Wewe na gamba lako gumu lisilo vuka ndio unawasemea UKAWA?Wana Jf wasalaam!
Likiwa joto la uchaguzi limeanza kupanda lakini kwa upande wa UKAWA bado wana mtihani mkubwa sana kumchagua atakaye wawakilisha kwenye kinyang'anyiro cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
Wana UKAWA wengi wamekuwa wakipendelea Mh prof .Lipumba apeperushe bendera ya UKAWA kwani kwa sasa ana mvuto ndani na nje ya UKAWA kuliko Dr Slaa ambaye anaonekana kulazimisha lazima agombee!
Wana Jf mwezi December nilipata nafasi ya kukaa na vijana kama kumi pale Tengeru na tulibadilishana mawazo kuhusu siasa za Tanzania na wengi walijikita kujadili nani anafaa kugombea Urais kati ya Lipumba na Slaa hapa ndio ubishi ulipo anza na wengi walitaka Slaa apumzike wakisema Lipumba ndio anaye faa kipindi hiki kama wanataka kuchukua nchi na atawasaidia kufuta zile propaganda za udini.
Lakini wengine walishikilia msimamo kuwa hata kielimu Lipumba anamzidi Slaa kwani Slaa hana Elimu yeyote zaidi ya kusomea dini na Ikulu hatupeleki kiongozi wa dini kwakweli kwenye hili walibishana sana wengi wakisema Elimu ya Slaa haitambuliki kimataifa na si mtaalam wa jambo lolote.
Kuna mwingine aliendelea kusema kuwa Slaa hafai kugombea Urais maana amekuwa akichochea migogoro ndani ya chama chake na kuwagawa wanachama kwenye makundi!
Wengi walikuwa wana sisitiza kuwa patachimbika kama Lipumba hatopitishwa na hakutakuwa na maelewano kwenye hilo na wakasema Lipumba asipopitishwa kura zao watampa mgombea wa CCM kama walivyo fanya 2010!
Wana Jf joto la uchaguzi liliendelea nilipo pata safari ya kwenda Tanga nilipita mtaa fulani pale Tanga mjini na hapo nilikuta wakijadili siasa kwa upana na wengi walionekana kuunga mkono UKAWA na walikuwa wanasema wana furahishwa na mwenendo wa UKAWA lakini wana kerwa nakampeni za chinichini zinazo fanywa ili kumpitisha Slaa kugombea Urais.. na wengi walikuwa wakiongea kwa jaziba huku wakisisitiza kuwa mipango ya kumpitisha Slaa kugombea Urais hazito kubalika na patachimbika kabisa siku hiyo na hawatoburuzwa na mtu...
Kuna kijana mmoja alisema kuwa wao kama UKAWA wana mhitaji Lipumba lasivyo patachimbika ..maana wanaona dalili za mizengwe! Pia alisema ana kerwa na baadhi ya viongozi wao kuwatuma vijana wao kwenye mitandao ili wawapambe na kuwapigia campaign wakati muda bado....na aliendelea kusisitiza kuwa "kama chadema wanataka kuwajua CUF ngangari kwa vitendo wajaribu mizengwe".
Kwakweli wana Tanga walionekana wenye imani kubwa na Lipumba na walisisitiza kuwa ni wakati sasa Mchumi huyo kuiongoza nchi hii!
Karibuni wana jamvi!
Aaaaah tafadhari ndugu, kaa na magamba yako uache kudandia safari usioijua.