I concur....washkaji waliokuwa mazuzu darasani wameshatusua sana maisha....yaani wako mbali sana
Ufaulu mkubwa unasaidia kama ukitaka kuendelea kusoma huko vyuoni na siyo kwenye kupata Ajira.
Huyo kachelewa sana kujua hilo.
Mimi kuna watu nawajua wanafanya kazi, mishahara mpaka 1.5M kwa mwezi, kusafiri ndani ya nchi kwa siku malipo Tsh 10,000 na pesa ya nauli ya ofisi, tena sonetimes ndege.
Hotel ya kufikia inakodishwa na ofisi na kulipiwa kila kitu.
Lakini elimu darasa la 7 tu tena wengine hawajui hata kusoma vizuri. Sisi tuliotoka vyuoni ndio tunawasaidia kutoa pesa ATM.
Narudia tena ufaulu mkubwa utakusaidia kusoma mikozi huko vyuoni, kwenye ajira ni mara chache sana.
off topic kidogo, Kwenye portal upande wa Afya kuna sehemu ya kujaza na ku-upload document kama mtu alishawahi kujitolea ?Kweli Mkuu!!
Huyu kijana alinichekesha sana kimoyo moyo nikasema laiti angejua matokeo yangu sijui kama angekuja pale stationary
Nimecheka leo nilipokuwa maeneo ya mjini huko, nilisikia vijana wakilalamika kuwa; wanajuta kufaulu kwa kiwango cha juu kwani hakuna maana yoyote na haisaidii popote pale.
Nina kiji-internet Cafe changu hapa mjini, sasa baada ya kusikia tangazo la ajira za waalimu na afya, nikasema acha nisimamie shoo mwenyewe kupiga pesa za wasaka ajira. Ofisi yangu ilianza kufurika jana saa tisa na mpaka saa nne usiku nilikuwa nao waomba ajira.
Sasa kinachonifanya niandike hapa, ni mwalimu mmoja mwenye umri wa miaka 29, aliyemaliza mwaka 2015 chuo cha DUCE.
Maneno yake yalinifanya nicheke lakini yalinitafakarisha sana.
Vyeti vyake vya O kevel anadivisheni one ya 16 masomo tisa. A'Level anadivisheni one ya 9 Combination ni PCM. Transcript yake niliona anaka-GPA ka 3.8 kutoka pale mlimani/Duce Ambapo GPA hiyo sio haba kwa kweli hasa kwa masomo ya Physics na Mathematics.
Yule kijana alisema akiwaambia wenzake aliokuja naye, baada ya kusifiwa kwa ufaulu huo ambao kimsingi ni mkubwa, yule kijana akasema;
"Kinachoniumiza ni kuwa nilijitesa bure ili nipate ufaulu mkubwa kwa lengo nikimaliza shule na chuo nisipate shida kupata ajira. Ninachoshangaa ni kuwa wenzangu wenye ufaulu mdogo wao ndio wanaajiriwa, mimi niliyekaza na kukesha usiku na kufaulu mpaka sasa nasota. Huu mwaka unaenda wa sita naomba ajira serikalini nakosa"
Maelezo hayo yalinichekesha kwani ni kweli kabisa, na yalinigusa hata mimi kwani mimi nilifaulu kwa madaraja ya mwisho kabisa.
O'level nilipata divisheni three ya 24, A'Levele nikapata divisheni three ya 15, Chuo kikuu nikapata GPA ya 2.6. Ingawaje sijasoma ualimu wala udaktari, lakini nilipata kazi mapema sana, miaka ya 2011 licha ya kuwa fani niliyosomea ajira zake ni ngumu kupatikana na wasomi ni wengi. Nilipata kazi nikiwaacha solembe wenye shule na misonge yao
Kufaulu sana sio kupewa kazi, acheni kujichosha vijana walioko chuoni au wanafunzi mlioko shuleni.
Muhimu elimu ikae kichwani zaidi.
Poleni sana mliojifanya chuoni hamli bata kisa kitabu
Povu Ruksa
Mkuu nani kakwambia ukiwa na 2.6 huwi Prof?Sasa mfano mtu anataka kuwa profesa bado unashauri asisome sana ili apate ka gpa ka 2.6 kama kako?
Maelezo hayo yalinichekesha kwani ni kweli kabisa, na yalinigusa hata mimi kwani mimi nilifaulu kwa madaraja ya mwisho kabisa.
O'Level nilipata divisheni three ya 24, A'Level nikapata divisheni three ya 15, Chuo kikuu nikapata GPA ya 2.6Ingawaje sijasoma ualimu wala udaktari, lakini nilipata kazi mapema sana, miaka ya 2011 licha ya kuwa fani niliyosomea ajira zake ni ngumu kupatikana na wasomi ni wengi. Nilipata kazi nikiwaacha solembe wenye shule na misonge yao
Kwani professa haruhusiwe kusoma akiwa na pass ?Sasa mfano mtu anataka kuwa profesa bado unashauri asisome sana ili apate ka gpa ka 2.6 kama kako?
Kwa mfumo wa Tanzania huwezi kuwa Prof kwa GPA hiyo iliyotajwa hapo.Kwani professa haruhusiwe kusoma akiwa na pass ?
Vigezo vya TCU kwa watu wanaostahiki kuwa wakufunzi na wahadhiri wa madaraja mbalimbali vyuoni ndio vimemwambia hivyo.Mkuu nani kakwambia ukiwa na 2.6 huwi Prof?
Watu wengi course ya ualimu walifuata priorities za mkopo nothing elseDivision 1 ya pcm kusoma degree ya ualimu ni ujinga... coet na conas kuna kozi kibao