Wanafunzi 33 na walimu 2 waliofariki kwa ajali ya basi Karatu, Arusha wazikwe pamoja. Mnara ujengwe

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Ndugu zangu wanJF,

Kutokana na msiba huu kubwa mkubwa kitaifa, napendekeza marehemu hawa wazikwe mahali pamoja iwe eneo la kumbukumbu na kuwaenzi watoto, ndugu, jamaa zetu.

Serikali kwa kushirikiana na wafiwa, ndugu, jamaa na shule husika tujenge mnara eneo la tukio kama ambavyo imewahi kufanya maeneo mengine, kama kumbukumbu ya marehemu hawa.

AJALI YA MV BUKOBA: Marehemu walizikwa pamoja na mnara ulijengwa huko Igoma, Mwanza.

AJALI YA WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD MORINGE SOKOINE:
Mnara ulijengwa pale Wami SOKOINE, Dakawa Morogoro.

KIFO CHA MWANDISHI WA CHANNEL 10, DAUDI MWANGOSI:
Mnara ulijengwa pale Nyororo, Mafinga Iringa.

KIFO CHA ALPHONCE MAWAZO:
Mnara ulijengwa

images.jpeg

Edward Moringe Sokoine
images-1.jpeg

Alphonce Mawazo.
 
Hapo ni mpaka Ruhusa itoke kwa wazazi,kumbuka mv Bukoba waliozikwa pamoja ni wale walioshindwa kutambulika.Kumbuka pia Imani huplay role katika mazishi.Sidhani kama wazazi waislam ama wakristo watakubali watoto wao wachanganywe,Maana hawa watoto wanatambulika so mazishi ya pamoja is impossible.
 
Uko vizuri sana. Hili wazazi wengi hawatalikubali hata chembe.

Back
Top Bottom