja na Elimu na hawapati hivi kweli kwanini wasiandamane kuwashinikiza WASICHUKUE 90,000,000/= kwa kila Mbunge kwa ajili ya gari (Shangingi)
  Tuache tu unafiki wa Vyama na kuona malipo yanaenda Dowans, matatizo ya umeme hebu km mna uchungu muwavamie Wabunge Bungeni kupinga posho zaidi maana imekuwa km Kenya
  Mtakumbuka Dr Slaa alishasema posho ni kubwa sana wanayochukua Wabunge naona wote mtakumbuka
   
 11. D

  Dopas JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Asante Mzee Mwanakijiji kwa hoja nzuri, tatizo sisi watanzania sijui tunasumbuliwa na ujinga(ufahamu), au sijui nini? Labda tunajua hela hizo wanazotanuanazo JK na waandamizi wake (bila ulazima) kuwa ni kutoka kodi zetu, lakini kwanini tunapuuza zikitumiwa na wachache kwa manufaa binafsi?

  Lakini nani atusemee? Tungefanya uchaguzi leo, nina hakika baadhi ya wabunge hata wa Chadema(Chama tunachotegemea kituletee Ukombozi), wasingepata kura wao, kwani tayari wapiga kura wanajuta kwanini wamewapa nafasi hiyo.

  Kwa mfano unategemea nini kwa Mbunge anayesema vijana wa Vyuo vikuu wasijihusishe kabisaaa.... na siasa. Anasahau kwamba wanavyuo ndio wanasiasa wa leo na kesho. Hawa ndio wakombozi au waangamizi wa Taifa letu leo na kesho.

  Ila ninatiwa moyo na Wabunge wengi wa Chadema ingawa wapo vibaraka wachache, wanaofanya jitihada ya kufungua matawi katika vyuo vya elimu ya juu. Ili kuwaelimisha hawa vijana wajibu zao katika jamii ya Tanzania.

  Tukirudi kwenye hoja ya msingi, vijana unaowazungumzia kuwa waandamane, ni wachache wenye uelewa huu, japo hao ndio 'wasomi wetu'. Sina hakika kama wanafahamu nafasi yao na kuwa sauti yao ina umuhimu kiasi gani katika maendeleo ya nchi hii.

  Naunga mkono wanavyuo vikuu kuandamana hata kama ikitokea baadhi watapoteza maisha kwa faida ya wanaobaki. Nasema hivi kwa sababu inauma wanafunzi wanavyuo vikuu hawana pa kulala(UDSM walimwambia Waziri Mkuu wanalala nje), hawana chakula: wanaomba kuongezewa Ths 5,000/-, ambao ni mlo moja tu wanaambiwa 'wafie mbali', hakuna hela 'ya kuchezea'.

  Kama hakuna hela ingeeleweka, ila inasikitisha zaidi pale hela ya kununua mashingingi ya Wabunge kwa bei ya mil 90 x idadi ya wabunge ipo, tena fasta.

  Wabunge ambao wana malipo na marupurupu lukuki, ambao kwa marupuru yao tu wangeweza kupata usafiri wao, labda serikali ingewaongezea mkopo kidogo 25% ya kununua magari yasiyo ya kifahari sana,(yasiyozidi mil 45).

  Sio haki wanafunzi kunyimwa elfu 5 tu kwa siku, hawana pa kulala, hawana chakula, hawana daftari, hawawezi kusafiri kwa daladala, hawawezi kufanya fotokopi, ilhali hela ya kufanya mengine ya kifahari IPO fasta.

  Wanafunzi wa vyuo vikuu waamke. Wasifikiri bado wao ni '... lala mwanangu... hakuja kucha.... Wasidanganyike!!!!
   
 12. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2011
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mlioichagua JK na watu wake ndio mliosababisha yote hayoo... Mungu awasaidie mjuteeeeeee halafu mrekebishe makosa. Kabla ya 2015 Fashisti, nduli, dikteta CCM awe ameondoshwa!!!!!!!!
   
 13. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2011
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Wabunge wa chama makini ndo walianzishe hili.Mhhh ama nao wanalinda matumbo yao.Teh teh the teh

  Yani kazi ya wabunge makini ndo mwabebeshe watoto tena wengine chini ya miaka 18.
   
 14. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  True Mkuu kama kuna kitu I feel strongly about ni matumizi ya Kodi yangu..., kweli kabisa this is serious Issue na nina uhakika wananchi wengi huko vijijini wangejua the extent kodi yao inavyofujwa wangefeel the same
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  ukidondoka fikiria namna ya kunyanyuka sio namna ulivyodondoka.
   
 16. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  hili nalo NENO..
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Bado tuna safari ndefu kwa kweli.
   
 18. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  [maoni yangu. hisia zangu. zenye harufu ya ukweli]

  serikali ya tanzania inafanya makusudi kwa watoto hawa wa vyuo vikuu.

  watawala wanajua kuwa wengi wa hawa wanafunzi ni watoto wa walalahoi.

  watoto wa wakulima wa jembe la kupinda mgongo.

  hizo kodi (P.A.Y.E) unazosema hawakatwi wazazi wao. hawana haki ya kudai kodi wanayokatwa vibopa wanaokurugenzi mashirika mbalimbali ya serikali (ambao kimsingi hawa ni watawala wenyewe au watoto wao).

  au gunia mbili za mahindi anazovuna mzee Ng'wanidako kule kijijini zinakatwa P.A.Y.E? kama ni hivyo sawa. waendelee kudai. vinginevyo waingie kitaa kama Tunisia na Masri. au wanyamaze tu waendelee kupewa msaada (mkopo) kwa huruma.
   
 19. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Wabongo bado sana,i said it before!inasikitisha sana kwasababu kuna watakaokata tamaa na hii nchi, kuna ambao wameshafanya hivyo,wengine wanakula na vipofu...Subiri uone kama kuna watakaokataa hayo malipo yenye kukufuru ama kama wanafunzi/wananchi wataandamana.
   
 20. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,725
  Likes Received: 3,143
  Trophy Points: 280
  Mods naomba msinifungie maana nitakachoandika hapa kitawaudhi. Tafadhali niwie radhi. Ni hivi hawa wabunge wa vyama vyote tuliwatuma waende wakalilie haki yetu au tuliwatuma waende kujirusha? Hivi kweli hata haya hamna nina maana ya wabunge wote iwe ni chadema ccm tlp na vingine mimi sifahamu majina ya vyama vingine.... hospitali hazina dawa shule hazina madawati halafu ninyi mnajilimbikizia mali mimi naona dawa sasa ni kuwasha moto kieleweke huu ni upumbavu uliozidi mipaka. Ole wenu wabunge ole wenu mkiwageuzia macho na mgongo wale waliowapigia kura. Haya Mbowe, Regia, Mnyika, Zitto tuelezeni mnachukua hayo magari au kuna tamko mtatoa??????mtujibu haraka maana sisi ndio tuliowachagua
   
Loading...