Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 15,311
- 9,740
Ndugu zangu Watanzania,
Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita, nyota ya matumaini na nuru ya wanyonge atawaongoza viongozi mbalimbali pamoja na watanzania katika ibada maalumu ya kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Hayati Edward Moringe Sokoine itakayofanyika Tarehe 12-4-2024,siku ambayo ndiyo alipofariki Dunia kwa ajali ya gari iliyotokea pale Mkoani Morogoro.
Ajali hiyo inasemekana kuna gari liligonga gari alilokuwepo kiongozi huyo na kupelekea kifo chake.japo haieleweki na ni kitendawili juu ya vipi na namna gani gari hilo lilipata nafasi ya kuingilia msafara wa waziri Mkuu na kupata mpaka nafasi ya kulifikia gari lililombeba waziri mkuu anayekuwa na msafara wa kutosha na ulinzi wa kutosha huku gari za ving'ora zikiwa mbele.lakini pia haileweki ni vipi gari hilo liliweza kuachwa mpaka linapelekea kwenda kugonga gari la waziri Mkuu ambaye gari zake zinakuwa katika mwendo wa kasi na kwa kufuatana karibu karibu. Ok hili tuliache tu maana hata mimi sina majibu na nilikuwa sijazaliwa.kikubwa tumuombee wazirii mkuu wetu ili Mungu aendelee kumuangazia mwanga wa milele.
Hivyo katika kumkumbuka ya kumkumbuka familia imeandaa ibada maalumu ya kumkumbuka itakayofanyika kijijini kwake Enguik Monduli juu wilayani Monduli. Hayo yameelezwa na msemaji wa familia ndugu Lembris Kipuyo. Ambapo amesema katika siku hiyo mambo mbalimbali yataelezwa hasa yale ambayo aliyafanya hayati wakati wa uhai wake kwa Taifa letu. Lakini pia kuna Taasisi ya Hayati Edward Moringe Sokoine ambayo imejikita katika kilimo,afya,vyanzo vya maji,hifadhi ya mazingira pamoja na elimu ambayo imeanzishwa.
Amesema Hayati Edward Moringe Sokoine atakumbukwa sana kwa mchango wake hasa katika Secta ya kilimo na mifugo ambayo pia ilichochea kuanzishwa kwa chuo cha kilimo Sokoine ,katika juhudi za kuhakikisha kuwa wataalumu wa kutosha wa kilimo wanazalishwa ili kufanikisha na kuhakikisha Taifa lina kuwa na chakula cha uhakika.
Hayati Edward Moringe Sokoine alizaliwa mwaka 1934 Agosti 1mkoani Arusha wilaya ya Monduli.ambayo mpaka sasa imetoa mawaziri wakuu wawili ambao wote wametangulia mbele za haki.
Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.