Wana JF Usiishi Kienyeji: Mbinu Aliyoitumia Yesu Kutoboa; Ijaribu na wewe utoboe!

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,527
14,403
Denis Mpagaze
_____________________
Kila kona ya Dunia hii Yesu anajulikana. Tena anajulikana kwa wanaomkubali na wasiomkubali. Unajua kwa nini? Ni kwa sababu hakuishi kienyeji. Kuishi kienyeji maana yake ni kuishi maisha ya business as usual. Maisha ya sisi tunafanyaga hivi, hatufanyi hivyo! Unaishi kwa za kuambiwa tu bila kuchanganya na za kwako. Ajabu sana. Au tuseme ni maisha ya wengi wape bendera hufuata upepo!

Unafanya kazi ya uvuvi kwa sababu baba yako alikuwa mvuvi, na mwanao atakuwa mvuvi. Mnaitwa ukoo wa wavuvi. Hadi huruma! Yesu angekubali kuishi kienyeji angekufa ni Fundiselemala kwa sababu baba yake alikuwa Fundiselemala, lakini alikataa. Kwanza aliondoka kwao bado mdogo. Hakusubiri kuotea ndevu nyumbani! Bila kutoka kwenu huwezi kukua. Unakuaje na wakati unakula bure? Mchungaji Mgogo anasema kama unakaa kwenu na umri umekwenda na wala haununui hata chumvi hunatofauti na paka. Bora hata paka anakula panya waharibifu.

Hata kuamini hauna akili kwa sababu walimu wako wamekwambia huna akili ni kuishi kienyeji. Hivi kama akili ni nywele na kila mtu ana zake kwa nini ukubali huna akili na wakati nywele unazo? Cha ajabu aliyekwambia huna akili hakulishi. Maisha ya kienyeji bana. Mtu unajlisha mwaka mzima mfululizo bila kuomba halafu unajiona mnyonge asiye na akili; unafeli sana ujue.

Ndo yaleyale ya kuogopa kuoa mwanamke aliyesoma sana kwamba atakudharau. Hayo ni mawazo ya kienyeji. Unaishi maisha ya kimaskini kisa unaogopa kuoa mwenye pesa, atakudharau. Hivi kuna mtu alikufa kwa sababu ya kudharauliwa? Achana na fikra za kienyeji, tafuta mke mwenye mawe walau muanze pazuri. Kwanza umri umekwenda, halafu unakomaa kutafuta maskini mwenzako. Hii haikubaliki. Maskini tafuta tajiri na tajiri tafuta maskini tubalance maisha bana!

Hata kuogopa kusoma sana kwamba utakosa mume ni kuishi kienyeji. Hebu soma uone kama utakosa mume. Ni wanaume wa kienyeji tu ndio wanaogopa kuoa wasomi. Wajanja wanasomesha kabisa wake zao wawe juu sana. Nimesema wanasomesha wake zao siyo wachumba zao. Kusomesha mchumba yataka moyo mkuu! Lakini kama unaweza fanya hivyo.

Lakini hata wewe binti unayeogopa kusoma sana kwamba utakosa mume nani alisema maisha lazima uolewe? Eti kuolewa ni bahati. Nani kasema! Basi kama kuolewa ni bahati basi kuoa ni balaa. Masuala ya ndoa yakufanye ukaishi kienyeji! Kwani Yesu alimuoa nani? Mbona aliishi fresh tu na watu kibao wanatamani maisha yake? Toka kwenye cave ya Plato uone utamu wa mambo! Toka mafichoni ubadilishe mambo ufaidi. Kataa taratibu zinazokunyima tija. Hata Yesu alifanya kazi siku ya sabato wenyeji wakashangaa. Akawambia tulizeni mpira; Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, lakini si mwanadamu kwa ajili ya Sabato.

Maana yake ni kwamba maisha ya kienyeji yasikuzuwie kufanya mambo yenye tija. Tuwe kama Nyerere, pamoja na ukristo wake alifanyiwa dua za nguvu na waislamu kipindi cha kutafuta uhuru wa Tanganyika, tena kati ya watu mashuhuri waliomfanyia dua ni Shekeh Ramiya wa Bagamoyo. Nyerere alivyofika kwa Sheikh aliambiwa aungane na waislamu kufunga na yeye akafunga hadi kichwa kikamuuma, alivyofuturu kikapona! Leo mwambie mlokole swafi akafanyiwe duna Sheikhe uone kama hajakwaambia ushindwe. Mwambie muislamu swafi akapige magoti akaombewe na mchungaji uojenmshituko wake.

Hata kuacha kufanya mambo mema kwa kuogopa rafiki zako walevi watakuonaje ni kuishi kienyeji. Badilika! Unachelewa sana. Tenda maajabu!

Umeng'ang'ania kufanya kazi za chini kwa sababu baba zako walifanya kazi hizo za chini. Kwamba maji hufuata mkondo. Unawaenzi. Huo ni ugonjwa. Wakati mwingine siyo lazima tufuate mkondo wa maji hasa kama unakoelekea siko.Tuwe kama Yesu. Ilifikia kipindi akasema “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wanaolisikia neno la Mungu na kulishika” Luka 8:21.

Yawezekana ulizaliwa kuwa mkuu wa wilaya lakini umeng’angania udereva wa malori kisa baba yako alikuwa dereva wa fuso! Huko ni kutenda wema for nothing! Amka ukachukue kiti chako cha Ukuu wa Wilaya. Acha kung'ang'ania nyota ya baba yako. Baba aliendesha fuso kwa sababu ndio fursa aliyoiona wakati huo. Using’ang’anie fursa ya baba yako ukafa maskini. Hebu niambie mtoto wa fundi saa za disco angesomea ufundi saa, leo angetengeneza saa za nani?

Unaogopa kujenga nyumba kijijini kwenu kwamba watakuroga. Bogus kabisa. Jenga wewe hakuna atakayeishi milele. Hata huyo utakayekurogo na yeye atakufa. Kwanza unajiita Mfuasi wa Yesu halafu unaogopa kurogwa. Kweli si kila aitaye bwanabwana anampano wa kwenda mbinguni.

Una pesa nyingi lakini unavaa hovyo, unakula hovyo, unalala hovyo, unasomesha watoto wako katika shule za hovyo na unaonekana mtu hovyo hovyo, kisa tu watu wasijue kama una pesa. Eti unaishi simple! Huko siyo kuishi simple. Huko ni kuishi kienyeji. Tujifunze kutoka kwa Yesu. Ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya haleluyaa. Yesu alikataa kuishi maisha ya jino kwa jino; maisha ya niguse ninuke, maisha ya ukinizungua tunazinguana; akaishi maisha ya samehe saba mara sabini; maisha ya akikunasa kibao shavu la kushoto mgeuzie na la kulia akunase tena, washenzi woteeee wakamshangaa.

Yesu hakuishia hapo tu. Alikula na washenzi, akanywa na washenzi, akawatetea wazinzi na kuwafia washenzi. Enzi zile wazinzi walipigwa mawe lakini Yesu akasema hiyo haikubaliki. Akawaambia kama kuna mtu hajawahi kuzini basi awe wa kwanza kumpiga mawe yule mwanamke mzinzi. Watu wote waliondoka kimyakimya wakiashiria kwamba na wao ni wazinzi.

Assume siku hiyo unamuona na bebi wako naye anaondoka kimyakimya na wakati alikwambia hajawahi kuzini. Ndiyo maana huwa najisema kuna maswali mengine siyo ya kumuuliza bebi wako! Ataishia kukudanganya ufe bure! Eti unamuuliza bebi wako wewe ni mpenzi wake wa ngapi. Hapa kama siyo kutafuta kifo ni nini?

Yesu hakufanya mambo kienyeji ndiyo maana alionekana mtu wa ajabu sana. Hebu piga picha mtihani wa samehe saba mara sabini ulivyomgumu lakini Yesu aliushinda! Pamoja na wale washenzi kumtundika msalabani, kumtemea makohozi, kumvua nguo lakini bado akamwambia Dingi yake awasamehe maana hawajui walitendalo. Tena anasema samehe saba mara sabini. Yaani leo anacheat, unamsahe, kesho anacheat tena, unamsamehe, anacheat anacheat, anacheteat unamsahe, loh! Kweli ni mtihani mgumu. Bila kuushinda huu mtihani ndugu yangu hutoboi, iwe kwenye ndoa, kazi, biashara na kadhalika.

Pamoja na kuwa mwana wa Mungu Yesu aliwaosha miguu wanafunzi wake. Simon Petro alikataa maana siyo utamaduni wao. Ngoja tusome kidogo. … Kisha akatia maji katika bakuli, akaanza kuwatawadha wanafunzi miguu, na kuifuta kwa kile kitambaa alichojifunga. Hivyo yuaja kwa Simon Petro. Huyo akamwambia, Bwana! Wewe wanitawadha miguu mimi? Yesu akajibu, akamwambia, nifanyalo wewe hulijui sasa; lakini utalifahamu baadaye. Petro akamwambia, wewe hutanitawadha miguu kamwe. Yesu akamwambia, kama nisipokutawadha, huna shirika nami…

Baadaye Simon Petro alikubali. Ilikuwa ngumu sana kwa sababu aliishi kienyeji. Mungu atuepushe na dhambi ya kuishi kienyeji maana hata kumuona Mungu kama mtu katili sana, muuaje, asiyekuwa na huruma ni kuishi kienyeji! Inatokea ajali mbaya, inaua watu wote unasema ni mpango wa Mungu; aliyenusurika kwenye ajili hiyo anasema machale yalimcheza. Kwa fikra kama hizo bro, huwezi kutoboa.

Yesu alitoboa kwa sababu alikuja na mtazamo chanya kuhusu Mungu. Alifundisha watu wamuone Mungu kama pendo. Watu wafurahie uumbaji wa Mungu, watu wafurahie dunia, wasiitukane dunia kwamba imeoza. Maisha siyo mapambano. Maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu. Wanapambana wanajeshi.

Msimuogope Mungu. Mpendeni Mungu. Ukifanya ya Mungu; Mungu atafanya yako. Ukifanya ya Shetani; Shetani atafanya yako! Mungu na Shetani hawaingiliani. Muamini Mungu lakini mfunge ngamia wako vizuri ni asije Shetani asimuibe! Acha kuishi kienyeji ufanikiwe. Mafanikio hayaji kwa watu dhaifu. Watu dhaifu ni wale wanaoishi kienyeji.

Utajuaje kama unaishi kienyeji au la. Kipimo ni jamii. Jamii inapokuona mtu wa kawaida sana tambua unaishi kienyeji sana. Ukiwa tofauti tu jamii itajua. Kuna wakati itakuona chizi. Nuhu alionekana chizi pale alipoanza kujenga safina kiangazi, tena jangwani. Daudi alionekana mlevi alipokwenda kupigana na Golithi akiwa na manati.

Unahitaji ukichaa ili kuacha kuishi kienyeji, lakini unahitaji ukichaa kufanya mambo yenye tija alisema Thomas Sankara.
Rusha Sh 20,000 tufunge ofa ya Siku. Mpesa 0753665484!
Ukitaka hardcopy Lipa Sh 10,000 kwa kila kitabu, piga namba hii 0753690907!

Vitabu vyewe hivi hapa!!!!!!
1. Ukombozi wa Fikra
2. Maisha ni Kutafuta siyo Kutafutana
3. Ukombozi wa Fikra za Mwafrika
4. Viongozi wanaoisho baada ya Kufa
5. Wasomi Huru gerezani
6. Fungua ubongo
7. Miamba ya Afrika
8. Fahamu ya ndoa kabla ya

Wako
Mwl. Denis Mpagaze
Muhenga wa Karne ya 21!
 
Vitabu vya dizain hiyo (kwangu mimi binafsi) Hata ukiniambia nilipie sh 100 (shilingi 100) siwezi kulipia.

Zingatia : KWANGU MIMI BINAFSI
 
Back
Top Bottom