Wana-jf nimefiwa na mke wangu!!

Wana-jf nimefiwa na mke wangu!!

Pole sana mkuu!!Mungu akutie nguvu na ujasiri zaidi uweze pita hayo mapito!!!
 
Hii ni habari ya kusikitisha sana mkuu, lakini maisha ndo yalivyo, leo kwako kesho kwa mwenzio, asnate kwa taarifa na hii itukumbushe kwamba sote tuko njiani. Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya kipenzi chako.
 
Pole sana kaka. Mwenyezi Mungu akupe nguvu. Pole sana.
 
pole sana mkuu
tupo pamoja ktk majonzi mazito uliyonayo

jamani nipeni utaratibu wa kutoa rambirambi maana huyu ni mmoja wa Jf members
 
Pole sana mkuu ni kipindi kigumu hasa kwako na watoto! Mungu awajalie amani yake na kama utahitaji mtu wa kuendelea nawe katika maisha muombe mwenyenz MUNGU akupatie atakae penda watoto wako kama wewe!
 
4f0241f4ac820.gif
 
Ahh looo! Msiba mkubwa, pole sana mkuu. Tunakuombea Mungu awe nawe muda wote akutie nguvu na ujasiri ktk kipindi hiki kigumu.
 
Ohhhh!
Pole sana kwa msiba wewe na familia yako yote.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, na awajalie ujasiri wa kupambana na kipindi hiki kigumu.
 
pole sana mkuu kwa mtihani huu.mungu akujaalie nguvu na faraja wewe na watoto.
 
Pole sana mungu akujalie moyo wa uvumiliv katika kipindi hiki kigumu.
 
Pole sana kamanda, mungu ailaze roho yake peponi
 
Pole sana Mkuu kwa msiba mkubwa uliokufika wa kufiwa na mkeo. Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu kwenu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN.

530489_enlrg.jpg
 
Pole mkuu..Mungu akupe imani na uvumilivu ktk kipindi hiki kigumu..
 
POLE SANA NJENGA...Mungu ailaze roho ya dada mahali pema peponi...nilikutafuta sana kwa simu sikukupata..Nipo Morogoro sikuweza kuja kuhudhuria mazishi...POLE SANA NJENGAAAAAAAA
 
pole sana Mkuu. najua una wakati Mgumu lakini Mungu muweza wa yote atakutia nguvu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen. Mia
 
Pole sana mkuu, sisi tulimpenda sana lakini Mungu kampenda zaidi.
Alale mahali pema peponi, amina!
 
Nasikitika kuwafahamisha kuwa nimepata msiba leo alfajiri mke wangu kipenzi amenitoka. Kimsingi mazishi yamefanyika leo saa 10 kwenye makaburi ya changanyikeni...wife ameniachia watoto wawili wa kike 11 & 8.

saj, pole sana kwa msiba mzito! Mungu akutie nguvu. Rip mama sajent
 
nimepokea taarifa hizi nzito za msiba kwa masikitiko makubwa sana, POLE SANA MKUU MUNGU AKUPE MOYO WA UVUMILIVU
 
Pole sana mkuu SAJENTI, inshallah Mwenyezi akutangulie katika kipindi hiki kigumu kwako na familia yako kwa ujumla. Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, ...........
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom