Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Tulikuwa wagombea 176, kwa kumbukumbu yangu kuna wagombea maarufu kuliko mimi, matajiri wakubwa, na wengine walikuwa viongozi hadi Mwenyekiti wa CCM wa mkoa, waliambulia kura 0!, akiwemo huyo chawa!.

Ila pia kwenye ugombea, sometimes ni umaarufu wa mtu, naweza kugombea kitu na Joti, nikashidwa!.
P
Mkuu 2025 jaribu tena, huenda ikawa ndio muda sahihi zaidi
 
Kuna watu wanadhani siasa ni blah blah!
Siasa ni sayansi ya siasa inafuata kanuni za kisayansi.
Kwa Tanzania, chama cha siasa kama chama ni chama kimoja tuu!, the one and only!. Sababu ni moja tuu!, ni chama dola! CCM sio tu ni chama tawala, bali pia ni chama Dola!
P
Kweli SIASA ni SAYANSI na SAYANSI imeegemea kwenye NAMBA au IDADI YA WAPIGA KURA. Sasa kwa upande wako, NAMBA hazikukubali au kwa lugha nyingine tunaweza kusema IDADI YA KURA hazikutosha.

Inabidi ujipe muda wa kujitafakari, kwa sababu haitoshi kusema kuwa "CCM INA WENYEWE" ndiyo sababu iliyopelekea wewe kupata kidogo IDADI YA KURA.

CCM ni CHAMA TAWALA na kina wigo mpana wa kupata viongozi wake, sasa inabidi ujichunguze pengine wewe utakuwa na DOSARI.

Pia ulifanya vibaya kuonesha mapema rangi yako ya asili, kwani wengine huwa hawafanyi hivyo mpaka kuhakikisha kuwa wamenufaika na CHAMA TAWALA.

Kitendo cha kuandika hii mada Hivi kweli kuna Mtanzania mwenye akili zake timamu anaweza kuichagua tena CCM, kwa Lipi? halafu utegemee kupata IDADI YA KURA kutoka kwa CCM, ni jambo ambalo lisingewezekana! Hata kupata hiyo KURA MOJA unapaswa kumshukuru MWENYEZIMUNGU.

Angalia mwenzio, leo ni NAIBU WAZIRI lakini sio kwamba hakuona MADHAIFU YA CCM! Aliona na anafahamu vizuri sana, sema wakati mwingine ukitaka kufanikiwa lazima ujifanye MJINGA.
 
Kweli SIASA ni SAYANSI na SAYANSI imeegemea kwenye NAMBA au IDADI YA WAPIGA KURA. Sasa kwa upande wako, NAMBA hazikukubali au kwa lugha nyingine tunaweza kusema IDADI YA KURA hazikutosha.
Yes, it's about numbers and techniques how to get them, huu utaratibu wa kakikundi kadogo la watu fulani kuamua nani awe kiongozi na nani asiwe, mimi nimeuita huu ni ujinga na ndio uliotufikisha hapa tunakosa watu wazuri na kuwapitisha viongozi wa hovyo, mabomu na wengine ni matakata kabisa!, lakini kwasababu they know how to play the games people play kwenye CCM iliyobinafsishwa and get the numbers in their favours kwa kuurefisha mkono ili numbers zitoshe na hata kwenye voting, kura sisipotosha, zinatosheshwa!.
Inabidi ujipe muda wa kujitafakari, kwa sababu haitoshi kusema kuwa "CCM INA WENYEWE" ndiyo sababu iliyopelekea wewe kupata kidogo IDADI YA KURA.
Huko kukubali tuu kuwa CCM ina wenyewe ndiko kujitafakari kwenyewe, kwasababu I know how to play it but I refused to play the dirty games kwa matumaini labda kuna watu wasafi watapokea chochote kitu lakini kwenye kuchagua watawachagua watu wazuri.
CCM ni CHAMA TAWALA na kina wigo mpana wa kupata viongozi wake, sasa inabidi ujichunguze pengine wewe utakuwa na DOSARI.
It's true, nimejichunguza nikajigundua ni kweli ni mimi ndio nina matatizo, mimi ni mkweli too much!, na ni mpenda haki, napenda hata kama ni CCM kushinda viti vyote, ishinde kwa haki!, hivyo I was the odd man out.
Pia ulifanya vibaya kuonesha mapema rangi yako ya asili, kwani wengine huwa hawafanyi hivyo mpaka kuhakikisha kuwa wamenufaika na CHAMA TAWALA.
Ukiwa mkweli toka ndani ya nafsi yako, utasimama na kweli!, mimi nimekuja sio mnyenyekevu!, mimi sio mtu wa ku bow down na kunyamazia ujinga!. Wakati wa kuchukua fomu ya kugombea nikaelezwa lazima kwanza niwaone 'wazee', wanipitishe kata zote 10 za Kawe 'kutambulishwa' kwa wajumbe, na kwenye kila utambulisho lazima wajumbe angalau wapate 'maji ya kunywa' na kuwaachia 'nauli'!. Mimi nikajifariji hakuna mwana Kawe asiyemjua Pasco Mayalla, hivyo sikufanya utambulisho wowote, sikutoa 'maji ya kunywa' kwa wajumbe wala sikutoa senti tano ya 'nauli'!. Hivyo nikavuna nilichopanda!.
Kitendo cha kuandika hii mada Hivi kweli kuna Mtanzania mwenye akili zake timamu anaweza kuichagua tena CCM, kwa Lipi? halafu utegemee kupata IDADI YA KURA kutoka kwa CCM, ni jambo ambalo lisingewezekana! Hata kupata hiyo KURA MOJA unapaswa kumshukuru MWENYEZIMUNGU.
Kwa kweli nimeshukuru hata kwa hiyo kura moja, that means at least there was someone who believes in me!, amekunywa maji ya watu na kupokea nauli ya watu!.
Angalia mwenzio, leo ni NAIBU WAZIRI lakini sio kwamba hakuona MADHAIFU YA CCM! Aliona na anafahamu vizuri sana, sema wakati mwingine ukitaka kufanikiwa lazima ujifanye MJINGA.
Ni kweli, naunga mkono hoja!, kiukweli namuomba sana Mungu anifundishe kunyamaza!, lakini the drivers inside me that pushes me to do something is bigger than sauti inayoniambia kunyamaza!, hii nchi ni nchi ya Watanzania, sio nchi ya mtu yoyote au chama chochote!, hivyo kiukweli kabisa nimeshindwa kuunyamazia ujinga wa systematically ili tuu kulamba asali!.
P
 
Yes, it's about numbers and techniques how to get them, huu utaratibu wa kakikundi kadogo la watu fulani kuamua nani awe kiongozi na nani asiwe, mimi nimeuita huu ni ujinga na ndio uliotufikisha hapa tunakosa watu wazuri na kuwapitisha viongozi wa hovyo, mabomu na wengine ni matakata kabisa!, lakini kwasababu they know how to play the games people play kwenye CCM iliyobinafsishwa and get the numbers in their favours kwa kuurefisha mkono ili numbers zitoshe na hata kwenye voting, kura sisipotosha, zinatosheshwa!.
a554749d8886e656abbc2c65ebdfc90a.png

hivyo kiukweli kabisa nimeshindwa kuunyamazia ujinga wa systematically ili tuu kulamba asali!.
P
Soma huu uzi wa Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana utakusaidia.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la ombi maalum kwa Wana JF wenzangu, nawaombeni sana mnipe pole na msinicheke, wala msinibeze, kujaribu kugombea ubunge wa Kawe kupitia CCM, nimeambulia kura 1!

Japo nimeshindwa kwa kupata kura moja, lakini sababu za mimi kugombea ni very valid na very genuine

Kwanza ni kushukuru kwa yote, hiyo kura moja niliyoipata ni kitu kikubwa sana kwangu, asante sana kwa aliyenipigia kura.

Pili, nimekubali matokeo na kukubali kuwa ama kweli CCM Ina wenyewe!, na wenyewe wenyewe ndio sisi, mimi nikiwemo!. Asiyekubali kushindwa sio mshindani.

Despite the facts ni njia gani wenzangu walizotumia kushinda, the end justifies the means, nawapongeza kwa dhati washindi wote,

Na tatu hili nilisema kwa moyo wangu, sina kinyongo chochote kushindwa, naahidi ushirikiano, na ile ahadi ya kutoa TZS Milioni 100 kwa CCM, nitaitimiza kupitia fund raising na sio kutoka mfukoni kwangu, hivyo naahidi ushirikiano wa dhati na kuendelea kuwa mwanachama mtiifu wa CCM.

Nipeni tu pole!.
Kidumu Chama cha Mapinduzi.
CCM Oye!.

Paskali

Uchaguzi 2020 - Pascal Mayalla aomba kura Kawe, adai akipitishwa atagawa Tshs. Milioni 10 kwa kila Kata

Uchaguzi 2020 - Kawe kunani? Why is a hot cake? Wamejitokeza wagombea 176! What is so special ? Kuchinja watu 175 kubaki 1, is not a joke!.Je, atakuwa nani?

Uchaguzi 2020 - Wingi wa wagombea CCM ni uthibitisho kazi nzuri ya Rais Magufuli kwa taifa letu. Je, Oktoba ni kuchagua au kuthibitisha tu taratibu?

Jimbo gani?
 
Back
Top Bottom