Wanafunzi 33 na walimu 2 waliofariki kwa ajali ya basi Karatu, Arusha wazikwe pamoja. Mnara ujengwe

Kila mwenye mtoto huenda akawa keshamchukua ili akazike na ndugu zake. Hata hivyo si lazima wakizikwa pamoja ndo mnara ujengwe. Hata akizikwa kila mmoja kwao, eneo la tukio mnara hujengwa.
Refer Shabiby ilivoua kule Songea mnara ulijengwa
Wanajeshi waliokufa pale Kisongo Arusha mnara ulijengwa.
 
Huyu atakuwa hana mtoto/watoto,sio kosa lake tumsamehe tu.Maana wazo lake hata mimi limenishangaza.

Sio wazo baya na sio lazima wazikwe pamoja ili mnara ujengwe. Mwaka 1999 wanafunzi wa shule ya mazoezi Patandi uko Arusha walipata ajali wakiwa wanatembelea ngorongoro crater na kusababisha vifo vya wanafunzia zaidi ya 15.
Mnara umejengwa kwenye hiyo shule,wenye majina ya wanafunzi wote waliopoteza maisha kwenye ajali.
 
Wanaweza wakazikwa kila mwanafunzi na kwao,mnara ukajengwa eneo la tukio.
 
Hii ajari imenikwaza sana kupita maelezo. Nawaonea huruma sana wazazi wa vitoto hivi kweli ni maumivu makali sana.

Mungu awatangulie na azilaze roho zao mahala palipo pema milele yote.

Amina!
 
Uzuri wa wazo hili ni nini?sijaona. Nisaidie. Na ungekuwa wewe mzaz ungekuwa tayari mtoto wako azikwe sehemu moja na wengine 30?
Uko vizuri sana. Hili wazazi wengi hawatalikubali hata chembe.
 
Siyo tu ana wazo la kushangaza ila ni la kijinga kabisa. Maana sioni mantiki ya kuzika hao watoto pamoja ikiwa wanatambulika kila mzaz anamtambua mtoto wake why wazikwe pamoja?

Hili ni wazo la kipuuzi la mtu ambaye hana mtoto au hategemei kupata. Au hajali hajui maana ya mtoto ni nin. Mzazi mwenye akili timamu hawezi toa wazo la kipuuzi kama hili.
Huyu atakuwa hana mtoto/watoto,sio kosa lake tumsamehe tu.Maana wazo lake hata mimi limenishangaza.
 
Back
Top Bottom