GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,647
- 109,034
Najua kuwa Kifo hakichagui, ila Kupunguza athari yake Kijamii inawezekana kama tu ukiwa makini.
Hivi kwa mfano Ndugu mpo 30 mnatoka Dar es Salaam kwenda Shughulini Mkoani Dodoma kwanini nyote mpande Gari / Moja?
Kwani mkijigawa Watu Watano Watano mpande Gari / Basi tofauti tofauti kwenda huko muendako ili hata kama ikitokea Ajali basi msiathirike Wote na Wengine wabakie kuendelea na Maisha na Kutunza Familia za Walioondoka?
GENTAMYCINE miaka ya nyuma hapa hapa JamiiForums nilianzisha Uzi ( Thread ) ya Kupinga Ndugu wengi Kusafiri pamoja kwenda Mikoani / Safarini ili kuepusha madhara Makubwa kama yakitokea bahati mbaya sikueleweka vyema na sasa yale niliyoyakemea yanaanza Kutokea.
Bahati nzuri nina Ndugu zangu hapa JamiiForums wakiongozwa na Mdogo wangu kabisa wa damu steveachi huu Utaratibu wangu Kaka ( Ndugu ) yao GENTAMYCINE wanaujua kwani tukiwa tunaenda Safari yoyote ile hata kama nikiwa hapa hapa Dar es Salaam au Morogoro ( Makao Makuu yetu ya Ukoo ) huwa sipendi Kusafiri na Ndugu wengi katika Gari / Basi moja na badala yake huwa Nawagawa ili hata kama likitokea la kutokea basi tusiondoke Wote angalau wengine wabaki.
Ajali ya Jana iliyoua Ndugu Wanne wa Familia Moja waliokuwa wakienda Msibani imeniumiza mno na kunifanya nikumbuke Ajali zingine za muundo huu huu na kuna moja ilitokea Bahari Beach ambayo kabla ya Watoto ( Ndugu ) hao Kuondoka Kwao GENTAMYCINE niliwakatalia hadi Kugombana na Mmoja wao kwa Kuwazuia wasipande Gari moja kwakuwa aliyekuwa akiwaendesha alikuwa ameshaanza Kulewa na baada ya dakika 30 nikapigiwa Simu kuwa kuna Ajali Mbaya imetokea na nilipoenda nikakuta ni wale wale Ndugu Sita ( 6 ) na Wote walifia pale pale baada ya Kugonga Mti mkubwa na leo imekuwa ni Historia.
Imagine Ajali Mbaya iliyotokea Jana imechukua wana Ndugu Wanne ( 4 ) na Kuwaacha Wazazi Wao wenye Umri wa miaka zaidi ya 85 ambao ndiyo walikuwa Wakiwategemea kwa kila Kitu.
Kila nikijaribu Kuvaa Viatu vya hawa Wazazi naona havinitoshi sana sana Huruma ( Huzuni ) juu yao inanipata huku kwa mbali Machozi yakinilenga.
Namalizia kwa Kusisitiza kuwa simaanishi kama Kusafiri pamoja ( kwa Uwingi wenu ) kama Ndugu ni Kosa au Vibaya ila kama Binadamu na Mtu wa kuona mbali naona haina Afya sana na badala yake Tahadhari ikichukuliwa kwa Ndugu Kujigawa kuna Faida nyingi kwa Familia zao na Ustawi wa Koo zao na Vizazi vyao.
Naziombea Roho za Marehemu ( Ndugu ) waliofariki Ajalini jana Mkoani Pwani Mwenyezi Mungu azilaze Roho zao mahala pema peponi.
Poleni Wafiwa, Ndugu, Jamaa na Marafiki kwa huu Msiba mkubwa. Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina lake Lihimidiwe.